Prof. Shivji na maoni yake kuhusu kadhia ya Law School

Prof. Shivji na maoni yake kuhusu kadhia ya Law School

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Prof. Shivji ametoa maoni yake kuhusu kadhia ya Law School. Anasema Shivji:

“Pasipo mijadala au ubunifu huwezi kuendeleza fikra, na hii inakwenda moja kwa moja kuathiri usomaji na ufundishaji.”

Prof. Shivji anafahamika kwa misimamo yake. Anachozungumzia hapo ni umuhimu wa critical thinking.

Nguli huyu amesoma na kina Yoweri Museveni na John Garang wakiwa katika ubora wao kama wapigania uhuru.

Nguli huyu mwandishi wa makala zake tata kama Ile ya "what is left to the left of the university of Dar es Salaam," haipo shaka kuwa atakuwa analiangalia tatizo la LST kwa mapana yake zaidi.

Atakuwa anawanyooshea vidole waliouwa na wanaouwa critical thinking mashuleni. Iliyokuwa academic freedom Leo Iko wapi?

Nguli Shivji radical kama alivyo haitakuwa ajabu kama atakuwa ana shangaa:

1. Ni vipi wanafunzi vyuo vikuu (ikiwamo UDSM na hasa faculty of law) wamelala hivi kuhusu katiba mpya na haki mbali mbali zinazoendelea kusiginwa.

2. Ni vipi wanafunzi LST wakijua mtaji wa maskini ni nguvu zao wenyewe waliendelea kusubiria kufeli mwaka hadi mwaka na kuwa 'at the mercy' ya hao wanaowatuhumu, kiasi cha kufikishwa huku tuliko sasa?

4. Ni vipi viongozi wa upinzani wamekuwa wakikamatwa, kubambikiziwa kesi hali vyama vya wanafunzi wakiwa hawana hata la kusema?

5. Ni vipi watuhumiwa wamekuwa wakiuwawa kinyume cha sheria, hali wanafunzi hawa wakiwa wamegeuka kuwa wapenzi watazamaji?

6. Ni vipi tozo za Mwigulu zimekuja na kutamalaki bila wanafunzi kujihusisha kwenye uhalali na uharamu wake?

7. Vipi haya ya magari ya mabilioni ya shilingi kila mwaka kwa ajili ya kununulia magari ya vigogo serikalini kutohojiwa na wanafunzi?.

8. Vipi ya haki za vyama vya siasa kuzuiwa kufanya siasa. Wanafunzi wanaangalia tu?

9. Nk nk.

Iko kwenye record wakati Prof Shivji akiwa mwanafunzi UDSM serikali ya Nyerere ililwaho kuleta malori ya jeshi kuwachukua wanafunzi kwenda kusafisha Jiji, wanafunzi 12 peke yao walisimama imara kulipinga Hilo.

Hawa walitandaza mbao zenye misumari kuyazuia malori kuondoka.

Katika 12 hao walikuwamo Shivji, Garang na Museveni.

Hazipo tena siku zile ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu walishurutisha madaktari waliokamatwa wakidai madai yao kuachiwa mara moja kutoka segerea?

"Nini kimetokea? Jibu ni kuwa kuporomoshwa kwa critical thinking mashuleni kwa mujibu wa nguli huyu."

Yasipotoshwe maoni ya Prof. nguli Issa Shivji.

Source:
Profesa Shivji asema tatizo ni mfumo ufaulu mtihani Uanasheria
 
Ajabu, mpaka pale ambapo walimu wanaotakiwa kuwa chemchem za fikra mpya nao wanageuka wenye mawazo mgando.

Hawa nao wanarithisha hayo mawazo mgando kwa wanafunzi wao, kuwaaminisha wanaofeli Law School hawasomi, au hawajaandaliwa vizuri kule walikotoka.

Huyu mwanafunzi anamaliza masomo yake Law School kwa kusherehekea na wazazi wake, huku kichwani akiwa amebeba mawazo mgando kuwahusu wale waliofeli.

Matokeo yake, huyu ndie anaenda mahakamani kumtetea mteja mwenye kesi mpya, ikiwa mwaka mzima aliokaa Law School alishindwa kujiuliza nini sababu ya wanafunzi wengi kufeli na kupata majibu yake sahihi, tofauti na yale yakuambiwa.
 
Hayo uliyoandika ndiyo maoni yake? Maana ume quote aya moja kisha umeendelea na uchambuzi wako, hayo ndiyo maoni yake?

Iko paragraph moja tu yenye maoni yake. Kwa maana hiyo nimechukua maoni yake yote.

Nimeeleza Shivji kama mwanafunzi, kama mwanazuoni nguli.

Nimeonyesha makala zake na associates wake.

Haipo shaka Shivji anashangaa na ineptness iliyopo kwa watu kushindwa kupigania haki zikiwamo zao wenyewe. Kwani sakata la LST limeanza lini?

Kwa nini hawakukomaa hata kuwafungia hao ma don nje ya compound ya chuo?
 
1. Ni vipi wanafunzi vyuo vikuu (ikiwamo UDSM na hasa faculty of law) wamelala hivi kuhusu katiba mpya na haki mbali mbali zinazoendelea kusiginwa.

2. Ni vipi wanafunzi LST wakijua mtaji wa maskini ni nguvu zao wenyewe waliendelea kusubiria kufeli mwaka hadi mwaka na kuwa 'at the mercy' ya hao wanaowatuhumu, kiasi cha kufikishwa huku tuliko sasa?

VIJANA WA TANZANIA KUANZISHA JUKWAA LAO HURU, NDIYO JIBU LA KUPATA NAFASI YA KUSHIRIKISHWA KTK NGAZI YA MAAMUZI KITAIFA

Duniani ni vijana wa vyuo vikuu ndiyo wanaoongoza kuchagiza mageuzi

Historia inaonesha mara baada ya uhuru wa kwanza kupatikana ktk mtaifa mbalimbalii iwe kwa mtutu wa bunduki au maandamano ya kuondoa wakoloni, baadaye kulifuatia msuguano wa wananchi wenyewe kwa wenyewe kwa kutoridhishwa na wale waliochukua utawala toka kwa wakoloni.

Sababu mbalimbali zilizua msuguano ktk nchi huru kama udiktekta, tawala kamdamizi ya chama kimoja, utawala mbovu, ubaguzi wa kielimu mfano mtoto aliyesoma shule za kata / st. Kayumba anadanganywa kuwa akihitimu chuo kikuu atakuwa na nafasi sawa na mwenzake aliyesoma St. Mary's akamaliza elimu ya chuo kikuu pia anayekimanya kiingereza / kispaniola vizuri zaidi na wajomba wake wapo ktk nafasi za kiutawala n.k

Vijana wengi pamoja na umasikini wa familia zao wanashawishiwa kwenda vyuo vikuu kwa kuchukua mikopo wakiwa na matumaini ambayo ni hadaa kuwa kwa kumaliza elimu ya juu watakuwa sawa na wale watoto wa tabaka la watawala anasema kiogozi wa vuguvugu la wanafunzi wa chuo kikuu wa Chile kamanda Gabriel Boric mwaka 2017.

Hapo ndipo Wanafunzi waliopo ktk nchi kama Sudan, Chile, Cuba, Afrika ya Kusini, Kenya walishiriki kudai mageuzi ili kuondokana na tawala zilizomgoa mkoloni.

Tanzania vijana hawajishughulishi kuhoji mambo yasiyowaridhisha wananchi kama matumizi mabaya ya kodi za wananchi, tozo ziluxokifu wananchi, demokrasia kubinywa, katiba kandamizi n.k

Chile nchi iliyo na kiongozi kijana Gabriel Boric ambaye ndiye rais kijana kabisa wa kuchaguliwa amezaliwa 11 February 1986 ambaye alichukua madaraka ya urais tarehe 11 March 2022 baada ya kushinda uchaguzi mkuu nchini Chile tarehe 19 December 2021 kwa kupata asilimia 60% ktk uchaguzi wa urais.

Gabriel Boric on the Chilean student movement 14 June 2017

Gabriel Boric on the Chilean Student Movement

Likes
59,554
Views
2017
14 Jun
In a presentation at the School of Public Policy on June 7, 2017; Gabriel Boric offers a historical perspective and reflects on lessons learned. He focuses especially on the role of social movements in a well-developed democracy and provides insights on how to sustain collective action over an extended period of time. He speaks also about his transition from being a member of a political movement to being a member of Parliament. Gabriel Boric is a Chilean parliamentarian, and a former leader of the national student movement. He was the president of the Student Federation of the Universidad de Chile, one of the most important student unions in the country. Boric currently represents the Magallanes and Antarctic Region in Chile’s Chamber of Deputies. He was elected as an independent candidate and is not associated with either one of the two political coalitions that have traditionally dominated politics in Chile. Source:

Department of Public Policy at CEU​

Mwanafunzi wa chuo kikuu toka familia masikini anazama ktk mkondo wa madeni ya fedha za mkopo wa elimu ya juu huku akiwa na matumaini potofu ya kupata ajira au kuwepo mazingira hewa ya kujiajiri.


Vijana vyuo vikuu na mijini pia vijijini badala ya kumezwa na ukiritimba wa UVCCM na ahadi kuwa ni viongozi wa kesho huku watoto wa vigogo wa CCM wanapewa nafasi sasa na siyo kesho wanatakiwa kuunda chombo chao kipya cha kutambulika kama mdau muhimu anayehitaji kuonekana katika majukwaa ya siasa pia ktk vituo vya redio, televisheni na mitandao ya kijamii kuchagiza mabadiliko na mageuzi ikiwemo pia kupewa nafasi nje ya mfumo wa vyama ili wagombee nafasi za kuchaguliwa na wananchi.


Gabriel Boric - The 100 Most Influential People of 2022 - TIME

time.com › collection › gabriel-boric

gabriel boric presidente from time.com
23 May 2022 · He is making Chile the social, economic, and political laboratory of the world once again. Stiglitz is a Nobel Prize–winning economist
 
Kwani wewe na Chadema mmelifanyia nini Taifa Hili?

Mkuu mimi na uliowataja kwa kukataa kuporwa critical thinking yetu tumeendelea kuhoji na kupigania haki na bila woga.

Ni kitu gani kilicho bora kuliko hayo.

Kama yalivyo pale hata Shivji hatushangai sisi, ila ninyi.
 
Mkuu mimi na uliowataja kwa kukataa kuporwa critical thinking yetu tumeendelea kuhoji na kupigania haki na bila woga.

Ni kitu gani kilicho bora kuliko hayo.

Kama yalivyo pale hata Shivji hatushangai sisi, ila ninyi.
Mmehoji nini?

Mmepigania nini iwapo miaka 30 ya Uhai wenu mnashindwa kufanya mikutano?

Mnahojia wapi ikiwa hata Bungeni na Kwenye mabaraza ya madiwani hampo?
 
Mmehoji nini?

Mmepigania nini iwapo miaka 30 ya Uhai wenu mnashindwa kufanya mikutano?

Mnahojia wapi ikiwa hata Bungeni na Kwenye mabaraza ya madiwani hampo?

Mkuu:

1. tunadai "katiba mpya" kwa vitendo.
2. Tuko bega kwa bega na wahanga wote kwa ajili ya haki zao.
3. Nk nk kama ilivyoorodheshwa kwenye mada kwa anayoshangaa Shivji.

NIsiache kukuasa hata wajukuu wenu watawadhangaa.

Hongera Pascal Mayalla kwa kukaa kwa kutulia.
 
Wamefanikiwa kujaza wahuni kule twiter kutwa nzima kuibeza serikali ,Hawa wahuni wanaongozwa na mtu mzima Lema

Ungetuwekea japo ka ushahidi kidogo tuone. Nani asiyejua kwenu kudai haki ni tusi?
 
Mkuu:

1. tunadai "katiba mpya" kwa vitendo.
2. Tuko bega kwa bega na wahanga wote kwa ajili ya haki zao.
3. Nk nk kama ilivyoorodheshwa kwenye mada kwa anayoshangaa Shivji.

NIsiache kukuasa hata wajukuu wenu watawadhangaa.

Hongera Pascal Mayalla kwa kukaa kwa kutulia.
Acha kituaminisha kuwa tatizo la nchi ni katiba
 
Wengine tunaona tatizo la nchi hii ni katiba. Wacha kudhani kuona kwenu tu ndiko kuliko sahihi.
Katiba inazuwiaje nchi kusonga mbele na Katiba unayoitaka itasaidiaje nchi kwenda mbele!?...yaani iondoe ujinga,umasikini na maradhi
 
Katiba inazuwiaje nchi kusonga mbele na Katiba unayoitaka itasaidiaje nchi kwenda mbele!?...yaani iondoe ujinga,umasikini na maradhi

Mambo mengi muda mchache. Sikujua kuwa kumbe ulifurukuta. battawi ana ujumbe kwako:

Screenshot_20230427-113556.jpg


Watanzania wajinga na kuvuna wanayopanda
 
Kwanza kabisa ninai blast tume ya Harrison Mwamwembe haikufanya lolote la kusaidia matatizo ya Law School. Mwamkyembe ni FAILURE katika ku deliver issues kama hizi. Kumbuka ripoti yake ya RICHMOND na Treni ya Metro aliyomleta Tapeli Shumake kutoka Chicago

Najielekeza kwenye hoja yangu sasa.

Gharama ya Law School of Tanzania kwa kwa mwanafunzi kwa mwaka Tsh. 3,000,000.

3,000,000 * 821 = 2,463,000,000

Kwenye udahili wa wanafunzi 821, unafaulisha wanafunzi 23 tu, halafu tunaona hii ni sawa?

Kirahisi kabisa tunaindividualize kwa kusema “wanafunzi hawana uwezo” halafu imeishia hapo

Mimi siyo mwanasheria wala sina masilahi, lakini hawa lecturers na management ya Law School wanafanya mzaha na biashara tu

Pendekezo:
Tufanye kama shule za RC (St Francis, Marian etc) ambapo wanaomba 1,000 na kulipia fomu kwa Tshs 10,000 tu halafu kwenye NECTA baada ya miaka 4 unakuta wanafaulu Div 1 na II pekee.

Kwa muktadha huo nashauri uanzishwe mfumo wa entry exam au matriculation exam ambapo watachukua wanafunzi wenye uelewa na wanaofundishika tu. Hii italeta faida zifuatazo:-

1. itaokoa muda na fedha za wanafunzi wanaofeli kwenye mtihani wa mwisho.

2. Lecturers watapata muda wa kutosha wa kufundisha wanafunzi kwa nafasi.

3. Watajuwa kuwa mshahara wao unatokana na kufaulisha wanafunzi hivyo watajituma zaidi ili wapate mishahara itokanayo na karo zao
 
Back
Top Bottom