- Thread starter
- #21
Kwanza kabisa ninai blast tume ya Harrison Mwamwembe haikufanya lolote la kusaidia matatizo ya Law School. Mwamkyembe ni FAILURE katika ku deliver issues kama hizi. Kumbuka ripoti yake ya RICHMOND na Treni ya Metro aliyomleta Tapeli Shumake kutoka Chicago
Najielekeza kwenye hoja yangu sasa.
Gharama ya Law School of Tanzania kwa kwa mwanafunzi kwa mwaka Tsh. 3,000,000.
3,000,000 * 821 = 2,463,000,000
Kwenye udahili wa wanafunzi 821, unafaulisha wanafunzi 23 tu, halafu tunaona hii ni sawa?
Kirahisi kabisa tunaindividualize kwa kusema “wanafunzi hawana uwezo” halafu imeishia hapo
Mimi siyo mwanasheria wala sina masilahi, lakini hawa lecturers na management ya Law School wanafanya mzaha na biashara tu
Pendekezo:
Tufanye kama shule za RC (St Francis, Marian etc) ambapo wanaomba 1,000 na kulipia fomu kwa Tshs 10,000 tu halafu kwenye NECTA baada ya miaka 4 unakuta wanafaulu Div 1 na II pekee.
Kwa muktadha huo nashauri uanzishwe mfumo wa entry exam au matriculation exam ambapo watachukua wanafunzi wenye uelewa na wanaofundishika tu. Hii italeta faida zifuatazo:-
1. itaokoa muda na fedha za wanafunzi wanaofeli kwenye mtihani wa mwisho.
2. Lecturers watapata muda wa kutosha wa kufundisha wanafunzi kwa nafasi.
3. Watajuwa kuwa mshahara wao unatokana na kufaulisha wanafunzi hivyo watajituma zaidi ili wapate mishahara itokanayo na karo zao
Kuna mbuzi watu kama hili Ujamaa ni mhimu ujuaji mwingii! Kutokea kwenye zile kazi zaitwa za laana hayawezi kukuelewa.