Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
PROF. SHIVJI AMWELEZA MWALIMU NYERERE
Ilikuwa siku ya uzinduzi wa nyumba ya Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere baada ya kufanyiwa ukarabati.
Baada ya uzinduzi wadau wa historia ya Mwalimu Nyerere tulijumuika kuzungumza.
Kabla ya shighuli hii nilitembelewa na maofisa wa nyumba hii ya kumbukuzi wakaniambia kuwa wameelekezwa kwangu na watu ili niwape historia ya Mwalimu.
Nilitumia nafasi ile kurekebisha baadhi ya makosa katika historia ya Mwalimu na nyumba ile ya Magomeni Mtaa wa Ifunda.
Maofisa wa nyumba ya kumbukizi walikuwa wakiwaeleza watu kuwa nyumba hii ya Nyerere imebeba siri kubwa ya historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika kwa kuwa hapo ndipo walipokuwa wakikutana viongozi wa TANU.
Niliwaeleza kuwa haikuwa kweli.
Nyumba iliyokuwa ndiyo makutano ya wanaharakati wa TANU toka enzi za TAA ilikuwa Kariakoo, Mtaa wa Aggrey na Sikukuu nyumbani kwa Abdul Sykes.
Nikawaeleza kuwa Nyerere aliishi nyumba hiyo kabla ya kuhamia Magomeni Maduka Sita si mbali na alipojenga nyumba hiyo ya Mtaa wa Ifunda.
Nyerere alihamia Magomeni Maduka Sita mwaka wa 1955 baada ya kuacha kazi ya ualimu.
TANU ilimtafutia nyumba hapo na sababu kubwa Ramadhani Aziz mdogo wake Dossa Aziz tayari alikuwa amepanga hapo na alikuwa na duka.
Rafiki zake Nyerere hawakutaka Nyerere aishi peke yake waliona pale kwa kuwa yuko Ramadhani Aziz atakuwa anamtupia jicho Nyerere na mkewe Mama Maria.
Siku hizo Mwalimu alikuwa mgeni hana mtu anaemjua.
Hawa maofisa walishangaa sana.
Haya hawakuyajua.
Nikawaongezea kuwa huwezi kueleza historia ya nyumba ya Mwalimu bila kutaja nyumba ya Ali Msham Mtaa wa Jaribu.
Mama Maria alikuwa akishinda kwenye nyumba hiyo akifanya biashara ya kuuza mafuta ya taa.
Nyumba hii ilikuwa tawi la TANU alilofungua Ali Msham na akampa sehemu Mama Maria atarazak.
Nikawaeleza kuwa Nyerere alijenga nyumba hiyo ya Mtaa wa Ifunda na kuhamia mwaka wa 1958.
Mwalimu hakuishi muda mrefu hapo serikali ya kikoloni ikampa nyumba Sea View.
Hii ilikuwa baada ya ushindi wa Kura Tatu na TANU iko ndani ya LEGCO Baraza la Kutunga Sheria la Waingereza.
Katika video hiyo hapo chini kijana Mzee Salum Khamis anaeleza vizuri historia ya eneo hilo.
Mzee ni kitukuu cha Chief Mohosh (Affande Plantan) kwa upande wa mama yake Bi. Maunda Plantan na nyumba yao iko jirani na nyumba aliyoishi Mwalimu.
Naamini wengi mnaifahamu historia ya Hermann von Wissmann na Abushiri bin Salim na jeshi la Wazulu chini ya Chief Mohosh Shangaan lililoletwa kutoka Imhambane, Mozambique kupigananae.
View: https://youtu.be/LYKo4repf-g?si=9_kB3Ne4mKH1Yn0B