Prof. Tibaijuka: Kwa sheria ya Mipango Miji ilitakiwa Viwanja 4 vya high density viunganishwe mbele na nyuma kujenga ghorofa Kariakoo!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mbobezi wa Makazi duniani Prof Tibaijuka amesema pale Kariakoo Kwa mujibu wa sheria ya Mipango Miji ilitakiwa Viwanja 4 vya High density viunganishwe mbele na nyuma Ili Kujenga ghorofa

Nimeogopa sana Kwa yale maghorofa ya Kikinga yaliyojaa Kariakoo na Manzese

Baadae Mlale unono 🐼

----
POLENI WAHANGA WA GHOROFA lililoanguka ila Ujenzi wa maorofa Kariakoo. NI JANGA KAMA LA JANGWANI.
Kwa sheria za mipango miji ilitakiwa viwanja 4 vya high density viunganishwe mbele na nyuma kipatikane kiwanja kimoja kikubwa cha kujenga orofa imara yenye basement kubwa kupaki magari. Orofa inayofunguka kwenye mtaa wa mbele na nyuma.

Awali katika awamu ya Tatu Ushauri huo wa watalaamu wa mipango miji ulishapuuzwa na viongozi kwa presha ya wawekezaji kwa hiyo maorofa Kariakoo na kwingineko yanajengwa kiholela kwenye viwanja visivyokidhi vigezo. Pamoja na madhaifu ya usimamizi wa UJENZI KIUHANDISI Ni vigumu majengo kuwa imara bila kuwa na eneo la kutosha kujenga kitako yaani base foundation stahiki. Naendelea kuhimiza kurekebisha kosa hilo.

Sasa tunavuna hasara kubwa ya upotevu wa mali.. na maisha na fursa za ajira na aibu ya kushindwa kusimamia viwango vya ujenzi Miaka 63 baada ya uhuru.. Tuwaombee wahanga auheni na waliopoteza maisha pumziko la milele.

Naendelea kushauri viwango vya vertical development vizingatiwe kuanzia sasa. Tujisahihishe.
 
Huyu mama baada ya kuwa nje ya mfumo ndo anaongea kama Professor wa ukweli.
 
Mbobezi wa Makazi duniani Prof Tibaijuka amesema pale Kariakoo Kwa mujibu wa sheria ya Mipango Miji ilitakiwa Viwanja 4 vya High density viunganishwe mbele na nyuma Ili Kujenga ghorofa

Nimeogopa sana Kwa yale maghorofa ya Kikinga yaliyojaa Kariakoo na Manzese

Baadae Mlale unono 🐼
Sio lazima. Japan, New York n.k. wanajenga skyscrapers katika maeneo madogo .
Kinachotakiwa ni kuwa na miongozo pamoja usimamizi bora wa ujenzi. Hizi zote ni kazi za Halmashauri. Ingawq technically unaweza kujenga ghorofa refu katika eneo dogo ni mahitaji mengine ndio yatakusumbua. K.m. ghorofa inavyokuwa ndefu, unahitaji lifti na ngazi za dharura za kutosha hivyo unaweza kukuta sehemu utakayoweza kutumia ikawa ndogo na hivyo kuifanya isilipe. Hivyo tatizo letu kubwa ni kuwa hatuna nia ya dhati ya kusimamia ujenzi wa maghorofa.

Wakati tunashupalia kuanguka kwa jengo inabidi pia tujiulize maji taka yote yanayotoka vyooni, kwenye mabafu, jikoni n.k. yanaenda wapi?

Amandla...
 
POLENI WAHANGA WA GHOROFA lililoanguka ila Ujenzi wa maorofa Kariakoo. NI JANGA KAMA LA JANGWANI.
Kwa sheria za mipango miji ilitakiwa viwanja 4 vya high density viunganishwe mbele na nyuma kipatikane kiwanja kimoja kikubwa cha kujenga orofa imara yenye basement kubwa kupaki magari. Orofa inayofunguka kwenye mtaa wa mbele na nyuma.

Awali katika awamu ya Tatu Ushauri huo wa watalaamu wa mipango miji ulishapuuzwa na viongozi kwa presha ya wawekezaji kwa hiyo maorofa Kariakoo na kwingineko yanajengwa kiholela kwenye viwanja visivyokidhi vigezo. Pamoja na madhaifu ya usimamizi wa UJENZI KIUHANDISI Ni vigumu majengo kuwa imara bila kuwa na eneo la kutosha kujenga kitako yaani base foundation stahiki. Naendelea kuhimiza kurekebisha kosa hilo.

Sasa tunavuna hasara kubwa ya upotevu wa mali.. na maisha na fursa za ajira na aibu ya kushindwa kusimamia viwango vya ujenzi Miaka 63 baada ya uhuru.. Tuwaombee wahanga auheni na waliopoteza maisha pumziko la milele.

Naendelea kushauri viwango vya vertical development vizingatiwe kuanzia sasa. Tujisahihishe.
 
Mbobezi wa Makazi duniani Prof Tibaijuka amesema pale Kariakoo Kwa mujibu wa sheria ya Mipango Miji ilitakiwa Viwanja 4 vya High density viunganishwe mbele na nyuma Ili Kujenga ghorofa

Nimeogopa sana Kwa yale maghorofa ya Kikinga yaliyojaa Kariakoo na Manzese

Baadae Mlale unono 🐼
kwan Prof.amegundua hilo lini kwa mfano gentleman?🐒
 
Back
Top Bottom