Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Aliyewahi kuwa Mbunge wa Muleba Kusini na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, amesema kuzuiwa kwa mgombea binafsi nchini kumeifanya Tanzania kuwa na demokrasia ya udikteta wa vyama.
Ameyasema hayo leo Septemba 14, 2024 alipokuwa akitoa mada ya ushiriki wa wanawake katika siasa katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Demokrasia, iliyoandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na kufanyika Chuo Kikuu cha cha Dar es Salaam.
"Kwa nchi hii kuna tatizo. Katiba yetu inasema kama unataka kugombea ni lazima ujiunge na chama na hilo ni kwa kila mtu, kwa hiyo hapa tuna demokrasia ya vyama lakini ni udikteta wa vyama. Ni kwa nini mgombea huru asiruhusiwe?" amehoji.
Profesa Tibaijuka aliyekuwa akitoa mada kuhusu ushiriki wa wanawake katika siasa, amesema hicho ni kikwazo kwa kundi hilo. "Hili ni tatizo ambalo Rais Samia kama ataweza afanye marekebisho ili aruhusu wagombea huru. Itasaidia wanawake na wanaume na Watanzania kuboresha ongozi wa siasa," amesema.
Amesema hofu iliyopo miongoni mwa vyama vya siasa ni kusambaratika, endapo mgombea binafsi ataruhusiwa, jambo alilosema si sahihi.
"Mbona Marekani havijapotea? Unaweza ukawa Democratic au Republican na unaweza kuwa huru. Hivyo ndivyo unavyoweza kuimarisha vyama, " amesema na kuongeza: "Hapa unyanyasaji wa viongozi watarajiwa unatokana na kuwanyima uhuru wagombea binafsi. Unajua wananchi wanapopiga kura, wananchi hawapigii chama, wanampigia mtu. Kwa hiyo vyama vimewafunga watu wenye mawazo tofauti, kwamba wakae kweye msimamo wa chama"