TANZIA Prof. Wamba Dia Wamba afariki dunia

TANZIA Prof. Wamba Dia Wamba afariki dunia

Mkuu kumbe wewe ni mhenga ila unaleta mambo ya kidwanzi kabisa hapa JF? Kuanzia leo itabidi nikupe heshima kwa umri wako hata kama utaongea mambo yako ya ushabiki wa kipuuzi.

JF mtu si anaweza kuandika lolote hata kudai yeye ndiye alikuwa mwalimu wa marehemu?

Kama huyu maugonjwa ni graduate, usomi hauna maana tena.

Labda ndiyo maana kina Bashite wanaendelea kudunda na labda hata kigamboni baso wakapenya kiroho safi na bila hata ya mzengwe.
 
R.I.P Pof.

Nakumbuka kamati yetu ya Free Wamba dia Wamba pale Mlimani iliyoongozwa na Prof. Ken Edwards (Mghululi) R.I.P, Prof. Horace Campbell, na Eberhard Chambulikazi R.I.P.
Hizo zilikuwa enzi.
My Boss Mr Chambulikazi R.I.P
 
Wow! Seriously? Lini?

Hapo naona nilipitwa....

Kolo na James nimesoma nao pale vidudu enzi hizo....

Mzee Wamba akija kuwachukua tulikuwa tunamuamkia ‘shkamoo’ na yeye anatujibu ‘good afternoon’.

Kuhusu Kimambo rejea tamko hilo hapo juu kwenye linki ya kwanza.

Kuhusu Luanda, sikumbuki mwaka ila ndani ya miaka miwili mitatu.

Naam, Profesa Wamba kwa kweli Kiswahili kiliendelea kumpiga chenga, cha ajabu alijifunza Kikemeti na akakiweza.
 
Wow! Seriously? Lini?

Hapo naona nilipitwa....

Kolo na James nimesoma nao pale vidudu enzi hizo....

Mzee Wamba akija kuwachukua tulikuwa tunamuamkia ‘shkamoo’ na yeye anatujibu ‘good afternoon’.
James na Mzee wake Mara mwisho walikua wanakaa Mikocheni B

James kn kipindi alikua ana promoti ngumi nadhani
 
Dah! Majonzi tele.

Wakongwe wa ile idara wanapukutika.

Nadhani waliobaki kwa sasa ni Josephat Mbwiliza, Isaria Kimambo, Nestor Luanda, na Frederick Kaijage.

Mishambi, Tambila, Mlahagwa, na sasa Wamba...wote ni marehemu!

Pumzika kwa amani jirani!
Professor mbwiliza aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa miaka ya zamani nimefanya naye kazi. Ameshastaafu. nimewahi kukutana naye posta mwaka 2018 and he was health and energetic.
 
Back
Top Bottom