Profesa aliyejiuzulu chuo cha Cambridge, Jason Arday akutwa amefariki ndani

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Professor wa chuo cha Cambridge aliyejiuzulu wiki iliyopita baada ya kukabiliwa na tuhuma za udanganyifu wa kitaaluma (plagiarism) pamoja na kuandamwa na vyombo vya habari amekutwa amefariki dunia Siku ya jana Agosti 14, 2026.

Jason Arday, ambaye akiwa na umri wa miaka 37 mnamo mwaka 2023 alikuwa profesa mweusi wa kwanza mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kupata nafasi hiyo katika Chuo Kikuu cha Cambridge, alijiuzulu kufuatia shinikizo kubwa la vyombo vya habari. Shinikizo hilo lilichangiwa na wiki kadhaa za tuhuma za kunakili kazi za taaluma za watu wengine, pamoja na maswali yaliyoibuka kuhusu ukweli wa mafanikio yake

Soma Profesa Mweusi wa Kwanza Chuo Kikuu Cha Cambridge, Uingereza Ajiuzulu kwa Kashfa ya Udanganyifu wa Kitaaluma (Plagiarism)

Magazeti ya The Times na Telegraph, pamoja na mashirika ya habari ya BBC na Sky News, yameripoti kuwa Arday, mwenye umri wa miaka 41, alikutwa tayari amefariki ndani ya nyumba moja eneo la Battersea, kusini mwa London, Ijumaa alasiri.

----------------
My take
Kupitia Mitandao ya kijamii, habari za kifo cha Jason Arday zimehuzunisha wengi, huku wengi wakizua madai na kunyoosha vidole dhidi ya namna vyombo vya habari vilisambaza taarifa za Jason bila utu, pia wengne wamehoji Chuo kikuu cha Cambridge kushare taarifa binafsi za kazi kuhusu Mfanyakazi wao

Hata hivyo bado wengine wamezua mjadala wa ubaguzi wa rangi

1786779723185.png

Source: AP NEWS & CNN
 
Social media bullying ni mbaya sana, ukianikwa mitandaoni na kila siku unasulubiwa unaweza kunywa sumu maana hata kutoka nje huwezi tena.

Hii dunia ni bora usiwe maarufu utaishi maisha bila pressure ya jamii nzima.
 
His lies caught up with him akashindwa kuvumilia all the dram that came with it.

Angevumilia kidogo tu upepo ungebadilika akaendelea na mambo mengine 🙇🏾
Tatizo la USA ni cancel culture, yaani hapo wafadhili wake wote walijitoa, wanafunzi wake tu walikua njiani kumfungulia kesi ya madai awalipe fidia kwahiyo kinachofuata angefilisika kabisa.

Ingekua huku Afrika ndio upepo ungepita chap na maisha yangeendelea
 
He was guilty of plagiarism and the allegations were confirmed to be legitimate and this might be the reason that led to his untimely demise.
 
Professor wa chuo cha Cambridge aliyejiuzulu wiki iliyopita baada ya kukabiliwa na tuhuma za udanganyifu wa kitaaluma (plagiarism) pamoja na kuandamwa na vyombo vya habari amekutwa amefariki dunia Siku ya jana Agosti 14, 2026.

Jason Arday, ambaye akiwa na umri wa miaka 37 mnamo mwaka 2023 alikuwa profesa mweusi wa kwanza mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kupata nafasi hiyo katika Chuo Kikuu cha Cambridge, alijiuzulu kufuatia shinikizo kubwa la vyombo vya habari. Shinikizo hilo lilichangiwa na wiki kadhaa za tuhuma za kunakili kazi za taaluma za watu wengine, pamoja na maswali yaliyoibuka kuhusu ukweli wa mafanikio yake

Soma Profesa Mweusi wa Kwanza Chuo Kikuu Cha Cambridge, Uingereza Ajiuzulu kwa Kashfa ya Udanganyifu wa Kitaaluma (Plagiarism)

Magazeti ya The Times na Telegraph, pamoja na mashirika ya habari ya BBC na Sky News, yameripoti kuwa Arday, mwenye umri wa miaka 41, alikutwa tayari amefariki ndani ya nyumba moja eneo la Battersea, kusini mwa London, Ijumaa alasiri.

----------------
My take
Kupitia Mitandao ya kijamii, habari za kifo cha Jason Arday zimehuzunisha wengi, huku wengi wakizua madai na kunyoosha vidole dhidi ya namna vyombo vya habari vilisambaza taarifa za Jason bila utu, pia wengne wamehoji Chuo kikuu cha Cambridge kushare taarifa binafsi za kazi kuhusu Mfanyakazi wao

Hata hivyo bado wengine wamezua mjadala wa ubaguzi wa rangi

Source: AP NEWS & CNN
Wazungu mambo madogo yanawaua? Sheikh wangu Walid uongo wao umekwisha
 
Tatizo la USA ni cancel culture, yaani hapo wafadhili wake wote walijitoa, wanafunzi wake tu walikua njiani kumfungulia kesi ya madai awalipe fidia kwahiyo kinachofuata angefilisika kabisa.

Ingekua huku Afrika ndio upepo ungepita chap na maisha yangeendelea
Kwanini awalipe?
 
Kwanini awalipe?
Umepata udaktari kwa uongo hivyo unachowafundisha kinakua na mashaka kama ni halisia.

Wengine pia wanasema wameathirika kisaikolojia sababu ya "kudanganywa" na kulaghaiwa na professor huyo.
 
Back
Top Bottom