Profesa Assad ahoji usiri wa uuzaji Nyumba za Serikali

Profesa Assad ahoji usiri wa uuzaji Nyumba za Serikali

Sakata la uuzaji wa nyumba za Serikali limeibuliwa upya na aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Musa Assad akikosoa utaratibu uliotumika kuziuza.

Dodoma. Utaratibu uliotumika kuuza nyumba za Serikali umekosolewa kutokana na kutolihusisha Bunge kama chombo cha wawakilishi wa wananchi.

Hayo yameelezwa na aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), Profesa Musa Assad ambaye amesema mchakato huo ulihusisha Baraza la Mawaziri na Makatibu wakuu huku Bunge likiwekwa pembeni.

Akizungumza kwenye mdahalo ulioandaliwa na Mtandao wa Asasi za kiraia uliojikita katika kuchagiza uwajibikaji kwenye uziduaji (Hakirasilimali) katika wiki ya Azaki inayofanyika mjini Dodoma.

Amesema Serikali imeuza nyumba hizo na mchakato ulikuwa ni baraza la mawaziri wakishauriwa na makatibu kutengeneza waraka na kupeleka kwa Rais ili akubali kuuza nyumba hizo.

“Nani kakuruhusu? Ni mawaziri na makatibu wakuu. Kwanini halizungumzwi sasa jambo hilo. Lingekuwa wazi tungesema hilo haliwezekani lakini tumekaa kimya na hakuna mtu ambaye amesema hili jambo lazima lirudi bungeni tulizungumze ili tutoe ruhusa maalum jambo hili lifanyike ama lisifanyike,” amesema Profesa Assad

Chanzo: Mwananchi
Huyu mpuuzi tu,
Aliponunua nyumba za nssf tanga akiwa mjumbe wa Bodi ya wadhamini wa nssf na hakujua taratibu hazikufatwa???
 
Sakata la uuzaji wa nyumba za Serikali limeibuliwa upya na aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Musa Assad akikosoa utaratibu uliotumika kuziuza.

Dodoma. Utaratibu uliotumika kuuza nyumba za Serikali umekosolewa kutokana na kutolihusisha Bunge kama chombo cha wawakilishi wa wananchi.

Hayo yameelezwa na aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), Profesa Musa Assad ambaye amesema mchakato huo ulihusisha Baraza la Mawaziri na Makatibu wakuu huku Bunge likiwekwa pembeni.

Akizungumza kwenye mdahalo ulioandaliwa na Mtandao wa Asasi za kiraia uliojikita katika kuchagiza uwajibikaji kwenye uziduaji (Hakirasilimali) katika wiki ya Azaki inayofanyika mjini Dodoma.

Amesema Serikali imeuza nyumba hizo na mchakato ulikuwa ni baraza la mawaziri wakishauriwa na makatibu kutengeneza waraka na kupeleka kwa Rais ili akubali kuuza nyumba hizo.

“Nani kakuruhusu? Ni mawaziri na makatibu wakuu. Kwanini halizungumzwi sasa jambo hilo. Lingekuwa wazi tungesema hilo haliwezekani lakini tumekaa kimya na hakuna mtu ambaye amesema hili jambo lazima lirudi bungeni tulizungumze ili tutoe ruhusa maalum jambo hili lifanyike ama lisifanyike,” amesema Profesa Assad

Chanzo: Mwananchi
Hizo nyumba ziliuzwa enzi za Mkapa na JK waziri hana mamlaka ya kuuza chochote bila idhini ya mkuu wa nchi.

Kwanini hajahoji mkuu wa nchi nguzo ya nne ana nyumba kadhaa Mikocheni A hadi Kawe Beach na kwanini kipindi akiwa ni CAG hakuhoji kimantiki kuhusua haya?
 
Huyu prof atulie tu,mbona alivyokuwepo Magu hakuwahi kufungua kinywa chake
Sasa hayupo, na uzuri wake hata akipokuwepo Assad alikuwa anamchana tuu yeye pamoja na Subuufa [emoji12][emoji12][emoji23]
 
Anataka katiba mpya
Huyu Prof huwa ananichanganya kweri kweri. Kwahiyo leo unataka Bunge Dhaifu na Mazuzu yashirikishwe? Au ndio ku "bow down" kumeanza baada ya "hali ngumu" mtaani?
 
Acha upuuzi ewe maamuma.. huyo magu wenu mnadhani alikuwa Mungu.. kila kitu kisemwe.

- Ule wizi wa 1.5trilion kipindi cha Shujaa wenu, aliusemea kipondi cha Nyerere?
Na aliposimamishwa pale Ikulu aongee unakumbuka alisema nini?! Huyu ni jasiri wa mabua tu naye.
 
Na aliposimamishwa pale Ikulu aongee unakumbuka alisema nini?! Huyu ni jasiri wa mabua tu naye.
Pale ulitaka ajibu nini? Na namna swali lilivyoulizwa? Suala la msingi kwenye vitabu vya audit huo ubadhirifu alishauonyesha
 
Prof. Assad, Mzee Warioba, Mzee Butiku, Dr. Slaa, Dr. Lwaitama, Ask. Bagonza, Ask. Mwamakula na watu wengine maarufu hapa nchini, karibuni katika uwanja wa kuhamasisha mijadala hai ya hitaji la wakati la haja ya kutaka kuwepo kwa katiba mpya.

Hakika mkifanya hivyo kwa dhati historia yenu itaandikwa katika wino wa rangi ya dhahabu.
 
Mimi nimepita bila kupingwa mara mbili!!! Nimechaguliwa na watu laki nne!! Halafu unaniita ZUZU mimi [emoji12][emoji12][emoji12][emoji23][emoji23][emoji23] alisikika mtu mmoja hukooo nyikani..
Huyo ndio UZUZU kumtandika bakora ya kichwa mwana ccm mwenzako
 
Hujui muzoga muzogo ndio wanadunda town....lengo ni kwamba legacy ya papa mukulu inakuwa kama tambala la dekio
Dogo nataka nidukue account yako ya cyptol Bitcoin nikuibie. Naona unaivest halafu unataka kutupiga humu jamvini
 
Prof hili suala la nyumba tuliache maana mkilivurumua tutaumbuka wengi..
 
Huyu Prof huwa ananichanganya kweri kweri. Kwahiyo leo unataka Bunge Dhaifu na Mazuzu yashirikishwe? Au ndio ku "bow down" kumeanza baada ya "hali ngumu" mtaani?
Mi nafikiri hapo anataka kumuonyesha anayesema yeye sio zuzu aanzekuona hoja ya uzuzu inapoanzia.
 
Huyu prof atulie tu,mbona alivyokuwepo Magu hakuwahi kufungua kinywa chake

Huyo alikuwa ni jizi tu, yoote aliyojilimbikizia kwisha habari yake! Fiti sita huko chini mchwa wanakung'uta nyonga tu!
 
Huyu prof atulie tu,mbona alivyokuwepo Magu hakuwahi kufungua kinywa chake
Ndugu,
Mwacheni afunguke ili kama TAIFA tuanze UPYA kuujenga utamaduni wa kujisafisa na kujitibu.
Kweli yawezekana kuwa alikuwa na uoga (au hata unafiki) wakati ule, LAKINI kuliweka wazi kutakuja lisaidia sana TAIFA na kuijenga zaidi nchi hii kwenye namna ya kuimarisha utawala bora, tofauti na tabia za ujima ambazo baadhi ya waTz wenzetu wanajitahidi kuanza kujivunia.
AMEN
 
Back
Top Bottom