Nyie ni wafanyakazi wa kuajiriwa? Angalia job description ya mkataba wako wa ajira. Je haisemi utafanya kazi hizi, hizi, na point ya mwisho kusema ...na kazi yoyote nyingine utakayopangiwa na mwajiri wako? Sasa tatizo liko wapi?
Na je, inapotokea dereva hana kazi kwa sababu kuna madereva wengi, mnataka alipwe bila kufanya kazi, wakati labda kuna nafasi kwenye masijala ambayo haina mtu? Kwa sababu option inakuwa ni kumpunguza dereva arudi nyumbani au kumwambia kaa hapa masjala (bila kuathiri mshahara wake) hadi tukiwa na gari nyingine ya ziada, badala ya kuajiri mtu wa masijala wakati kuna mtu hana gari na ni dereva. Mmefikiria hilo au hamjui mambo ya HR management mnalaumu tu?