TANZIA Profesa Augustine Massawe, Daktari bingwa wa Magonjwa ya Watoto afariki dunia

Pumzika kwa amani Prof Massawe
 
Kwani ugonjwa gani ambao hauui?Surua,kifua kikuu,ndui,pepopunda,kifaduru na kadhalika zote zina chanjo na zinaua.Kinachotakiwa kufanyika ni binadamu kutumia akili yake optimally.

Sasa hivi Corona ina chanjo na bado inaua lakini binadamu angekaa kimya bila kufanya lolote ingeua zaidi.Kinachotakiwa kufanyika ni kuongeza jitihada zaidi na wala siyo kubeza jitihada zinazoendelea.

Imani bila matendo imekufa.Binadamu wakikaa tu chini bila ya kufanya lolote na kusema kuwa Mungu ni mkubwa sana wataisha wote.Cha msingi ni kuendelea kutumia akili tulizo nazo.Hata mbuyu ulianza kama mchicha,usitegemee Corona ikamalizwa yote ndani ya siku moja.Kila kitu huhitaji muda.
 
Ulikuwa unaishi nchi IPI? Mbona enzi za Magu watu wamekufa sana mpaka barabaran unaokota watu
 
Very sad. Mungu afariji Familia yake.
Amesaidia Watoto wengi sana kuwatibu.
 
Duh.! Ni kama mzaha hivi...R.I.P Daktari
 
Duh, Pumziko La Amani Apate.

Nimepata sana mafundisho yake kupitia TV.
 

Hatujawahi kusikia watu walio uliwa na kuambukizwa na chajo hizo nyingine kwa jinsi ya na chanjo hii ya corona.

Tumeanza kusikia hii ya corona ikituulia wapendwa wetu kwa namna ya kuogofya acha wakiobanwa na matumbo ya kuhara na kukosa nguvu mwilini, kifo kiliwadip/beep baada ya kuchanjwa..
 
Paix à son âme ... Poleni wafiwa.
 
Mlimwita 'mjinga/nchi inaongozwa na washamba' kwa maamuzi ya kuhimiza kumtegemea Mungu kwanza na mengineyo. Ngoja tuwaone wajanja wa kutegemea akili zao na si Mungu watakapo tufikisha kama Taifa.
Mi sipo kinyume na taaluma ya mtu lakini approach ya Magufuli ya kututaka tusiipe airtime corona bali tumwangalie Mungu ni sawa na ile ya approach ya Musa jangwani kwamba atengenenze nyoka wa shaba ili wale watakaoinangalia nyoka ile watapona. Watakaokazana kutazama chini ili wasiumwe na nyoka watapukutika.

Hivi vitabu vya dini vina hekima iliyojificha. Tusipuuze. Ngoja tuone huu mziki utaishaje. Nchi yenyewe hii haina hata uwezo wa kuzuia malaria eti inahangaika na machanjo yasiyosaidia hata. Machanjo yenyewe dozi milioni moja kati ya watu milioni 60. Mnaambiwa weka tumaini lenu kwa Mungu mnasema ni ujima na ushamba. Washamba ndio wanaobaki sasa na wenye hekima wanaangamia.

RIP profesa.
 
Unaweza kuthibitisha kuwa wameuawa na chanjo ya Corona na wala siyo kwa kitu kingine chochote kile?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…