Lala salama baba. Tunakushukuru sana wa huduma Mungu aliyokuwa amekujalia
Uliitumia vyema karama Mungu aliyoiweka ndani yako
Mwendo umemaliza 💔💔💔
---
Daktari Bingwa wa Watoto Dr Augustine Massawe wa Furaha Medical amefariki Dunia leo Jijini Dar es Salaam. Taarifa kutoka kwa familia ni kwamba Dkt. Massawe amefariki asubuhi hii katika hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa kwa matibabu.
Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano kwa umma Muhimbili, Aminiel Aligaesha amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, “Amefariki saa mbili na nusu asubuhi leo.
Mtoto mkubwa wa marehemu Dk Furaha Augustine amesema baba yake alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upumuaji.
“Baba amefariki asubuhi ya leo alikuwa anaumwa na alilazwa Muhimbili kwa zaidi ya wiki na leo saa tatu asubuhi Mungu akamchukua,” amesema Dk Furaha ambaye ni daktari wa magonjwa ya kina mama na uzazi.