Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ObUnaweza kukumbuka kama ilikuwa Hanang, Kibo, Shengena au mawenzi?
Wee uliokota wangapi mkuuUlikuwa unaishi nchi IPI? Mbona enzi za Magu watu wamekufa sana mpaka barabaran unaokota watu
Matatizo ya upumuaji ndio corona? Au ni ugonjwa mwingine umeingia Tanzania?Hatari sana peno hasegawa
Of course kusoma old moshi ilikuwa ni heshima sana hasa kwa PCB na PCM kwa hata 70s sijui baada ya hapo!Probably ilikuwa Mawenzi. House master alikuwa mzungu,britisher. By the way,Mengi alikuwa Moshi Sec,nilipokutana naye siku moja ( mara moja tu nilipokutana naye)akaniambia,"habari za siku nyingi?" Sikuelewa maana ya Ile salamu mpaka baàda ya kifo chake nilipofahamu kwamba alikuwa anasoma Moshi Sec.
Wale watu wa Moshi Sec.,they have a very high opinion of themselves. Na Mengi aliposoma kule,halafu akaanzisha TV Tanzania,ile wameona uthibitisho kwamba Ile shule safi.
Siyo TV tu,na muziki pia alileta Mengi. Toka siku Ile mtangazaji wa Radio One aliposema,"kuanzia leo usiku Radio One itakuwa inapiga muziki usiku kucha",Tanzania ikawa nchi ya muziki.
Ob
Chanjo haikupi kinga papo hapo, inachukua at least 2 weeks toka uchome kupata kinga.INA maana alikuwa bado hajachoma chanjo?
Nimehuzunika Sana mimi na familia yangu maana mtoto wangu alitusumbua Sana tangu atibiwe na huyu mzee hajawahi ugua tenaLala salama baba. Tunakushukuru sana wa huduma Mungu aliyokuwa amekujalia
Uliitumia vyema karama Mungu aliyoiweka ndani yako
Mwendo umemaliza [emoji174][emoji174][emoji174]
---
Daktari Bingwa wa Watoto Dr Augustine Massawe wa Furaha Medical amefariki Dunia leo Jijini Dar es Salaam. Taarifa kutoka kwa familia ni kwamba Dkt. Massawe amefariki asubuhi hii katika hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa kwa matibabu.
Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano kwa umma Muhimbili, Aminiel Aligaesha amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, “Amefariki saa mbili na nusu asubuhi leo.
Mtoto mkubwa wa marehemu Dk Furaha Augustine amesema baba yake alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upumuaji.
“Baba amefariki asubuhi ya leo alikuwa anaumwa na alilazwa Muhimbili kwa zaidi ya wiki na leo saa tatu asubuhi Mungu akamchukua,” amesema Dk Furaha ambaye ni daktari wa magonjwa ya kina mama na uzazi.
Unaweza kuthibitisha kuwa wameuawa na chanjo ya Corona na wala siyo kwa kitu kingine chochote kile?
Ndio maelekezo yake pia.... lakini shida ikitokea hamna namna unakwenda kufuata msaada.
Kwani nia ni afufuke?Ukithibitisha ndio atafufuka?
Waziri anasema kuwa wahakikishe kuwa habari haziwafikii wananchi kuwa amechanjwa kwa sababu wananchi wengi wana elimu ndogo hawajui mambo ya side effects za chanjo.Kwa kuwa wana elimu ndogo wanaweza kufikiri kuwa imetokana na ubaya wa chanjo wakati ni side effects za kawaida kabisa.Kuna yule mmoja Mungu aliamua kuwaumbua kwenye podium akakata mawasiliano. Waziri anasema hakikisha habari haitokikufikia wananchi kama amechanjwa. Mungu wambinguni kama aishivyo atazidi kuweka mambo yote hadharani.
Sasa hivi watu wanajiendea tu! Hamna msisitizo wa barakoa wala sanitizer. Madaladala yanajaa hamna tahadhari yoyote
Kwani nia ni afufuke?
Waziri anasema kuwa wahakikishe kuwa habari haziwafikii wananchi kuwa amechanjwa kwa sababu wananchi wengi wana elimu ndogo hawajui mambo ya side effects za chanjo.Kwa kuwa wana elimu ndogo wanaweza kufikiri kuwa imetokana na ubaya wa chanjo wakati ni side effects za kawaida kabisa.
Lakini pia kuna mambo ya coincidence.Kwa mfano unaweza ukawa umechanjwa wakati sukari yako ipo chini.Ukaanguka kutokana na sukari kuwa chini halafu kwa sababu umeanguka wakati umechanjwa basi wananchi wakaamini kuwa ni chanjo.Kwa hiyo waziri alikuwa anajitahidi kuepusha yote haya yasiwachanganye wananchi.
Sasa waziri mkuu kudanganya kuwa anachanjwa kuna ajabu gani?Kwani kwa mfano kwenye utawala wa Magufuli ambao ulikuwa unapinga chanjo mawaziri kufanya kitu kama hicho ingekuwa ni ajabu?Muambie kakosea na hana hekima. Kumbuka zipo clips kibao zinasambaa mitandaoni kama moto wa nyikani za huko chanjo zilipotoka zikionesha wakubwa wahuko wakidanganya kuchanjwa kumbe ni geresha tu. Iko ya waziri Mkuu wa Australia, Mayor wa londoni nk. Halafu Waziri wa Afya unatamka wananchi wasijue. Mungu kamfanya ahujumu kampeni kwa maneno yake mwenyewe. Ngoja tuone Rsas atasema nini juu ya hili. Wale wa Arusha wanyonge wa vyeo vya chini barua ilitoka masaa machache tu.
Fikiri, John na Simon siyo wadogo zake.Duh! Poleni wanafamilia ya Massawe hasa wale wa kijijini kwake Mkomongo Moshi alikozaliwa. Nilibahatika kufundishwa na mama na baba yake enzi hizo na pia nilibahatika kusoma na wadogo zake kina Fikiri na Simon. Poleni mno na Mungu ampumzishe Kwa mahali pema peponi.
Mkuu binti wa 2005 bado yupo form two?? Kwanini ulimchelewesha hivyo?2005 nilipata huduma toka kwa huyu mzee pale morocco. Binti yangu aliyezaliwa tu akiwa na siku kama 6. Alikuwa akilia sana muda wote. Akipewa nyonyo ananyonya baada ya muda kidogo analia tena.
Nikampeleka pale. Sitakaa nidharau taaluma ya mtu. Hata akiwa mkuluma.
Mzee masawe akamwambia wife akamue maziwa ajazi kikombe kilikuwa pale. Kukamua kumbe mama maziwa hana na mtoto analia sababu hashibi. Nikaanza kuingia super market kununua mazuwa ya kopo. Kwa sasa ni mkubwa na yupo form two pale St marie Eugen.
Pumzika kwa amani mzee wangu Masawe.
Sorry Kwa kuchanganya. Unamaanisha Dr. Massawe alikuwa mdogo wake mwl. Beda na Manningi?Fikiri, John na Simon siyo wadogo zake.
Wale ni wadogo zake Mzee Dominic-alokuwa Mkurugenzi wizara ya kilimo