Profesa Janabi apuuzwe!

Tatizo hana nuance.

Hebu soma hapa.


Profesa Janabi kwenye uzinduzi wa Professor Jay Foundation ametaja dalili za mtu ambaye tayari anaugonjwa wa figo.


"Ukiwa na hizi dalili sio za mwanzo tena, tayari wewe umeingia kwenye ugonjwa wa Figo"

Katika kutaja dalili hizo, salamu hizo amelekeza kwa wale Wazee wa bapa, k-vant, Nyagi na wote wanaopiga vileo vikali ili kukomesha mademu na mengine kama hayo. Prof J hata kwenye interview yake alisema kwa siku alikuwa anachoma sindano za laki 8,

Dalili za ugonjwa wa Figo

1. Kuchokachoka ambako hakuelezeki.
2. Kulala siku inakuwa shida.
3. Hamu ya kula inapungua bila kujielewa.
4. Huwezi kufikiria sawa.
5. Mwili unaanza kuwasha.
6. Miguu inaanza kuvimba.
7. Ukiamka asubuhi jiangalie kwenye kioo uso wako utakuwa wa mduara na kadiri siku zitakavyokwenda inapotea.
8. Taste ya chakula inaanza kupotea
9. Kupumua hata rafiki zako wanaanza kugundua harufu yako ya kupumua inakuwa si nzuri sana.
10. Tumbo kuuma
11. Usiku kutoka mara kwa mara kwenda haja ndogo
12. Haja ndogo kuanza kuwa na povu
13. Unaanza kuona chembechembe za damu kwenye mkojo"
 
Vizuri umeambatanisha kabisa na kiapo husika ili tuweze kujadili kwa upana wake.

Ukisoma katika kiapo husika, naomba kuinukuu 'Kwamba hutajitangaza wala hutakubali utangazwe kwa NIA YA KUJIVUTIA WAGONJWA'.

Tafadhali rejea nilipobold na kuandika kwa herufi kubwa.

Kiapo kinatukataza kujitangaza kwa nia ya kujivutia wagonjwa. Na wala Prof Janabi hajawahi kujitangaza kwa ubingwa wake ili aweze kupata wagonjwa.

Motive yake siku zote imekuwa ni katika kuionya jamii kubadili njia zisizofaa, haswa ulaji na unywaji.

Leta ushahidi kuwa anafanya kwa nia ya kujitangaza ili kuwavuta wagonjwa waifate huduma yake.
 
Mkuu,

Tafadhali iweke vizuri hoja yako ili tuweze kujadili. Sijaelewa ama kicharazio chako kimeenda kinyume na ulichokusudia kuandika.
 
Sawa hulipwi, basi sio chawa,

Ila jukumu la kujali afya ni la mtu binafsi aisee, na kama huyo jamaa angekua anajali sana angetengeneza muongozo mrefu unaojitosheleza.

Kwanza haya mambo ya vyakula unajua yalivyo shady, kuna makampuni yanafaidika watu wakiharibu afya zao.

Ila sawa tu, watu wengi tz hawapendi kukosoa mambo, ni kazi bure
 
Kuna shirika linaitwa MDH na lingine Icap,haya yabahusika na ugawaji wa ARV nchini,sasa katika kuboresha ARVs kuna side effect imeibuka ambapo dawa hizi zinaumiza figo,client wengi wa ARVs wameripotiwa kuwa na matatizo ya figo,kuna watu maarufu nchini hibi jaribuni wanaumwa au walikufa kwa matatizo ya figo ula kiukweli walikuwa ni HiV victims
 
Binafsi sikuwah mwelewa na simwelewagi kabisa ana mikwara uchwala sana, Ni anatetemekewa sana mpaka aga nashangaa kunaniπŸ˜…
Sana tu, anaweza kuwa nia yake nzuri tu lakini mwisho wa siku anaweza kutufanya sisi na Ng'ombe tukagombania nyasi. Maisha yenyewe mafupi usile uka enjoy unabaki unachunga afya wakati mwili umeumbwa kupokea kila kitu la viungo vinafanya kazi kuweka mambo sawa shida inatokea organ moja ikiwa hai perform kabisa au kidogo. Binadamu kama gari tu, ukiona taa imewaka ujue kuna shida, unaenda kupima unajuwa shida nini unarekebisha sio taa ya gari inawaka wewe unaendelea kuitumia tu mpaka inakuja ina fail. Na sisi ndio hivyo ukiona mwili wako hauko sawa nenda Hosp sio mpaka huwezi kutembea tena. Jamani kuleni, kunywa ishi maisha yako ila ushauri tu mdogo tembea kidogo usijiachie tu lakini kulaaaaaaa
 
Ni utumbo jamani siyo moyo 😁😁😁

View attachment 2856453
Mimi toka mdogo nakula pilau na soda mbili juu mpaka naenda uzeeni niko poa tu. Lakini kama hili lina ukweli kwa sheria za kiafya kama sigara inaandikwa hatari inasababisha cancer lakini hukatazwi kuvuta. Sasa pilau zineendikwa usile pilau na pepsi hata mahotelini ingepigwa marufuku, si hatari kwa afya. Pepsi zoe ziandikwe usinywe na pilau ni hatari ya utumbo wako. Au sio jamani
 
Watanzania mna changamoto sana.

Kujali afya ama kutokujali ni uamuzi binafsi. Hakuna mtu atakuja kukushikia fimbo kuwa lazima ufanye hivi na vile.

Prof Janabi anajitahidi kutoa elimu (hata kama ni ndogo) ili walau kwa uchache wake, watu wawili watatu waache mtindo huo usiofaa. Na kweli wapo wanaobadilisha.

Sasa unataka aanze kutoa kitabu cha muongozo? Kama tu ushauri mdogo unakuletea ukakasi na kumuona hafai, je akileta kitabu? Si ndiyo utamuona shetwani?

Ndiyo, wapo watu wanafaidika sana. Kampuni za utengenezaji wa dawa wanategemea watu waumwe ndiyo faida iongezeke maradufu. Sasa kwani Prof Janabi anazipigia chapuo? La hasha!.

Bali anakushauri ili baadae usiwe mteja wa dawa na matibabu. Yeye kosa lake ni lipi?
 
Mkuu,

Tafadhali iweke vizuri hoja yako ili tuweze kujadili. Sijaelewa ama kicharazio chako kimeenda kinyume na ulichokusudia kuandika.
Hizo dalili za ugonjwa wa figo na maneno ya nukuu ya moja kwa moja ya Profesa Janabi unavichukuliaje?

Mfano. Ukikojoa mkojo wa povu tayari upo kwenye ugonjwa wa figo na hizi si dalili za awali tu?

Katika kazi ya utabibu, matabibu wanafundishwa "first, do no harm".

Mtu kaenda kapiga bia zake nne, karudi nyumbani, kakojoa mkojo wa povu, kwa sababu kanywa bia nne.

Akiangalia mkojo anaona wa povu. Akikumbuka Profesa Janabi kasema ukikojoa mkojo wa povu tayari una ugonjwa wa figo.

Huoni hapo Profesa katengeneza unnecessary panic?

Kuna dalili zimetajwa hapo zinaweza kuwa za magonjwa mengi sana, au zikawa si za ugonjwa wowote.

Kimsingi Profesa ameagua en masse watu ambao hata hajawaona, bila hata kusisitiza waende kuonana na wataalam.

That is scary.
 
Ameisha wapa maoni yake kama daktari bingwa. Sasa changanya akili zako uamue mwenyewe. Yeye kusha tenda wema hangoji kusifiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…