Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Tatizo hana nuance.Ok, uchawa una malipo yake, hujarelate mimi napata malipo gani kutoka kwa Prof Janabi. Mtu ambaye hata hanijui kwa lolote.
Tuachane na hayo;
Prof Janabi hajiamkiagi tu na kuanza kuzungumza. Bali anapoalikwa na kutakiwa kutoa maoni hufanya hivyo bila kusita.
Kama hufahamu, moja ya majukumu ya msingi ya Wahudumu wa afya ni kutoa ushauri elekezi juu ya namna bora ya kujitunza. Na hili si lazima pawe katika kituo cha huduma za afya, popote pale anapohitajika kufanya hivyo.
Kuna watu wanafanya mitindo fulani ya maisha pasipokuwa na uelewa wa athari zake hapo baadae. Mathalani, wewe unavyonyonya nyuchi za warembo, unafanya kwa kuongozwa na hisia. Baadae unakabwa na saratani ya koo, unaanza kuja kutia huruma. Eti,laiti ningelijua!.
Sasa wataalam wa afya (akiwemo Prof Janabi) wanafanya majukumu msingi kuwasanua ninyi vijana na rika zote ili mchukue tahadhari. Tena ni ushauri bila ya shurti.
Unapenda kusikia ukiambiwa kula kupita kiasi? Lewa ugaregare ndiyo ujue kuwa hakuchanganyi? Ukiambiwa fakamia junk foods, ndiyo utajua huyu ndiye mtaalam sasa? Huo ni ujuha.
Tengua kauli yako kuwa mimi ni Chawa.
Hebu soma hapa.
Profesa Janabi kwenye uzinduzi wa Professor Jay Foundation ametaja dalili za mtu ambaye tayari anaugonjwa wa figo.
"Ukiwa na hizi dalili sio za mwanzo tena, tayari wewe umeingia kwenye ugonjwa wa Figo"
Katika kutaja dalili hizo, salamu hizo amelekeza kwa wale Wazee wa bapa, k-vant, Nyagi na wote wanaopiga vileo vikali ili kukomesha mademu na mengine kama hayo. Prof J hata kwenye interview yake alisema kwa siku alikuwa anachoma sindano za laki 8,
Dalili za ugonjwa wa Figo
1. Kuchokachoka ambako hakuelezeki.
2. Kulala siku inakuwa shida.
3. Hamu ya kula inapungua bila kujielewa.
4. Huwezi kufikiria sawa.
5. Mwili unaanza kuwasha.
6. Miguu inaanza kuvimba.
7. Ukiamka asubuhi jiangalie kwenye kioo uso wako utakuwa wa mduara na kadiri siku zitakavyokwenda inapotea.
8. Taste ya chakula inaanza kupotea
9. Kupumua hata rafiki zako wanaanza kugundua harufu yako ya kupumua inakuwa si nzuri sana.
10. Tumbo kuuma
11. Usiku kutoka mara kwa mara kwenda haja ndogo
12. Haja ndogo kuanza kuwa na povu
13. Unaanza kuona chembechembe za damu kwenye mkojo"