Mkuu, ukiandika tena fanya proof reading kabla ya kuiachia. Kuna sehemu napata shida kung'amua unachokimaanisha.
Turudi kwenye mada;
Kila ugonjwa una dalili. Na maradhi mbalimbali yanaweza kuwa na dalili zenye kufanana. Haimaanishi kuwa dalili fulani LAZIMA iwe ni kwa ajili ya ugonjwa fulani pekee.
Lakini hiyo haimaanishi tuache kutaja dalili za ugonjwa husika kwa kuhofia kuwa zina mfanano na ugonjwa mwingine.
Kabla ya kukupima lazima tukuulize unavyojisikia na hilo litatusaidia kudadisi ugonjwa unaokusibu kutokana na dalili tajwa. Vipimo vitathibitisha.
Prof Janabi alikuwa wazi kuwa dalili za ugonjwa wa figo ni moja, mbili tatu. Na maradhi ya figo yana nyakati tofauti. Ukishaona dalili alizoanisha Janabi basi unakuwa katika nyakati siyo za awali tena bali ugonjwa umeshaanza kukomaa.
Kwa hiyo sijaona kosa lake kutaja dalili hizo. Uthibitisho utakuja baada ya vipimo kufanyika.
Natumia simu, nakosoa typos muda wote. Kama kuna niliposahau hujaelewa naomba post number nipitie. Be specific.
Matabibu wana wajibu wa kutofanya mambo yawe mabaya zaidi. First, do no harm.
Na kama ulivyosema, kuna dalili nyingi, kama za uchovu, kukosa hamu ya chakula na kukojoa mkojo wenye povu, zinaweza kuwa za magonjwa mengi tofauti, au si za ugonjwa wowote ni hali fulani tu mtu anapitia kwa sababu kala au kanywa kitu fulani, kapitia mazingira fulani etc.
Sasa, it is irresponsibke kwa Profesa kusema ukikojoa mkojo wa povu tayari una ugonjwa wa figo, hii si dalili ya awali.
It is irresponsible kwa sababu, unaweza kukojoa mkojo wa povu bila kuwa na ugonjwa wa figo. Kuna mtu akila ma supplements fulani tu anakojoa mkojo wa povu.
Unaweza kukojoa mkojo wa povu mara moja kwa sababu umekunywa pombe tu. Ukapata kihoro ukaona una ugonjwa wa figo, Profesa Janabi kasema. Ukafa kwa heart attack. I am overdramatizing for effect, but there is a major point of creating unnecessary panic here. Wakati kumbe hata huo ugonjwa wa figo huna, umekojoa mkojo wa povu kwa sababu umekunywa pombe nyingi kwa nuda mfupi tu, au umekula supplements fulani tu.
This is simple logic that does not need a medical degree.
Profesa anatakiwa kuwa more nuanced kwenye matamko yake, kuna watu wanamsikiliza kama mtaalam na wanafuatisha kila anachosema, akisema mambo bila nuance, anawapotosha watu waone wana ugonjwa wa figo, wakati hawana.
Usichoelewa nini?
Matokeo ya kukosa nuance ndiyo haya sasa watu wanasema "Profesa Janabi apuuzwe", wanakosa msaada mzuri tu ambao Profesa angeweka nuance kidogo tu angeweza kuwasaidia vizuri zaidi.
Yani Profesa kafanya kama anapima joto kwa mkono badala ya kutumia thermometer kuwa specific zaidi.