Profesa Janabi: Bei ya sukari imepanda juu, take advantage

Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi amezungumza kuhusu ongezeko la wagonjwa wa kusafisha figo ambapo amesema kwa siku hospitali hiyo inahudumia wagonjwa 120 hadi 130, hivyo ameihimiza jamii kuchukua tahadhari na kufuata mtindo bora wa maisha.

Profesa Janabi amesisitiza kwamba vitu hatari zaidi kwa afya ya mwili ni sukari na wanga na wala sio mafuta kama wengi ambavyo hudhani, na kwamba mwili hautunzi wanga wala sukari, badala yake huvibadilisha kuwa mafuta. Hivyo, amewataka watu kupunguza matumizi ya vyakula vyenye sukari na wanga.

“Sukari ni ugonjwa hausababishwi na fangasi, hausababishwi na bacteria, unasababishwa na lishe, lazima tubadilishe mtindo wa maisha, mtakaopata nafasi mzungumze na mtu anayefanyiwa dialysis (kusafisha figo) ndio mtafahamu umuhimu wa kutunza figo,”amesema.

Profesa Janabi ameeleza kuwa kuepuka ugonjwa huo ni jambo linalowezekana kwa kubana matumizi ya chakula, kutembea kwa hatua 10,000 kwa siku, na kupunguza vyakula vyenye sukari. “Bei ya sukari imepanda juu, take advantage.”
Siku hizi watu wenye Afya migogoro ndio wanajitia washauri wa watu wenye Afya zao

Unakuta mtu ana Afya migogoro kaambiwa acha sukari na wanga Kwa Afya migogoro uko nayo anamgeukia mkulima kijijini usile wanga ugali achana nao kituko Cha mwaka

Watu wa mjini mna mambo
 
Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi amezungumza kuhusu ongezeko la wagonjwa wa kusafisha figo ambapo amesema kwa siku hospitali hiyo inahudumia wagonjwa 120 hadi 130, hivyo ameihimiza jamii kuchukua tahadhari na kufuata mtindo bora wa maisha.

Profesa Janabi amesisitiza kwamba vitu hatari zaidi kwa afya ya mwili ni sukari na wanga na wala sio mafuta kama wengi ambavyo hudhani, na kwamba mwili hautunzi wanga wala sukari, badala yake huvibadilisha kuwa mafuta. Hivyo, amewataka watu kupunguza matumizi ya vyakula vyenye sukari na wanga.

“Sukari ni ugonjwa hausababishwi na fangasi, hausababishwi na bacteria, unasababishwa na lishe, lazima tubadilishe mtindo wa maisha, mtakaopata nafasi mzungumze na mtu anayefanyiwa dialysis (kusafisha figo) ndio mtafahamu umuhimu wa kutunza figo,”amesema.

Profesa Janabi ameeleza kuwa kuepuka ugonjwa huo ni jambo linalowezekana kwa kubana matumizi ya chakula, kutembea kwa hatua 10,000 kwa siku, na kupunguza vyakula vyenye sukari. “Bei ya sukari imepanda juu, take advantage.”
Hii haiwahusu Wasukuma hata kidogo. Yaani tangu saa 12 alfajiri niko shamba mpaka saa 12 jioni hayo maglycogen yatatoka wapi!
 
Ni vizuri kama unaumwa tafuta tiba badala ya kusingizia vyakula iwe wanga,,nyama,sukari,Mafuta au soda

Afya ikiwa migogoro tafuta tiba.Waachie wenye Afya zao waendelee navyo
Umesema na yangu mkuu! Eti yanasingizia nyama ya ng'ombe. Hivi nini kimebadilika kati ya 1900 na 2000? Babu zangu walikuwa hawali mboga nyingine zaidi ya nyama ya ng'ombe siku 365 na wamekuja kufariki wakiwa na miaka zaidi ya 90! Msukuma na Mmaasai umwambie aache nyama ya ng'ombe hatakuelewa!
 
Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi amezungumza kuhusu ongezeko la wagonjwa wa kusafisha figo ambapo amesema kwa siku hospitali hiyo inahudumia wagonjwa 120 hadi 130, hivyo ameihimiza jamii kuchukua tahadhari na kufuata mtindo bora wa maisha.

Profesa Janabi amesisitiza kwamba vitu hatari zaidi kwa afya ya mwili ni sukari na wanga na wala sio mafuta kama wengi ambavyo hudhani, na kwamba mwili hautunzi wanga wala sukari, badala yake huvibadilisha kuwa mafuta. Hivyo, amewataka watu kupunguza matumizi ya vyakula vyenye sukari na wanga.

“Sukari ni ugonjwa hausababishwi na fangasi, hausababishwi na bacteria, unasababishwa na lishe, lazima tubadilishe mtindo wa maisha, mtakaopata nafasi mzungumze na mtu anayefanyiwa dialysis (kusafisha figo) ndio mtafahamu umuhimu wa kutunza figo,”amesema.

Profesa Janabi ameeleza kuwa kuepuka ugonjwa huo ni jambo linalowezekana kwa kubana matumizi ya chakula, kutembea kwa hatua 10,000 kwa siku, na kupunguza vyakula vyenye sukari. “Bei ya sukari imepanda juu, take advantage.”
Huyu jamaa mjinga sana
 
Prof.Janabi ni moja ya watu muhimu Tanzania hasa kwa elimu yake ya afya ili kupambana na magonjwa yasiyoambukizwa.
Huyo Prof mwambieni Sasa Ni wakati muafaka alete kidonge Cha mchanga kisichokuwa na wanga ili tukila tunashiba na kutosikia njaa, hata hivyo tusipokula vyakula vyenye wanga mwili utapataje nguvu? Wake zetu watahudumiwa na nani?
 
Mimi napingana nae kwenye kubana matumizi ya chakula, bali alitakiwa aseme tule kile mwili inachohitaji tu na si zaidi. Na kufanya shughuki zinazoweka mwili fit, sio lazima kutembea hatua elfu 10, hata kukata viuno kitandani inaunguza sana wanga..
 
Umesema na yangu mkuu! Eti yanasingizia nyama ya ng'ombe. Hivi nini kimebadilika kati ya 1900 na 2000? Babu zangu walikuwa hawali mboga nyingine zaidi ya nyama ya ng'ombe siku 365 na wamekuja kufariki wakiwa na miaka zaidi ya 90! Msukuma na Mmaasai umwambie aache nyama ya ng'ombe hatakuelewa!
Ndo mana Janabi anasema Nyama sio Shida,Shida n Wanga ugali , wali hvyo ndo hatari vinakuwa converted kuwa Fat
 
Kwenye hili nakubaliana nae, sukari sio nzuri. Najisikia vibaya ninapomuona mtu mkononi ameshika soda.

Mafundisho yake mengine unaweza kuona kila mlo haufai kwa binadamu
Mimi asubuhi huwa napendelea kahawa ya maziwa au cream na nakunywa kavu bila sukari. Ila linapokuja suala la kuadimika au kupanda bei kwa sukari kwenye nchi, hili ni suala jingine. Kuna wakati ambao sukari inalazimika kutumika eg watoto, wagonjwa, mapishi ya aina fulani etc, na siyo kwamba unaitumia kwa kupitiliza bali unatumia kiwango sahihi.
 
Profesa anataka kusema hii sukari iliyoadimika ndio chanzo cha ugonjwa wa sukari?
Kwamba isipokuwepo na wagonjwa wa sukari watapungua ?
Msukuma mbunge kila siku bungeni analia na wasomi moja ya sababu ni kauli kama hizi kutoka kwa watu ambao tunaamini ni wasomi .
 
Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi amezungumza kuhusu ongezeko la wagonjwa wa kusafisha figo ambapo amesema kwa siku hospitali hiyo inahudumia wagonjwa 120 hadi 130, hivyo ameihimiza jamii kuchukua tahadhari na kufuata mtindo bora wa maisha.

Profesa Janabi amesisitiza kwamba vitu hatari zaidi kwa afya ya mwili ni sukari na wanga na wala sio mafuta kama wengi ambavyo hudhani, na kwamba mwili hautunzi wanga wala sukari, badala yake huvibadilisha kuwa mafuta. Hivyo, amewataka watu kupunguza matumizi ya vyakula vyenye sukari na wanga.

“Sukari ni ugonjwa hausababishwi na fangasi, hausababishwi na bacteria, unasababishwa na lishe, lazima tubadilishe mtindo wa maisha, mtakaopata nafasi mzungumze na mtu anayefanyiwa dialysis (kusafisha figo) ndio mtafahamu umuhimu wa kutunza figo,”amesema.

Profesa Janabi ameeleza kuwa kuepuka ugonjwa huo ni jambo linalowezekana kwa kubana matumizi ya chakula, kutembea kwa hatua 10,000 kwa siku, na kupunguza vyakula vyenye sukari. “Bei ya sukari imepanda juu, take advantage.”
Vip kuhusu juice ya miwa😆
 
Back
Top Bottom