Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahahaha namkumbali sana profesa, anatamani waTz wote wangekua VegetariansBaga, kfc, pepsi baridi, chipsi. Ukikutwa umeshika hivyo na prof Janabi ni viboko. Profesa anataka 75% ya sahani yako ijae mboga mboga za majani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Mohamed Janabi amesema utumiaji wa sukari kupita kiasi haufai kwa afya ya mwanadamu.
“Ukinywa glass moja asubuhi machungwa matano, mchana matano na jioni matano maana yake kwa mwezi ni machungwa 450, unaharibu afya yako, ogopa zaidi vitu vitamu tamu, unavyozungumzia sukari sio sukari tu bali ni vitu vitamutamu. Pale Muhimbili tunao watoto wa miaka tisa wana kisukari.” amesema Profesa Janabi
Amasema hayo mkoani Mwanza wakati akiwasilisha mada katika mkutano wa Mafunzo wa 108 wa watayarishaji wa vipindi vya Elimu kwa Umma ulioandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Washiriki wa mkutano huo ni watumishi kutoka taasisi mbalimbali za serikali.
Ni mwendo wa vitu vchungu, juisi iwe maji ya betriMateso haya😅🤣
Hakuna sehemu alisema mnywe vitu vichunguUsiku unywe muarobaini. Anataka tufe tukiwa na viungo kamili? Inatakiwa urudi kwa Sir.God hadi mwenyewe akushangae kwani maini yametoboka, moyo umevimba, figo zimeoza, mapafu yamejaa maji n.k