Profesa Janabi: Wakazi wa Rombo kunyweni maji sana

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Wakuu!

Prof Janabi ametuma ujumbe kwa ndugu zetu wa Rombo mkoa wa Kilimanjaro kwamba maji na matunda ndiyo muhimu katika kula na kunywa katika kipindi hichi cha sikuu ya Xmass.

Ila Janabi nimekunyooshea mikono juu kwa ushauri wako 😀 :EZclap:
================
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili na Mshauri wa Rais wa Masuala ya Afya na Tiba, Profesa Mohamed Janabi, amewasisitiza wakazi wa Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro kunywa maji akisema mandhari ya maeneo ya juu ya mlima husababisha damu kuwa nzito.

Akizungumza na wakazi hao jana Jumatatu Desemba 23, 2024, Profesa Janabi amesema katika maeneo ya juu, kama ilivyo Wilaya ya Rombo, damu za watu huwa nzito zaidi kutokana na mabadiliko ya kimo cha ardhi, hivyo kunywa maji ni muhimu kwa afya zao.

“Hapa Rombo, maji ni muhimu sana kwa sababu mpo juu, mkiwa juu damu inakuwa nzito kidogo, hivyo ni muhimu kunywa maji,” amesema Profesa Janabi.

Soma Pia: Prof. Janabi: Sijanywa juisi aina yoyote takriban miaka 20

Pia, amewahimiza kuzingatia ulaji wa matunda na mbogamboga ili kudumisha afya njema na kuongeza nguvu za mwili.

“Matunda na mboga ni muhimu kwa afya na kupumzika pia ni muhimu, hizi zote ni hatua zinazosaidia mwili kuwa na afya nzuri kila wakati,” amesema Profesa Janabi.

Credit: Mwananchi

janabi.jpg
drink-more-water.jpg
 
Janabi tupumzishe aisee, unatufata mpaka Rombo!? Umetunanga sana Jijini, sasa tumekuja Rombo bado tunafatana tu!!!??? Jiheshimu.
 
Ashajua hao wazee wa vichungu BIA wanazugia tu
 
Back
Top Bottom