Profesa Janabi’s Diet: Njia rahisi ya Kupungua na ukaona matokeo ndani ya mwezi mmoja tu

Kibongo bongo, ni ngumuu sanaaa
Imagine unamwambia mtanzania asile ugali, asile chapati, viazi au mihogo[emoji16][emoji16][emoji16]. Jaman embu muwe serious na maisha ya watu.

Haya maisha ukizidi ku complicate ndio yanazidi kukuchanganya!.
 
Imagine unamwambia mtanzania asile ugali, asile chapati, viazi au mihogo[emoji16][emoji16][emoji16]. Jaman embu muwe serious na maisha ya watu.

Haya maisha ukizidi ku complicate ndio yanazidi kukuchanganya!.
Yaani nimecheka ' kuweni serious na maisha ya watu.....'

Swala la diet kila mtu ana ujuzi wake wa kuelezea

Nimeshuhudia mtu aliyekuwa anakula healthy maisha yake yote hajawahi kuvuta sigara wala kunywa pombe, wanga kwake ilikuwa mwiko alitumia pesa nyingi kula chakula natural vitamin protein etc kwa wingi... Aliugua kidogo tu yaliyofuata alilia sana akauliza 'why ??
Aligundulika ana matatizo ya moyo kibaya zaidi aligundulika ana cancer alipewa muda wa miezi mitatu kuishi (bahati mbaya sikuwahi kuzungumza naye tena lakini niliambiwa alifariki)

Mwili tusiulazimishe kuadjust tuuuu ilimradi wamesema
Wahindi na Waarabu idadi ingepungua maana ndugu zetu hawa wanga ndio chakula chao kikuu
* Kila mtu na metabolism yake....zoezi ndio jibu
Huu ni mtazamo wangu
Tutaweza acha maandazi na vitumbua kweli??
 
Kumbuka enzi hizo kijijini, mzunguko ulikuwaje!!!

Ni mara ngapi unakutana nachakula tofauti na ugali??? Labda ukale mabibo na korosho, lakini wazee walitoboa bila taabu mpaka 90yrs.

Siku hizi vijana kwa watu wazima tunang'ang'ana kula kwa draft lakini waapi, mara huyu kaamka anaumwa kichwa, mwingine korodani ya kulia imevimba, mwingine nyonga haina vilainishi, unakaza wee kupiga tizi mara paap, unatanua hipsi kama.....

Halafu kuja wajinga wameacha tu maisha yaendelee kama yanavyotaka[emoji1787][emoji1787], na yenyewe yamewaacha wafanye mambo yao[emoji16][emoji16].
 
Kwa uelewa wa kawaida tu brain cells zinatumia only glucose as fuel, hazitumii kingine chochote zaidi ya glucose ktk ufanyaji kazi wake.

Protein ni molecule kubwa na fatty acid zinabound na protein (albumin) hivyo haziwezi kupita kwenye blood brain barrier (BBB).

Sasa kama watu wataepuka vyakula vyenye glucose ndani yake tutegemee ubongo utafanyaje kazi?
 
Atakufa tuuu tena kizembe kweli. Ana udhaifu wake hiyo.
Wamuulize habari ya pombe na wanawake !!!
 
Daaah maisha ayo ndio naishi mimi wakuuu na mwalimu wa izo diet kwangu mm ni de boaz mkumbo na nainjoi kwa kwel na sisikiii njaa ovyo asbui supu tuu mchana kabich na usiku nyama choma na salad no kitambi na uzito na nafunga sana.
 
Kwa msosi huo, kwa kijana mambo yetu itakuwaje sasa? au kwa the oldies tu?
Unapiga safi tena unakuwa mwepesi zaidi kwa mfano mm ni kijana wa miaka 24 mwaka jana nilikuw na uzito wa kg 93 nikafanya iyo diet na nipo poa now nina kg 70 na nina muenekano mzuri tu
 
Chakula ni suala MTAMBUKA, bibi yangu ana miaka 90+, diet yake ina wanga wa kutosha, hajawahi kulazwa hoi kitandani...
 
Unapiga safi tena unakuwa mwepesi zaidi kwa mfano mm ni kijana wa miaka 24 mwaka jana nilikuw na uzito wa kg 93 nikafanya iyo diet na nipo poa now nina kg 70 na nina muenekano mzuri tu
👏🏼👏🏼👏🏼
 
Hahaaaa.. ,kazi kweli kweli..

Hebu mniache nile kitu roho inapenda;

Unajibana kote huko halafu unakuja kuwa diagnosed with diabetes melitus (kisukari) na presha uliyoridhi kutoka kwa wajomba zako[emoji28][emoji28]
 
Ukiwasikiliza sana hawa wasomi mwisho wa siku either utachanganyikiwa zaidi au utajawa na hofu karibu ya kila kitu maishani mwako..

Yeye anadai anakula samaki wa kuchoma waka kuna tafiti kibao tu zilizofanyika zinaelezea hatari ya kupata kansa ya kwenye utumbo (colorectal cancer) kutokana na ulaji mwingi wa vyakula, na hasa nyama za kuchoma (including samaki)
 
Anachokizungumza Prof ni hypothesis kwenye eneo ambalo anajaribu kufanyia tafiti. Kula wanga mwingi au kutokula hakuwezi kukuongezea maisha ila kunaweza kukajenga au kubomoa afya yako.Maisha anatoa Mungu ila usimjaribu bwana Mungu wako, ukipata maarifa tumia kuzuia madhara kwenye mwili wako.
 
Mi nafikiri shida yetu kubwa ni sedentary lifestyle. Maisha ya daladala, bodaboda na bajaji.
 
Nimeacha kuamini hawa Ma prof.
Yaani kukataa nachoro juisi[emoji485] ndio hoja halafu unakula ndizi mbivu[emoji287] huku umekataa tende? Hautaki kula whole grain food? Atafanya utafiti mwingine muacheni
 
Mungu azidi kumbariki Daktari Janabi kwa kutupatia watz maarifa kwaajili ya maisha yetu !

Imeandikwa” watu wangu wanawngamia kwa kukosa maarifa”

Prof hakutaka kuwa mchoyo wa hizo habari njema!

Mwenye masikio na afahamu
 
Dah!!

Wale wa biriani la kwa Sele Bonge na Mariam ndo basi tena
 
Hata ufanyaje ukifika muda wako utarudi kwenye udongo tu.. Hivi nchi hii na uchumi huu utaishi bila ya kutafuna ugali au mikate.. Ashindwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…