Jay ndio anapotea kabisa ,nilishaanzisha thread kuhusu nyimbo yake mpya ya aliyoitoa mwaka huu "Kama ipo ..." Ila wadau wakamtetea sana.Ukweli ni kwamba Prof kwa sasa hana jipya na kwa wanaomfuatilia sana kwa kakaribu watakubaliana nami kuwa huyu jamaa kalewa sifa na amejisahau sana.Ila tumwombee asijeakaishia kuwa kama Mr. Nice. Yupo mwingine anayejisahau na kujiona yeye ni wa kimataifa zaidi AY,tatizo la AY anapata nafasi ya kufanya ft na wasanii wa nje ila anashindwa kutumia hiyo nafasi vyema.Ukisikiliza hizo nyimbo alizofanya ft kama vile anawaiga wao naye aonekane wa huko.Kwenye sanaa hakuna kitu cha msingi kama kuheshimu ID yako.Faly Ipupa amefanya ft na Olivia na amepata heshima coz ameweza kulinda ID yake (style) yake.