Profesa Kabudi hayo mafanikio ya Rais Samia hayatokani na yeye kusimama kwenye mabega ya watangulizi wake?

Profesa Kabudi hayo mafanikio ya Rais Samia hayatokani na yeye kusimama kwenye mabega ya watangulizi wake?

jindundu

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2025
Posts
679
Reaction score
581
Baadhi ya Viongozi wa nchi hii siyo tu kwamba wanaonekana kuelewa madaraka na uchawa, bali Sasa wameanza kukufuru.

Mmoja wao ni Profesa Kabudi. Huyu anajua baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere enzi za uongozi wake alifanya mambo mengi makubwa na ya kukumbukwa.

Nyerere alituunganisha watanzania tukawa wamoja, Nyerere alisimamia vema sekta ya Kilimo ambayo ndiyo msingi mkubwa wa Maendeleo ya Uchumi wa Taifa letu.

Enzi zile Elimu ilitolewa bure, gharama za maisha zilikuwa chini, shilingi yetu ilikuwa na thamani zaidi ukilinganisha na miaka hii.

Tulizalisha na kuuza mazao ya Kilimo kwa wingi zaidi kuliko ilivyo Leo.

Soma Pia: Kabudi: Samia ametimiza aliyoshindwa mwalimu Nyerere

Uzalendo, Uadirifu na uwajibikaji Serikalini ulikuwa ni wa kiwango bora kuliko leo. Nikitaja kwa uchache. Pamoja na mazuri haya, Nyerere kama binadamu alikuwa na mapungufu yake ambayo kwa kiwango kikubwa yanatokana na mfumo wa Siasa za wakati ule, mfumo wa Kidunia katika Sayansi, Teknolojia na Ustaarabu.

Chini ya uongozi wa Samia, Kuna kasoro nyingi zinazosemwa na ambazo hazisemwi hadharani.

Wanasema wameboresha Sekta ya Kilimo lakini uhalisia hauko hivyo, rushwa, ufisadi, wizi na ubadhirifu wa mali ya umma, vitendo vya kikatili.

Uadirifu na uzalendo kwa watumishi.wengi wa umma ni msamiati mgumu. Tatizo la kukatika kwa umeme ndio usiseme.

Profesa Kabudi baada ya kushindwa kutimizq ndoto zake, Sasa anajifanya hamnazo .Anaongea mambo ambayo yanaweza kuibua maneno na ukosoaji mwingi dhidi ya boss wake kwa kujaribu kumpandisha na kumtweza Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

Zaidi ya yote, Mama Samia kasimama kwenye mabega ya watangulizi wake. Katika mafanikio ya mama Kuna mkono na nguvu nyingi za awamu zilizopota.

Ningekuwa Mimi ndiye yule, huyu alikuwa harambi tena uteuzi, ningemuona mnafiki anayetafuta kunichonganisha na umma kwa kunipa sifa nisizostahili.
 
Back
Top Bottom