Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 122,494
- 96,074
Mkuu umetoa ushauri mzuri sana wa kitaalam, hongera sana ila naona hukumuelewa vizuri mpandisha uzi.
Mtu kama wewe ambae hauna taarifa za mambo mengi ya nchi yako kuhusu kilimo huna moral authority ya kumshambulia na kumkosoa Prof. Kabudi kama ulivyofanya hapa.
FYI, aina ya Vanilla inayolimwa Madagascar ipo kwa wingi tu inalimwa mkoani Kagera. Hakuna haja ya kwenda kufuata mbegu za vanilla nchi nyingine.
Na vanilla kabila hiyo ndiyo bora zaidi duniani, inalimwa kwa wingi pia nchi jirani ya Uganda kiasi kwamba wanunuzi wakubwa wa vanilla ya Kagera wanatoka Uganda. Labda mshauri waziri wa kilimo akafanye hamasa ya miradi mikubwa ya kulima vanilla kibiashara zaidi kule Kagera. Ukitaka vanilla tuber cuttings kwa ajili ya mbegu wewe sema tukuuzie.
Pia ungeshauri watanzania wasiuze vanilla pods mbichi bali wafanye vanilla cure and vanillin extraction process hapa hapa nchini na kuuza bei ya soko la dunia.