Uchaguzi 2020 Profesa Kitila Mkumbo atangaza kugombea Ubunge 2020

Uchaguzi 2020 Profesa Kitila Mkumbo atangaza kugombea Ubunge 2020

Nchi hii ni ya wote, ukiwa mtu sahihi na mahali sahihi, ni kugusa tu kuielekea ndoto yako!

Maana kuna watu ktk kazi zao, huwa nawambia, unaweza ukawa ni mtu sahihi katika kazi zako, lakini Kwa vile kazi yako si sahihi, huwezi kupata matunda ya kazi yako, lakini vikevile, kazi yako inaweza kuwa ni sahihi lakini wewe si sahihi katika kazi hiyo, hivyo pia huwezi kupata matokeo ya kazi hiyo

Kilichopo, ni lazima kufahamu kuwa, wewe ni mtu sahihi katika kazi sahihi, vitu Hivi viwili vikiwa sahihi Vyote, ni kuteleza tu kuelekea mafanikio

Mtu sahihi Chama sahihi na Kwa muda sahihi, Kwa nini usifike uendako?
Katibu mkuu wa wizara sharti awe mtaalamu wa sekta husika. Kitila na water resources wapi na wapi? Kitila si mtu sahihi kwa nafasi aliyonayo hivi sasa. Nafasi sahihi kwake ni kufundisha na kufanya tafiti. Hapo tu ndio ataweza kurejesha kwa taifa gharama za kumsomesha mpaka hapo alipo
 
Naunga mkono hoja mkuu, lakini kama ni kupotea tulishaanza kitambo Sana, Embu wacha tujaribu na hilo
 
Huu ndiyo muda wa kutoana kafara🤗,kule Mkumbo vs Mwigulu

Sasa ametambua kuwa kule kwa Mwigulu asikuguse kabisa, na ndiomaana kajibu vizuri sana na kutobaini ni jimbo gani anatarajia kugombea.

Namtahadharisha kuwa kule kwa Nchemba asiguse kabisa atakufa kisiasa. Kama alifikiri CHADEMA na ACT wanafigisu akigusa huko atitambua CCM kwa undani na hatahitaji kuisikia maishani mwake.
 
Hizi njaa, ameshasahau kuwa alikuwa mpinzani advocating for change to a democratic state
Njaa ni nini sasa hapo? Upinzani wenyewe wanashindana "kuboresha" katiba zao ili wenyeviti wao watawale milele. Au hiyo ndiyo tafsiri ya demokrasia siku hizi.
 
Je kamaliza kazi aliyopewa na Mkulu? Je nchi nzima inapata maji masaa 24 bila mashaka? Je hakuna wanaokunywa maji machafu Tanzania nzima? Mheshimiwa raisi kashasema kama kakuteua na hujamaliza kazi zako basi tulia ulipo. Kwan mkuu Kitila Mkumbo unazani kazi uliyopewa ya kuhakikisha nchi inapata maji tiririka safi umeshaimaliza?
Hayo ulitangaziwa lini? Kwamba amepewa "malengo" ya kuhakikisha nchi nzima inapata maji 24/7? Unadhani kazi ya kumpelekea maji safi kila mtanzania ni ya kufumba na kufumbua? Siku hizi mitandaoni kumejaa wasomi hewa.
 
Ndo umuulize Polepole aliesema au hukuskia umekuja tu umekurupuka.
 
Sasa ametambua kuwa kule kwa Mwigulu asikuguse kabisa, na ndiomaana kajibu vizuri sana na kutobaini ni jimbo gani anatarajia kugombea.

Namtahadharisha kuwa kule kwa Nchemba asiguse kabisa atakufa kisiasa. Kama alifikiri CHADEMA na ACT wanafigisu akigusa huko atitambua CCM kwa undani na hatahitaji kuisikia maishani mwake .
Mkuu kule nayeye ni kwao? Au kavamia tu
 
Kwa jinsi alivyojibu ni dhahiri shahiri kuwa hatochuana na Madeluu bali jimbo lililokuwa upinzani ili kuongeza mtaji wa ccm!!
 
Back
Top Bottom