Profesa Kitila Mkumbo: Deni la Serikali limefikia Tsh. Trilioni 96.8

Profesa Kitila Mkumbo: Deni la Serikali limefikia Tsh. Trilioni 96.8

Kidogo sana kwa utajiri tulionao Tanzania.
1730510049274.png
 
Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema hadi kufikia mwezi June mwaka huu 2024, deni la Serikali liliongezeka na kuwa Tsh. bilioni 96,884.18 (Tsh. trilioni 96.8) ambapo Kati ya kiasi hicho, deni la ndani lilikuwa shilingi bilioni 31,951.24 na deni la nje lilikuwa shilingi bilioni 64,932.94.

Akiongea leo November 01,2024 Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2025/2026, Prof. Mkumbo amesema fedha zilizosababisha deni hilo zilielekezwa katika kugharamia miradi ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege, umeme na maji

“2023/24 kampuni za Fitch Ratings na Moody’s Investors Service zilifanya mapitio ya tathmini ya Nchi kukopesheka katika masoko ya mitaji ya kimataifa na kuchapisha matokeo ya daraja B1 na B+ mtawalia, matokeo mazuri ya tathmini hizo yalitokana na ukuaji mzuri wa uchumi unaoweza kuhimili mitikisiko ya kiuchumi, utekelezaji wa mageuzi ya kimuundo yanayoboresha mazingira ya biashara, ufanisi wa ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa fedha za umma, matokeo hayo yatawezesha kupungua kwa gharama za mikopo (riba za mikopo) kutokana na kuongezeka kwa imani kwa Wakopeshaji na hivyo kuwezesha ugharamiaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, kuongezeka kwa uwekezaji kutoka nje ya Nchi ambao utasaidia kukuza uchumi”

Itakumbukwa wakati akitoa hotuba ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2023, Bungeni Jijini Dodoma June 13,2024, Waziri Mkumbo alisema hadi kufikia March 2024, deni la Serikali lilikuwa shilingi bilioni 91,708.3 (Tsh. trilioni 91.7) ikilinganishwa na shilingi bilioni 77,010.4 (Tsh. trilioni 77.) katika kipindi kama hicho mwaka 2023, sawa na ongezeko la asilimia 19.1.

Kwa upande wake CAG Charles Kichere, wakati akiwasilisha ripoti kuu kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kwa Rais Samia Ikulu Dodoma March 28,2024 alisema hadi kufikia June 30,2023 deni la Serikali lilikuwa Tsh. trilioni 82.25 sawa na ongezeko la 15% kutoka Tsh.trilioni 71.31 kwa mwaka 2021/2022.

BUNGENI
Maisha ni kucheka maisha ni kufurahi manufaa ya Utawala wa wenye kutumia hisia zaidi kuliko akili, Mungu akupe nini anachukua anakupa anaweka pwaaa
 
91.7 tri March, 2024 - hadi 96.8 June, 2024 ni nyongeza ya trilioni 5.1 kwa miezi mitatu - April, May na June, 2024 sawa na wastani wa 1.7 trilioni kwa mwezi katika hiyo miezi mitatu.
March 28,2024 Tri.82 Jana November 1 Tr. 96, Anachukua anaweka twa twa anatulia anaweka pwaaa
 
Sio rahisi kuelewa maana inahusisha deni la ndani,denk la Nje,deni la sekta binafsi na hati fungani za serikali.

Hilo ni somo linalojitegemea kwenye Masomo ya Uchumi
Sio rahisi kuelewa maana inahusisha deni la ndani,denk la Nje,deni la sekta binafsi na hati fungani za serikali.

Hilo ni somo linalojitegemea kwenye Masomo ya Uchumi
Ni very simple, ni deni la serikali na ondoa hiyo deni la sekta binafsi haihusiki, tunajua mlidanganywa na yule mchumi wenu fake Mwigulu
 
Concept ya deni la Serikali haieleweki na wengi
Tutakopa sana lakini hufika pahala, taifa letu halitahitaji tena mikopo, maana kila hitaji la nchi litakuwa limekamilika, hapo ndipo urejeshwaji hufanyika kwa kasi ya ajabu, na wananchi hula tunu za nchi yao!, mf. Amerika au kanada zimejengeka kiasi fedha nyingi haziendi kwenye miundombinu bali hurudi katika huduma za kijamii zaidi, maana miundombinu ndicho kinachotafuna fedha kwa 90%.
°low brain hawataweza kunielewa, piteni tu.
 
Hahaha Mwigulu aliisha sema HAMTAPIGIWA HODI mlipe tatizo lenu nini?
 
Sehemu ya pesa za hilo deni zimeenda kufanya huu upuuzi
20241101_194236.jpg
 
Tutakopa sana lakini hufika pahala, taifa letu halitahitaji tena mikopo, maana kila hitaji la nchi litakuwa limekamilika, hapo ndipo urejeshwaji hufanyika kwa kasi ya ajabu, na wananchi hula tunu za nchi yao!, mf. Amerika au kanada zimejengeka kiasi fedha nyingi haziendi kwenye miundombinu bali hurudi katika huduma za kijamii zaidi, maana miundombinu ndicho kinachotafuna fedha kwa 90%.
Mama alikopa hela za Uviko 19 akajenga miundombinu ya Afya ,maji,kuboresha Hifadhi za Taifa ,shule nk ila akatukanwa sana kwamba eti anakopa kujenga shule.

Naunga mkono Serikali kukopa na kuboresha Huduma zote za kijamii na kiuchumi isipokuwa kukopa eti kuboresha mifumo ya sheria nk sio Tija sana.

Mwisho kabla ya kushangaa deni unatakiwa ujue Ukubwa wa Uchumi wa Nchi.
 
91.7 tri March, 2024 - hadi 96.8 June, 2024 ni nyongeza ya trilioni 5.1 kwa miezi mitatu - April, May na June, 2024 sawa na wastani wa 1.7 trilioni kwa mwezi katika hiyo miezi mitatu.
Kushuka thamani Kwa Shilingi ndiko kumechangia ongezeko kubwa la deni la Taifa.

Hata hivyo Uchumi wa Tanzania una Trilioni 215 less Trilioni 97 ,hakuna deni la kubabaisha Nchi yaani kiufupi hata nusu ya Uchumi Bado
 
Ni very simple, ni deni la serikali na ondoa hiyo deni la sekta binafsi haihusiki, tunajua mlidanganywa na yule mchumi wenu fake Mwigulu
Hujui kitu.Nakupa mfano Majizi hapo NMB na CRDB zilioata Mkopo wa mabilioni ya Shilingi na taasisi za Kimataifa kuja Tanzania,hela hizo zinahesabiwa kwenye national debt na sio government debt.

Nyie mbulula hiyo ni kozi ya somo la Uchumi hamuwezi elewa bila kwenda darasani how it works na siku zote unapokoti maneno ya kiuchumi uwe makini na matumizi yake.
 
Ndiyo viongozi wetu,, hawawazi jinsi ya kulipunguza wanawaza jinsi ya kuliongeza ila liwe vumilivu,, duuuuuuu
 
Sio rahisi kuelewa maana inahusisha deni la ndani,denk la Nje,deni la sekta binafsi na hati fungani za serikali.

Hilo ni somo linalojitegemea kwenye Masomo ya Uchumi
Deni ni deni tu
Maana ya deni ni kwamba unadaiwa yaani ulikopa Baada ya kuwa huna na unatakiwa kulipa
 
Back
Top Bottom