ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Sasa Hilo sio swali la kuuliza Kwa mtu anaeelewa.Ndio maana nikasema concept ya deni wengi hamuelewi.Je Bado tunakopesheka, au tumevuka mstari wa kutokopesheka
Inatakiwa tupewe kizo hela Ili Kila mtu alipe kivyake ππNdugu MTANZANIA mwenzangu kama .nchi tunadaiwa Trillion 96.8 manake wewe na mimi tunadaiwa milioni 2 kila mmojaπ
Hapo kama unafamilia na wasiojiweza pia wanadaiwa
Utalipa utake au usitake.Huyu mama anakopa anatapanya Kwa ufisadi harafu mabwege wanazubaishwa Kwa goli la mama
Kushuka Kwa Thamani ya Shilingi imechangia zaidi kuongezeka Kwa deni.Hilo deni mbona linazidi kuongezeka tu bila kupungua huku tukiambiwa uchumi wetu unakua?
Kwanini hilo deni lisipungue?
Kwanini uchumi ukue na bado deni lizidi kukua?
Huwa hatulipi madeni?
Kwenda, Hela zinatapanywa kila sehemu hovyo eti Mkifunga GOLI mnapewa hela...Tutakopa sana lakini hufika pahala, taifa letu halitahitaji tena mikopo, maana kila hitaji la nchi litakuwa limekamilika, hapo ndipo urejeshwaji hufanyika kwa kasi ya ajabu, na wananchi hula tunu za nchi yao!, mf. Amerika au kanada zimejengeka kiasi fedha nyingi haziendi kwenye miundombinu bali hurudi katika huduma za kijamii zaidi, maana miundombinu ndicho kinachotafuna fedha kwa 90%.
Β°low brain hawataweza kunielewa, piteni tu.
Tunamuangalia tu anavyowajaza watu...Ni very simple, ni deni la serikali na ondoa hiyo deni la sekta binafsi haihusiki, tunajua mlidanganywa na yule mchumi wenu fake Mwigulu
Nani kaishusha hiyo shilingi...?Kushuka Kwa Thamani ya Shilingi imechangia zaidi kuongezeka Kwa deni.
Economic circumstances ikiwemo wewe hapo umechangiaNani kaishusha hiyo shilingi...?
Unatafuta pa kutetea Uongozi mbovu...πππ
Jibu swali, mkopo wa nyumba yako ni deni la serikali?Umekopwa kutoka Nje ya Nchi? Au hujawahi sikia Serikali inatoa guarantee Kwa kampuni binafsi kuchukua mikopo Nje Kwa Ajili ya uwekezaji?
Simply Google tu,Evidence!
Simply Google tu,Evidence!
So yule Mpini hana jipya ππWaziri wa Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema hadi kufikia mwezi June mwaka huu 2024, deni la Serikali liliongezeka na kuwa Tsh. bilioni 96,884.18 (Tsh. trilioni 96.8) ambapo Kati ya kiasi hicho, deni la ndani lilikuwa shilingi bilioni 31,951.24 na deni la nje lilikuwa shilingi bilioni 64,932.94.
Akiongea leo November 01,2024 Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2025/2026, Prof. Mkumbo amesema fedha zilizosababisha deni hilo zilielekezwa katika kugharamia miradi ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege, umeme na maji
β2023/24 kampuni za Fitch Ratings na Moodyβs Investors Service zilifanya mapitio ya tathmini ya Nchi kukopesheka katika masoko ya mitaji ya kimataifa na kuchapisha matokeo ya daraja B1 na B+ mtawalia, matokeo mazuri ya tathmini hizo yalitokana na ukuaji mzuri wa uchumi unaoweza kuhimili mitikisiko ya kiuchumi, utekelezaji wa mageuzi ya kimuundo yanayoboresha mazingira ya biashara, ufanisi wa ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa fedha za umma, matokeo hayo yatawezesha kupungua kwa gharama za mikopo (riba za mikopo) kutokana na kuongezeka kwa imani kwa Wakopeshaji na hivyo kuwezesha ugharamiaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, kuongezeka kwa uwekezaji kutoka nje ya Nchi ambao utasaidia kukuza uchumiβ
Itakumbukwa wakati akitoa hotuba ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2023, Bungeni Jijini Dodoma June 13,2024, Waziri Mkumbo alisema hadi kufikia March 2024, deni la Serikali lilikuwa shilingi bilioni 91,708.3 (Tsh. trilioni 91.7) ikilinganishwa na shilingi bilioni 77,010.4 (Tsh. trilioni 77.) katika kipindi kama hicho mwaka 2023, sawa na ongezeko la asilimia 19.1.
Kwa upande wake CAG Charles Kichere, wakati akiwasilisha ripoti kuu kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kwa Rais Samia Ikulu Dodoma March 28,2024 alisema hadi kufikia June 30,2023 deni la Serikali lilikuwa Tsh. trilioni 82.25 sawa na ongezeko la 15% kutoka Tsh.trilioni 71.31 kwa mwaka 2021/2022.
BUNGENI