BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Serikali imeshauriwa kuboresha na kuipanua barabara ya Dar es Salaam-Morogoro hadi Dodoma ili kupunguza uwezekano wa ajali kutokea kutokana na wingi wa magari yanayotumia njia hiyo kwa sasa.
Ushauri huo umetolewa kutokana na wimbi la ajali mfululizo katika barabara hiyo, ikionekana kuwa wembamba wa barabara unaweza kuwa chanzo cha ajali nyingi.
Mbunge wa Ubungo, Profesa Kitila Mkumbo ameshauri hivyo wakati akiaga miili ya Profesa wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Honest Ngowi na aliyekuwa dereva wake, Innocent Mringo ambao walifariki kwa ajali Machi 28, 2022, Mlandizi Mkoani Pwani wakiwa njiani kwenda Morogoro.
"Mara zote lazima kifo kiwe na sababu, lakini takwimu zinaonyesha kuwa barabara hii ya Dar hadi Morogoro hadi Dodoma ni kweli ina magari mengi sana, ni vema Serikali ikawa na mradi wa kuipanua ili iendane na matumizi," alisema Profesa Mkumbo.
Miili ya wawili hao imeagwa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Chanzo: MwanaHalisi