Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema wingi wa watu kwenye mikutano ya kampeni ya wagombea wengine wa urais haumtishi.
Profesa Lipumba amesema hayo jana Iringa Mjini wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa kampeni mpaka sasa.
Profesa Lipumba amesema anachokifanya ni kwenda maeneo ya vijijini ambako ndio kuna changamoto kubwa za Wananchi na sio kukusanya watu kwenye malori na mabasi kuwapeleka kwenye mikutano kama vyama vingine.
"Kampeni mpaka hivi sasa zinaendelea vizuri na nimejikita zaidi kwenda vijijini maana ndiko ziliko kero za Watanzania, mimi siishii mijini kama wenzangu ambao wamekuwa wakikusanya watu kwenye malori na mabasi.
Chanzo: Mwananchi