Hakika misiba inasikitisha siku zote. haizoeleki. ni majonzi na simanzi kwa wafiwa, jamaa, ndugu, marafiki na walihusiana kwa lolote katikati ya maisha yake pamoja na wakusoma. neno moja muhimu maprof; wanasoma sana. tena vitabu vingi. wanavielewa na kuvichambua hata kutunga mambo mapya yatokanayo na ufahamu huo walio upata. hayo yote ni ya kitambo kidogo yaani wakati pumzi yako Mungu hajaitaka. Akiichukua ndio mwisho wa yote. mmoja wetu ameandika Mungu amulaze mahala alipo mpangia. kumbe unaweza kupangiwa pema au pabaya. sasa jamani maprof mbona hamsomi kitabu kimoja kilicho muhimu kuliko vyote? kitabu kinachofanya upangiwe mahala pema au pabaya. fikiri sas juu ya prof; amepokewa na nani? Yesu au shetani? na huo ndio u milele wake. neno linasema natangulia kwenda kuwawekea makao kama yasingelikuwapo ningeliwaambia. nani hao anaowawekea makao, waliomtii na kumuamini na kumfuata YESU. aliyesulubiwa naye alighamua akasema usinisahau kwenye ufalme wako. akajibiwa hakika nakuambia leo hii utakuwa peponi pamoja nami kwa baba. jifunzeni kwa msiba huu na mkajiandae.