TANZIA Profesa Masuha wa UDSM afariki dunia

mmmmm nina mashaka na weledi wako ndgu
 
Mimi sikuwa faculty of engineering lakini nakumbuka kuwa alikuwa dean wa faculty hiyo baada ya kuondoka Prof Rwakabamba kurudi Rwanda. RIP Senior Prof.
Alianza kuwa dean baada ya Rwakabamba kupata kazi kweye taasisi fulani ya kimataifa kule Nigeria. Baada ya mkataba wa Rwakabamba kuisha alirudi Tanzania na kutumia muda wake pale temporarliya kabla ya kuamua kurudi Rwanda. Masuha alikuwa Dean wa Foe kwa vipindi viliwli, cha kwanza kile alichmorithi Rwakabamba, alikimaliza nadhani mwaka 1991, akarithithiwa na profesa Materu ambaye alipomaliza kipindi chake alikwenda juu kiutawala na baadaye kuhamia World Bank kwenye mradi wa Africa Virtual University. Masuha alichukua tena kipindi cha pili kuanzia mwaka 1998 baada ya Materu kuondoka ingawa aliondolewa madarakani na Profesa Luhanga kwa kutokuelewana kutokana na kuwa na misimamo tofauti kutokana na mambo ya wanafunzi. Interestingly, Profesa Luhanga kabla ya kupanda vyeo, alipandishwa na Masuha kuwa Associate Dean a wa Postgraduate mwanzoni mwa miaka tisini, jambo ambalo lilifanya Luhanga apande hadi kuwa Director of postgraduate studies, Chief Academic officer na baadaye kuwa Vice Chancelleor. Lakini safari hii Luhanga akamgeuka mtu aliyemfungulia mlango.

Mimi binafsi sikufudishwa Masuha lakini alikuwa rafiki yangu sana. Tulielewana wakati wa uhariri wa kitabu chake cha kwanza cha Production Engineering alichotoa baada ya kumaliza muhura wake wa kwanza wa uDean; kwa vile kilikuwa typeset kwa software ya Latex, na tulikuwa wachache sana ambao tulikuwa tunaweza kutoa ushauri wa typeset ya namna hiyo alinisihi sana niwasaidie wale akina Malya kule DUP ili waweze kukitoa mapema sana. Baada ya hapo nikagundua kuwa alikuwa mtu mzuri sana; iIlikuwa ukikaa naye nje ya kazi mkaongea mambo mbali mbali ya maisha alikuwa ni msikivu na mshauri mzuri sana. Mungu aipumuzishe roho yake pema peponi.
 
Kweli yaani chuo ni sehemu nzuri sana good memories yaani hata Mimi nimepa miss sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…