Profesa Ndakidemi atimiza ahadi yake,aipa Milioni 5 familia iliyopoteza watu wanne Kata ya Kimochi mafuriko ya April 25 mwaka huu

Profesa Ndakidemi atimiza ahadi yake,aipa Milioni 5 familia iliyopoteza watu wanne Kata ya Kimochi mafuriko ya April 25 mwaka huu

Ndagullachrles

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
153
Reaction score
161
Profesa Ndakidemi aipa Milioni 5 familia iliyopoteza watu wanne kwenye mafuriko Kata ya Kimochi

MOSHI

Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini (ccm),Profesa Patrick Ndakidemi ametimiza ahadi yake baada ya kuipa shilingi Milioni tano familia iliyopoteza watu wanne ambao walifari Dunia baada ya nyumba yao kuangukiwa na kifusi baada ya mvua kubwa Iliyonyesha usiku wa April 25 Mwaka huu .

Mvua hiyo ambayo ilileta uharibifu mkubwa Katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Kilimanjaro ilisababisha mafuriko ambayo yaliharibu Mali za watu zikiwamo nyumba ,mifugo,vyakula.

Profesa Ndakidemi alitoa ahadi hiyo wakati wa mazishi ya watu hao Katika kata ya Kimochi jimboni humo.

Alisema kiasi hicho cha fedha kitatumika kuwarejeshea makazi yao baada ya nyumba Yao kuanguka na kukosa makazi.

Katika mazishi hayo,Profesa Ndakidemi alitoa ubani wa shilingi laki tano kwa familia hiyo huku akitoa tani mbili za mahidi kwa wananchi wa Kata za Mabogini na Arusha chini ambazo ziliathiriwa na mafuriko hayo.
Akizungumza na Jamiifourms ,mwenyekiti wa ukoo wa Mchaki,Elikunda Chaki amesema profesa Ndakidemi alitimiza ahadi yake Agosti 21 mwaka huu kupitia kwa Katibu wake,Alois Robert .

"Ni kweli mheshimiwa mbunge alimiza ahadi yake na sisi kama familia tumemshukuru kwa kukamilisha ahadi yake",amesema Chaki.

Septemba 11 mwaka huu familia hiyo ya Chaki ikamwandilia barua ya shukrani Profesa Ndakidemi kutokana na kutimiza ahadi yake.
"Mhe.Mbunge wa Moshi Vijijini husika na MADA tajwa hapo juu".
"Sisi wanafamilia wa familia hizi mbili tunapenda kuleta shukrani za kipekee kwa kwa mchango wako uliowezesha ujenzi wa nyumba kwa ndugu zetu katika maafa ya mafuriko katika kata ya Kimochi ,kijiji cha Lyakombilo".

Mhe.Mbunge wa Moshi,familia kwa moyo wa unyenyekevu mkubwa na shukrani nyingi tunakushuru sana wewe binafsi kwa mchango wako wa Tsh,5.000.000 ulioutoa tarehe 22/8/2024 kutoka kwa Katibu wako Alois Robert alioukabidhi kwa niaba yako na kupokelewa na Ndugu Elikunda Chaki kwa niaba ya ukoo wa Chaki"

"Mhe.Mbunge wa Moshi Vijijini ,familia inakuombea kwa mungu akulinde na atimize haja ya moyo wako pia kukuinua katika viwango vingine".

Familia hiyo ikahitimisha salama za pongezi kwa mbunge huyo kwa kunukuu maandiko matakatifu kutoka kitabu cha Mathayo sura ya 25 mstari wa 40 na hapa nanukuu

"Na mfalme akajibu,akawaambia Amin nawaambia kadri mlivyomtendea mmojawapo na hao ndugu zangu waliowadogo,mlinitendea mimi ".mwisho wa kunukuu.

Zaidi ya watu 4,000 wariripotiwa kuathiriwa na mafuriko hayo yaliyosabishwa na mvua kubwa zilizokuwa zikiendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro.

Mbali na hao zaidi ya Kaya 906 ziriripotiwa kuathiriwa na mafuriko hayo huku watu sita wakiripotiwa kufariki dunia kutokana na mvua hizo.

Hiyo ni kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Zephania Sumaye April 29,2024 Mjini Mosh wakati akipokea Misaada ya kijamii kutoka kwa msamalia mmoja kwa ajili ya wahanga wa mafuriko hayo waliopatiwa hifadhi kwenye shule ya Sekondari ya kutwa ya Lucy Lameck.

Akipokea misaada hiyo Sumaye alisema wahanga hao wa mafuriko wana uhaba mkubwa wa chakula ,huku wengi wakiwa hawana malazi huku akimpongeza msamalia huyo kwa moyo wake wa kujitolea kwa kuwasaidia wahanga hao wa mafuriko ikiwemo Magodoro, Unga , Mafuta, Mchele, Sabuni, Taulo za kike , Kalamu, Madaftari pamoja na Mikungu ya ndizi.

Mafuriko hayo yalisababisha mto Rau kujaa huku kingo za Daraja la Otieno lililopo Kata ya Msaranga kusombwa na Maji na kusababisha baadhi ya nyumba kusombwa na Maji huku maji mengi yakiingiq ndani ya makazi ya watu na kusababisha uharibifu wa vitu vingi vya ndani vikiwamo vyakula.
 
Back
Top Bottom