Profesa Nonga: Vifaranga 62,730 kutoka Ubelgiji vilivyokamatwa JNIA vyote vimefia Airport

Hii ndiyo hoja ya msingi! Huyo mwekezaji kama kweli anavyodai mkurugenzi wa DVS kwamba ameona barua baada ya vifaranga kufika Dar basi ni mpuuzi kama wapuuzi wengine! Serikali imefuata matakwa ya sheria!
 
Na hayo ndiyo maswali wanayoyapenda,je kuna sheria yoyote halali inayokataza kununua mifugo au breed zingine nje ya nchi?
Sheria ya katazo haipo ila kuna sheria na miongozo ya kuingiza mifugo na mazao yake kutoka nje! Sasa wafanyabiashara wetu wakubwa wamezoea njia za mkato ili wapige faida kubwa!
 
Kwenye bidhaa zinazoingia nchini kukamilisha taratibu siyo option bali ni prerequisite.

Baada ya vifaranga kufa huyo Importer asubiri kupandishwa kizimbani kujibu tuhuma za kuhujumu uchumi. Mambo yako wazi tusipepese macho.
 
Una kiwango gani Cha elimu
 
Uko sahihi mkuu! Naona hapa kuna ndezi zinatetea ujinga! Huyo mwekezaji amechemka!
 
Una kiwango gani Cha elimu
Nina Masters Degree na nimewahi kuwa CEO wa Taasisi kubwa ya Serikali inayohusiana na importation, kwa sasa ni retired officer.

Njoo tatatibu usilete matusi
 
Kwa hiyo unashauli tusifate sheria ila mambo yakiharibika turekebishe mbele kwa mbele?
 
Hasara haziwezi kuisha iwapo asilimia themanini katika taasisi hiyo ni wabovu na wapenda rushwa.
Nchi inaendeshwa kwa taratibu. Kama aliingiza vifaranga hivyo bila kibali acha avune alichokipanda.
 
Ndio uelewe nchi hii ni ngumu sana.
 
Ingekua ni enzi ya mpendwa wetu Magufuli, angeambiwa yeye ndiye kaamuru hao vifaranga wakamatwe.ila kwa sababu hii ni awamu ya malaika basi hatusikii kelele za akina Mbowe wala Lisu.
Tulishajua kwamba nchi hii hakuna upinzani, wote ni wasaka tonge tu. Tulishaamua ni CCM tu itawale hata miaka mia ijayo.
 
Watendaji wa wizara wa kipindi cha JPM waliochoma vifaranga ndo wale wale walioshindwa kutoa vibali vya awo vifaranga, hakuna jipya apo....mwendo ni uleule bora hata tutokapo kuliko tuendako.
 
Kipi bora, Vifaranga 62,730 kutoka Ubelgiji vilivyokamatwa JNIA vyote vimefia Airport, au Vifaranga 3,000 vilivyo chomwa moto mpaka wa Tanzania na Kenya huko Namanga?
 
Nini tofauti ya yule Dikteta aliyevichoma moto vifaranga kutoka Kenya kule kwenye mpaka wa Namanga na huyu mama mipasho aliyeviua kwa njaa vifaranga kutoka ubeligiji hapo uwanja wa ndege wa DAR?

Chama cha Mambuzi ni kile kile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…