Profesa Nonga: Vifaranga 62,730 kutoka Ubelgiji vilivyokamatwa JNIA vyote vimefia Airport

Atakaye wajibika ni muagizaji sio aliyezuia.

Kwanza kuagiza bila kibali ni kosa tayari kwahiyo kama amekutuma kamwambie ameyakanyaga this time[emoji23]
Utawajibika Kwa mauwaji ya viumbe wasiokuwa na hatia. Kwani vifaranga vilishikiliwa na nani baada kukamatwa. Ni muingizaji au nyie. Shughuli pevu kwenu
 
Kwahiyo DVS alivizuia Kwa kukosa kibali. Je alijua ni viumbe hai au ni mawe. Kwanini hakuvipa huduma ya maji na chakula huku wakisubiri hatma ya vibali. Je hapo airport hao watu wanaozuia kuingia nchini bila vibali Huwa wanaachwa bila maji na chakula. Kuna Sheria za haki za binadamu na haki za wanyama ambazo zote zipo hai Tanzania.
 
Wapuuzi wengi wamejazana serikalini kiasi kwamba nchi nzima tunaonekana wapuuzi wapuuzi.

Hapo ni maagizo ya kukomoana na kukamiana.

Mungu atawamulika wajinga wote na wataenguliwa bila kujali nafasi zao
 
Huyo Mkurugenzi bwana Prof. Ni msemaji ws TRA?
 
Hujanielewa, namaanisha wawaishwe na pia wawe kwenye karantini.
Kweli kabisa hajakuelewa. Yaani wanakazania vibali tu wakati huduma za maji na chakula hawakuwapa. Wamefanya makosa makubwa sana Kwa kushindwa kuwapeleka kwenye karantini ambayo ndiyo ingetoa hitimisho ya vibali na magonjwa huku vikipatiwa huduma zote muhimu ambazo gharama angelipia muingizaji. Kuna watu wanasafirisha mbwa kwenda uingereza. Kufika kule mbwa waliwekwa karantini ya siku 14 kusubiri vipimo vya magonjwa na huku wakipatiwa huduma ya chakula na maji.
 
Bado huelewei kitu kwenye hizi taratibu.

Export permit ni kibali cha kule vilipotoka lakini kuingiza nchini kwetu lazima kuwe na import permit na cheti cha Afya.

Jaribu kutafakari vema haya mambo weka interest pembeni kwanza
Sasa hiyo Export Permit ilipokelewa na hao watu ?
 
Wewe ni Sukuma gang tu mnaongoza kwa Roho mbaya kupoteza uhai wa viumbe hamwoni shida bahati mbaya mlizaliwa Bara la giza mngezaliwa Ulaya au Marekani dunia ingejaa mateso ya kila namna.
Wafanyabiashara wa kipumbavu wanataka kutuingizia magonjwa ya mlipuko tukose kuku hapa nchini! Niko upande wa maafisa wa serikali!
 
Hakuna cha kufa hapo vimeshangia kwenye circle sasa hivi mnakula nyama zake🤣🤣🤣
 

Unajitia ujuaji usio na maana.
Wapelekwe karantini kwa mujibu wa Sheria gani?
Hizi taratibu zilishaandika Kisheria sio kujisikia tu unafanya.

Humu mnakomenti kwa sababu mna bando, mkielimishwa mnakimbilia oooh mbona unatetea sasa kama tunajua taratibu kwanini tusiwambie nyie msiojua?
 

Huna ujualo utasubiri uone kama kuna mtu atachukuliwa hatua zaidi ya aliyeagiza vifaranga.

Enzi za JPM vilichomwa moto kabisa, enzi hizi za Samia Serikali imekuwa na uungwana mwingi ndio maana muagizaji aliambiwa avirejeshe vilikotoka
 
Huna ujualo utasubiri uone kama kuna mtu atachukuliwa hatua zaidi ya aliyeagiza vifaranga.

Enzi za JPM vilichomwa moto kabisa, enzi hizi za Samia Serikali imekuwa na uungwana mwingi ndio maana muagizaji aliambiwa avirejeshe vilikotoka
Lakini majibu tutayapata tu yawe positive au negative.
 
Hujui lolote ni kelele tu na kulazimisha ueleweke. Hata Sheria ya mifugo kuingia nchini hujui. Weka Sheria hapa . Kama wewe ni afisa huko au muuza kuku mwenye wivu na wauza kuku wengine ni lazima muwajibike. Na lazima mama kaisha yapata kuwa mnataka kumuhurabia kupitia kichaka Cha Sheria badala ya kutumia busara
 
Wewe ni Sukuma gang tu mnaongoza kwa Roho mbaya kupoteza uhai wa viumbe hamwoni shida bahati mbaya mlizaliwa Bara la giza mngezaliwa Ulaya au Marekani dunia ingejaa mateso ya kila namna.
Chief sheria za nchi lazima zifuatwe!
 

Wahusika wote wamefanya makosa makubwa sana! Wanafahamu joto Ulaya Sasa hivi ni nyuzi joto 0 mpaka 7 hivi. Hapo bongo ni nyuzi 32na zaidi. Joto lenyewe linatosha kuviua. Kwa kutambua hilo, wangeviachia kwa masharti na utaratibu maalum.
 
Bora aliyechoma moto na akaonesha msimamo wake hadharani
 
Asante mkuu kwa ushauri mzuri
Ushauri wa namna hii ndio ulioifikisha Nchi hii hapa ilipo kila mtu atakikufuata sheria kwa kutegemea njia za mkato na ndio maana kiongozi akifuata sheria tu anaonekana ni mtu mbaya/dikteta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…