Profesa Nonga: Vifaranga 62,730 kutoka Ubelgiji vilivyokamatwa JNIA vyote vimefia Airport

Mamlaka za kibongo zina ukiritimba sana!!??
so vifaranga vimekufa kwa njaa!!?
Tujifunze kufata utaratibu

Tujifunze kupanga mambo yetu vizuri kabla ya kuanza utekelezaji.

Tujifunze pia kujua "utamaduni" wa taasisi na vyombo vyetu vya maamuzi.

Haya yanaweza kutusaidia KUYOKUOATA HASARA zinazoweza kuepukika.
 
Nchi hii ina wapuuzi wengi sana,ndio maana Proffesa Asad alisema watumishi wengi na viongozi serikalini wana uwezo mdogo sana

Ndio maana hatuendelei, maana wenye uwezo na akili wengi wakipata nafasi wanakimbilia nje,kuanzia wawekezaji, wanasiasa na wasomi,tunabaki na wapumbavu watupu

Wanaofaa kuwa maraisi wazuri na wabunge wamekimbia nchi,wafanyabiashara wakubwa wanawekeza nje,wasomi nao wakipata shavu nje hawarudi.
Wafuate huko walipokimbilia we nyau.
 
Acha ujinga,hivi vitasisi vya Serikali kuna baadhi ya Watendaji ni wapumbavu sana TRADE BARRIERS hasa Wizara ya Kilimo.
huna sababu ya kuhamaki, nimekutana nayo sana hayo madudu, je tuna mfumo wa kuwajibishana inapotokea issue kama hii. Cha msingi ni kufuata taratibu tu, kama ukikatisha kwa mazoea ndo kama hivi. Nani hajui haya mambo kama yapo?????
 
Unachekesha. Kwa hiyo kwa kutokujibiwa ndio anakosa mtu wa kumlaumu? Au kinyume chake?
Kama aliomba kibali Wizarani na hakupata majibu, kwa nini aliingiza mzigo? Mzigo ungekuwa na hitilafu bado tungewalaumu Wizara kwa kutodhibiti uingizaji bidhaa holela. Namsikitikia mkulima huyu. Ila kama alifuata taratibu akadai haki/fidia mbele ya sheria.
 
huna sababu ya kuhamaki, nimekutana nayo sana hayo madudu, je tuna mfumo wa kuwajibishana inapotokea issue kama hii. Cha msingi ni kufuata taratibu tu, kama ukikatisha kwa mazoea ndo kama hivi. Nani hajui haya mambo kama yapo?????
Utaratibu usiyofuata sheria na maadili ya kazi siyo utaratibu.Nowdays dunia ni kijiji mfanyabiashara anaweza nunua bidhaa mahali popote kulingana na uhitaji wake wa kisheria na kibiashara.Tunapozungumzia uzalendo wa kulinda mifugo yetu na vyakula vyeti isiwe sababu ya kuwanyima watu fursa ya kupata vibali kwa muda mwafaka.
 
Bahati mbaya mimi na wewe tunajadiliana hapa kama kukumbushana tu, hatuna chochote tunachokijua juu ya sakata hili zaidi ya hizi taarifa za mtandaoni. Kawaida ya ukweli huchelewa kuja, tuvute subira.
 
Kama aliomba kibali Wizarani na hakupata majibu, kwa nini aliingiza mzigo? Mzigo ungekuwa na hitilafu bado tungewalaumu Wizara kwa kutodhibiti uingizaji bidhaa holela. Namsikitikia mkulima huyu. Ila kama alifuata taratibu akadai haki/fidia mbele ya sheria.
Sasa hapo ni kujua utaratibu nini kinaanza na kama kulikuwa na mazungumzo kabla na Wizara kuwa wewe agiza mzigo by the time unafka kibali kitakuwa kimetoka. In any case, kama aliomba kibali, Wzara inawajibika kumjibu kuwa kapewa au la, badala ya kukaa kimya.
 
Utaratibu usiyofuata sheria na maadili ya kazi siyo utaratibu.Nowdays dunia ni kijiji mfanyabiashara anaweza nunua bidhaa mahali popote kulingana na uhitaji wake wa kisheria na kibiashara.Tunapozungumzia uzalendo wa kulinda mifugo yetu na vyakula vyeti isiwe sababu ya kuwanyima watu fursa ya kupata vibali kwa muda mwafaka.
Niliwahi kurudisha mbuzi nilikowatoa sababu ya kukosa vyeti vya bwana mifugo wa wilaya husika. Ni utaratibu, niliumia lakini ndo ukweli.
 
Je huko ulikokua hakukuwa na Wataalam wa kukusaidia kupata vyeti katika zama hizi utandawazi?
 
Tujifunze kufata utaratibu

Tujifunze kupanga mambo yetu vizuri kabla ya kuanza utekelezaji.

Tujifunze pia kujua "utamaduni" wa taasisi na vyombo vyetu vya maamuzi.

Haya yanaweza kutusaidia KUYOKUOATA HASARA zinazoweza kuepukika.
Hasara haziwezi kuisha iwapo asilimia themanini katika taasisi hiyo ni wabovu na wapenda rushwa.
 
huna sababu ya kuhamaki, nimekutana nayo sana hayo madudu, je tuna mfumo wa kuwajibishana inapotokea issue kama hii. Cha msingi ni kufuata taratibu tu, kama ukikatisha kwa mazoea ndo kama hivi. Nani hajui haya mambo kama yapo?????
Tatizo ofisi za umma zimejaa rushwa. Watoaji vibali kama waliombwa, waulizwe kwa nini hawakutoa?

Kama hawakutoa kwa uzembe na kusubiria rushwa, wafukuzwe kazi, na mafao yao yatumike kumfidia mkulima.
 
Ndicho walichotaka.

Unawezaje kuxuia vifaranga what's next ni lazima vife.

Vifaranga havikuwa na mtetezi.
1. Le Professeri anasema wenye vifaranga wana kesi ya kujibu?au sijaelewa?

2. Anaongea hayo wakati V8 imepaki kumsubiria boss impeleke hotelini, kisha

3. Asubuhi aanze Tena safari ya kurudi Dodoma baada ya kula per Diem ya kuja kuangalia vifaranga Dar airport
 
Team walamba asali wamekaa kimya , kipindi cha magu kuchomwa wale vifaranga sidhani ata kama buku wanafika waliimba kila nyimbo za kumkashifu jpm ,hili la vifaranga zaidi ya elfu sitini imewabidi walamba asali wafunike makalio yao na kuacha mbupu zinaning'ia kwa aibu.
 
Wafuate huko walipokimbilia we nyau.
Ni ukweli kwamba watendaji wengi wa Serikali wana uwezo mdogo sana na wamekosa maadili, hawa ni kikwazo kwa maendeleo ya nchi.

Kulikuwa na uwezekano wa kuwaweka karantini vifaranga, wakawa hai; na wakati huo huo kulinda usalama wa nchi dhidi ya maambukizi ya magonjwa yanayoweza kysababishwa na mifugo kutoka nje.

Akili ndogo na ukosefu wa maadili kwa watendaji wa Serikali, ni kikwazo kwa maendeleo ya nchi. Ucheleweshaji wa kibali, uwezekano mkubwa walikuwa wanasubiria rushwa, na muagizaji hakuwa tayari kutoa rushwa.
 
Kama aliomba kibali Wizarani na hakupata majibu, kwa nini aliingiza mzigo? Mzigo ungekuwa na hitilafu bado tungewalaumu Wizara kwa kutodhibiti uingizaji bidhaa holela. Namsikitikia mkulima huyu. Ila kama alifuata taratibu akadai haki/fidia mbele ya sheria.

Na pia uwauluze hao watoa vibali. Kama muagizaji aliomba vibali kwa nini hawakutoa? Watumishi wa Serikali wapuuzi kama hao wa Wizara ya kilimo wanatakiwa kufukuzwa kazi mara moja, na wapoteze haki zao zote. Kila mahali wanategeshea rushwa.
 
1. Le Professeri anasema wenye vifaranga wana kesi ya kujibu?au sijaelewa?

2. Anaongea hayo wakati V8 imepaki kumsubiria boss impeleke hotelini, kisha

3. kesho asubuhi aanze Tena safari ya kurudi Dodoma baada ya kula per Diem ya kuja kuangalia vifara Dar airport
Inasikitisha kwa kweli.
 
Back
Top Bottom