Profesa Nonga: Vifaranga 62,730 kutoka Ubelgiji vilivyokamatwa JNIA vyote vimefia Airport

Profesa Nonga: Vifaranga 62,730 kutoka Ubelgiji vilivyokamatwa JNIA vyote vimefia Airport

Kama nawaona ofisini,
Lazima kila mtu alikuwa anaviulizia,
but kama kawa kila mtu anamsukukia uskani mwengine, no one taking action

Hasara
 
Siamini chochote kutoka hii serikali, kuna mtu kanyimwa 10% basi kaamua kumwaga mboga kakalia vibali,kila kona ya serikali imejaa huu utopolo
 
View attachment 2466380
Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo,Herzon Nonga akionesha Vifaranga vya kuku wa mayai vilivyozuiwa kuingia nchini,kutokuwa na vibali na cheti cha afya katika kago ya mizigo ya uwanja wa ndege wa Juliasi Nyerere,jijini Dar es Salaam jana.

Kukamatwa kwa vifaranga vilivyokuwa vikiingizwa nchini kumeibua masuala ya uwajibikaji na kutofuata sheria miongoni mwa viongozi wa Serikali na wadau wa sekta ya ufugaji wa kuku.

Vifaranga vilivyozuiliwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 22, 2022, ni mali ya Kampuni ya Phoenix Farms Limited iliyopo Mkuranga mkoani Pwani.

Vifaranga hivyo vilivyofungwa kwenye maboksi 697 yenye thamani ya Sh200.262 milioni, vilikamatwa wakati wa ukaguzi walipokuwa wakiingizwa nchini kutoka Ubelgiji.

Mwananchi imebaini kuwa Kampuni ya Phoenix Farms Limited iliwasilisha barua ya maombi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuomba kibali cha kuagiza vifaranga kutoka nchi hiyo ya Ulaya.

Pia, imethibitishwa kuwa waagizaji walikuwa wamepewa cheti cha mifugo na mamlaka ya Ubelgiji.

Baadhi ya wadau katika sekta hiyo wameishutumu wizara hiyo kwa kushindwa kutoa leseni za uagizaji bidhaa kutoka nje na kuchukua hatua za ziada kuwalinda wawekezaji wa ndani.

“Mamlaka zimeshughulikia suala hilo kwa njia isiyo ya haki. Walitakiwa kutoa kibali hicho kwa kuzingatia kwamba nchi haina uwezo wa kuzalisha kuku wa kukidhi mahitaji yake,” alisema mdau kwa sharti la kutotajwa jina.

“Vifaranga hivyo vingeweza kupelekwa kwenye shamba la kampuni hiyo na kuwekwa karantini humo. Vingegundulika kuwa na afya njema mwekezaji angeweza kuadhibiwa na vifaranga virudi kwake,” kiliongeza chanzo hicho.

Alipotafutwa, Ofisa Mkuu wa Phoenix Farms Limited, Irfan Mitha alikataa kutoa maoni yake kuhusu uhalali wa hati mbili zilizotajwa hapo juu.

“Niko busy leo; nipigie simu kesho, nitakuwa kwenye nafasi ya kutoa maoni yangu,” aliliambia gazeti hili.

Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo (DVS) katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Hezron Nonga alisema ombi la kibali cha kuagiza cha Desemba Mosi, 2022, halijafika ofisini kwake wala wizarani.

“Tuliona barua ya maombi ya vibali kutoka nje ya nchi, muda mfupi baada ya vifaranga kukamatwa JNIA. Kadhalika, cheti cha mifugo kilichoandikwa na Shirikisho la Ubelgiji la Usalama wa Mnyororo wa Chakula (FACFAS),” alisema Profesa Nonga.

Akitoa taarifa ya vifaranga hivyo, Profesa Nonga alisema vyote 62,730 vimekufa baada ya kutelekezwa kwenye uwanja wa ndege.

“Mwagizaji ana kesi nyingine ya kujibu mbele ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuwa mipango ya uteketezaji wa kuku inaendelea,” alisema.

Chanzo: Mwananchi
Mtu kashapiga hesab zake za makaratas. Mtaj 200m.. vifaranga 67k... Nikuza kila kifaranga elf3 sikos 800m
 
Mnaanza kushutumu mapema sbb vimekufa vingetuhusiwa na pakatokea magonjwa lawama zingeanza
 
Hapana, wizara Kwa njia rahisi ilitakiwa ithibitishe Kwa vipima hivyo vifaranga, zoezi la siku Moja , huo ni uzembe wa watumishi wa serikali, hovyo kabisa, hata huyo Mkurungenzi akili zake ni kama layman, kaenda airport bila watalaam.
Sheria inasema hivyo?

Taratibu za kuingiza vifaranga zipo, au hazipo, zilifuatwa?
Huyo Mkurugenzi ni mtaalam, huoni ni Profesa kabisa katika eneo hilo la mifugo?

Watu kama nyinyi ndio mnaopindisha kila kitu kwa matakwa yenu, bila ya kufuata taratibu tulizojiwekea zitumike.
Ilaumu hiyo kampuni, na baadhi ya matapeli walio wizarani, waliowadanganya na kukiuka taratibu za uingizaji wa hao vifaranga.
 
Sasa kukosa kibali ndio achukue uamuzi wa kuagiza vifaranga? Sawa huenda kunakosa kwenye mamlaka lakini kwann na yeye aagize bila kibali? Kunawakati mtu anajitafutia matatizo alafu mwishowe anakuja kutafuta lawama. Hata haya masikitiko na lawama za mtandaoni haziwezi msaidia.
 
Nimesoma The Citizen wwameandika:
1) Veterinary certificate inatakiwa kutolewa baada ya kibali cha uhagizaji. Lakini Phoenix Farm Limited walipewa kabla ya kibali kutoka.
2) Phoenix Farm Limited walipiga simu wizarani kuomba kibali lakini wizara ikasema haiwezi kutoa kibali kutokana bird flu.
3) Wizara ikawatafutia Phoenix suppliers wa ndani na walikuwa tayari ku supply idadi waliyokuwa wanataka ku import. Lakini Phoenix wakakataa.
 
Hivi huyu serikali ni nani na anaishi wapi....maana amekuwa chanzo cha matatizo mengi....na kwanini wananchi wenye nchi yao hawamuwajibishi au kumnyang'anya madaraka yake!?
 
Hii nchi ina ujinga mwingi kweli kweli. kufanya biashara hapa lazima uwe master wa kona kona vinginevyo unafilisika.
Kuna vitu lazima ufuate utaratibu na hasa mazao ya mifugo na ndege.Moshi Kilimanjaro wazalishaji wa vifaranga waliteketeza vifaranga baada ya kukosa soko la kuviuza huku wengine wanaingiza vifaranga uenda supply and demand ina shida au hakuna tarifa za kutosha kwenye uzalishaji na mahitaji ya ndani.
 
View attachment 2466380
Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo,Herzon Nonga akionesha Vifaranga vya kuku wa mayai vilivyozuiwa kuingia nchini,kutokuwa na vibali na cheti cha afya katika kago ya mizigo ya uwanja wa ndege wa Juliasi Nyerere,jijini Dar es Salaam jana.

Kukamatwa kwa vifaranga vilivyokuwa vikiingizwa nchini kumeibua masuala ya uwajibikaji na kutofuata sheria miongoni mwa viongozi wa Serikali na wadau wa sekta ya ufugaji wa kuku.

Vifaranga vilivyozuiliwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 22, 2022, ni mali ya Kampuni ya Phoenix Farms Limited iliyopo Mkuranga mkoani Pwani.

Vifaranga hivyo vilivyofungwa kwenye maboksi 697 yenye thamani ya Sh200.262 milioni, vilikamatwa wakati wa ukaguzi walipokuwa wakiingizwa nchini kutoka Ubelgiji.

Mwananchi imebaini kuwa Kampuni ya Phoenix Farms Limited iliwasilisha barua ya maombi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuomba kibali cha kuagiza vifaranga kutoka nchi hiyo ya Ulaya.

Pia, imethibitishwa kuwa waagizaji walikuwa wamepewa cheti cha mifugo na mamlaka ya Ubelgiji.

Baadhi ya wadau katika sekta hiyo wameishutumu wizara hiyo kwa kushindwa kutoa leseni za uagizaji bidhaa kutoka nje na kuchukua hatua za ziada kuwalinda wawekezaji wa ndani.

“Mamlaka zimeshughulikia suala hilo kwa njia isiyo ya haki. Walitakiwa kutoa kibali hicho kwa kuzingatia kwamba nchi haina uwezo wa kuzalisha kuku wa kukidhi mahitaji yake,” alisema mdau kwa sharti la kutotajwa jina.

“Vifaranga hivyo vingeweza kupelekwa kwenye shamba la kampuni hiyo na kuwekwa karantini humo. Vingegundulika kuwa na afya njema mwekezaji angeweza kuadhibiwa na vifaranga virudi kwake,” kiliongeza chanzo hicho.

Alipotafutwa, Ofisa Mkuu wa Phoenix Farms Limited, Irfan Mitha alikataa kutoa maoni yake kuhusu uhalali wa hati mbili zilizotajwa hapo juu.

“Niko busy leo; nipigie simu kesho, nitakuwa kwenye nafasi ya kutoa maoni yangu,” aliliambia gazeti hili.

Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo (DVS) katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Hezron Nonga alisema ombi la kibali cha kuagiza cha Desemba Mosi, 2022, halijafika ofisini kwake wala wizarani.

“Tuliona barua ya maombi ya vibali kutoka nje ya nchi, muda mfupi baada ya vifaranga kukamatwa JNIA. Kadhalika, cheti cha mifugo kilichoandikwa na Shirikisho la Ubelgiji la Usalama wa Mnyororo wa Chakula (FACFAS),” alisema Profesa Nonga.

Akitoa taarifa ya vifaranga hivyo, Profesa Nonga alisema vyote 62,730 vimekufa baada ya kutelekezwa kwenye uwanja wa ndege.

“Mwagizaji ana kesi nyingine ya kujibu mbele ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuwa mipango ya uteketezaji wa kuku inaendelea,” alisema.

Chanzo: Mwananchi
"Kuchoma moto vifaranga kutoka Kenya ulikuwa uamuzi mbaya". Sijui aliitoa nani hii kauli!!!
 
Wewe mgeni nchii hii au unahisi Kila mtu ni Mjinga Kama wewe?
Asante ndugu. Ila kumbuka vifaranga siyo kama nguo au spea za magari. Ni delicate goods. Unapoagiza lazima uhakikishe njia ni nyeupe, yaani makaratasi yakamilike.

Kuagiza vifaranga ni mchakato pia. Lazima uweke booking shambani, ujue siku ya kutotolewa, ujue na chanjo za mwanzo na siku ya kupakia.

Huwezi kuacha mayai kwenye incubator, huku ukijua ni siku 21, ndo uanze kushughulikia documents. Obviously hutatoboa. Maana muda utakuwa mfupi.

Ndo maana nasema, huyu mwagizaji alizoea short cuts. Na every short cut is a wrong cut. Huyu amezoea kupita airport kihivyohivyo tu. Ghafla amekuta mfumo umebadilika. Anayemjua kahamishwa au kagundulika mchezo wao.

Tunahitaji kukusanya mapato ndugu
 
Daah inamaana kulikuwa hakuna namna nyingine ya kusolve na hao walioleta hao vifaranga? Wenye mamlaka wanashindwa hata kutafakari vizuri kweli? Nikweli kabisa inawezekana waliowaleta walikosea kufuata utaratibu na sheria lakini nadhani kulikuwa na namna bora ya kusolve hili
 
Matatizo haya yanayosababishwa na mamlaka zetu ndiyo yanayofanya watu waamue kupitisha kinyemera biashara zao maana ukipitisha njia halal badala ya kusidiwa unpuuzwa
 
Huu uuwaji utakwenda na wengi. Sababu naona watu wanataka kumuharibia mama. Muda utasema
 
Back
Top Bottom