Profesa Nonga: Vifaranga 62,730 kutoka Ubelgiji vilivyokamatwa JNIA vyote vimefia Airport

Profesa Nonga: Vifaranga 62,730 kutoka Ubelgiji vilivyokamatwa JNIA vyote vimefia Airport

wewe huna akili, unatangulizaje kitu huna kibali cha kuingiza? huo si upumbavu... kama una huruma na vifaranga mbona unavila wakiwa wakubwa. Nyambaf! ungeenda kuwalisha basi airport
Badala ya kumjibu kwa hoja, unamwita mpumbavu. Kutukana ni uthibitisho wa awali kuwa mtu hayupo sawasawa. Tuna watendaji wa Serikali ambao upeo wao unaishia kwenye pua zao. Serikali haitakiwi kutenda kama unavyofikiria. Serikali inatakiwa kuwa mwezeshaji na siyo mfukarishaji.

Nchi hii haiendelei kwa sababu ya watendaji wa Serikali wenye uelewa duni. Hutatui kosa kwa kufanya uharibifu.

You need to find best solution for every mistake. Siyo kutatua tatizo kwa kusababisha hasara. Wajinga wanadhani hiyo hasara ni ya huyo muingizaji vifaranga pekee. Hawajui kuwa hiyo mil 200 imeenda Ubelgiji, wablegiji hawajapata hasara yoyote, sisi kama nchi ndio tumepata hasara. Uchumi wa Mtanzania mmoja mmoja ndiyo uchumi wa Tanzania. Kumfukarisha Mtanzania mmoja ni kuifukarisha nchi. Hiyo milioni 200 ingegusa maisha ya wengi. Kulikuwa na njia kumwadhibu huyo ambaye hakufuata utaratibu, kama alikosea bila ya kufanya maangamizi ya kiuchumi. Kwa kumpiga faini, faida yake ingepungua lakini kwa upabde wa nchi tusingekuwa tumepoteza chochote kwa sababu hata faini ambayo angelipa ingekuwa imebakia nchini.

Nchi hii atitude ya watumishi wa umma, walio wengi ni zero.
 
na ww unajifanya unajua kwasababu yameshatokea.. Unatumaje vifaranga kwenye ndege bila kibali chochote, hiyo si dharau. Na huwezi jua pengine ndio kawaida yao, wanaingia bila vibali airport watu wanapiga rushwa maisha yaendelee, ni bahati unakuta siku hiyo kuna ki-system kilitumwa kichunguze kikakutana na huo ujinga
Huwezi nidanganya ni mengi nimeyaona kwenye hiyo Idara,ngoja nikupe mfano;mwaka 2014 kulikuwa na njaa Wilaya ya Musoma Vijijini na Ukerewe wenye mitaji wakawa wananunua mahindi kutoka Kenya,unajua kilichotokea,baadhi ya watumishi wa Wizara hiyo wakasema mahindi ya Kenya yana sumu na yakapigwa marufuku lakini kwa wakazi wa mipakani na Kenya waliendelea kununua mahindi hayo hayo na hata hao baadhi ya maafisa walikuwa wanakula mahindi bila kudhurika.Figisu figisu kwenye biashara husababisha magendo.

Kuna mteja kutoka Kenya mwaka juzi alinunua alizeti kutoka Singinda magunia thelathini alipofika mpakani aliambiwa alizeti haiwezi toka Tanzania kwenda nje kwa sababu Tanzania tuna viwanda vya kukamua mafuta hivyo kama anataka kuuza airudishe alizeti aiuze Tanzania kwa sababu tuna uhaba wa mafuta ya kula.Hii mifano ni michache ni mengi tuliyoona kwa macho.Na si kweli kuwa mwagizaji wa vifaranga hakufuata utaratibu,alifuata ila kuna taarifa potofu za usalama na kuthamini bidhaa za ndani.
 
ndicho cha kushangaza na vingepita vikaja leta madhara ungesikia tena maofisa wa hovyo waondolewe.Tararatibu zipo wazi na siyo Tanzania tu na nje ya Tanzania huwezi ingiza bidhaa za nyama bila vibali hata kama ni nyama choma.Tumeshasikia sana mafua ya ndege sasa mlitaka mtu ajiletee tu vifaranga bila pewa kibali?
Sisi ni watu wa kulalamika tu mkuu. Yani humu utakutana na wajuaji wa kila aina. ishu kama hii mtu analeta ushabiki. sijaelewa kosa la maafisa ni nini hapo? walitaka airport igeuke Mr Kuku farms, au viachwe viende kwenye destination yake, na je kuku hata mmoja kati ya hao angekuwa na ugonjwa na tayari wako inland ingekuaje? hii ngoma imepangwa in the most humane way possible wafe, kwasababu mambo ya kuchoma rais alishakataza
 
yani wabongo mnajifanyaga mnajua mambo kwasababu ya Hindsight. Nchi ina sheria na maofisa lazima wafuate sheria. Hivi ingekua Marekani au nchi nyingine inayojielewa hao vifaranga wangechomwa kitambo, kwanza hao waBelgiji wasingehata thubutu kuwaweka kwenye ndege kabla vibali havijarudi
Yawezekana hiyo Marekani na Ubelgiji unaisikia tu, hujawahi hata kufika.

Sisi wengine, tumepata bahati ya kusihi mataifa mbalimbali ya Ulaya, America na Australia. Watumishi wa Serikali wana falsafa inayowaongoza, SERIKALI NI MWEZESHAJI, na siyo mfukarishaji. Kufanya tendo lolote la kumfukarisha mtu ni pale ambapo kuna uthibitisho wa kutosha kuthibitisha kuwa hakuna namna nyingine yoyote inayoweza kufanyika bila kupata madhara makubwa.

Imgekuwa ni Ulaya, siku ile ile wataalam wa wizara wangeebda kuwapima vifaranga kuthibitisha kama ni salama. Na kama ni salama, wangeruhusiwa kupita aurport. Baada ya pale zingefuata taratibu nyingine, na kufuatilia kulikuwa na tatizo gani mpaka vifaranga wakafika nchini bila vibali:

1) Mwingizaji aliziona mamlaka zinazohusika?

2) Muingizaji kama aluziona mamlaka zinazohusika, mamlaka hizo zilimsaidia vipi kuhakikisha anafuata taratibu zote?

3) Kama alikamilisha taratibu alizoelekezwa, ucheleweshaji wa kibali ulifanywa na taasisi gani, na ofisa gani?

4) Nini kifanyike ili tatizo hilo lisitomee tena?

Wenzwtu wameendelea kwa sababu ya kuwajali na kuwawezesha watu wao. Lakini watumishi wa Serikali kwa nchini mwetu ni watu negative wanaofikiria kuwa kazi ya Serikali ni kuwakomoa au kuwakomesha wananchi.
 
ndicho cha kushangaza na vingepita vikaja leta madhara ungesikia tena maofisa wa hovyo waondolewe.Tararatibu zipo wazi na siyo Tanzania tu na nje ya Tanzania huwezi ingiza bidhaa za nyama bila vibali hata kama ni nyama choma.Tumeshasikia sana mafua ya ndege sasa mlitaka mtu ajiletee tu vifaranga bila pewa kibali?
Je kuna report yoyote ya kisayansi iliyofanyiwa kazi na kuona kuwa vifaranga hivyo vilikuwa na tatizo/ugonjwa wowote?Na kama kulikuwa na mambo hayo mwagizaji wa Vifaranga alichukuliwa hatua gani?Mkasubiria vife mje na sababu kuwa vingeleta madhara kwa mawazo ya kufikirika.Huyo aliyeingiza vifaranga kwa nini hakupigwa faini na kumwambie avirudishe vilikotoka kwa gharama zake ili asije rudia kuvunja utaratibu?Vitu vingine vyaihitaji moyo wa hekima.
 
Yawezekana hiyo Marekani na Ubelgiji unaisikia tu, hujawahi hata kufika.

Sisi wengine, tumepata bahati ya kusihi mataifa mbalimbali ya Ulaya, America na Australia. Watumishi wa Serikali wana falsafa inayowaongoza, SERIKALI NI MWEZESHAJI, na siyo mfukarishaji. Kufanya tendo lolote la kumfukarisha mtu ni pale ambapo kuna uthibitisho wa kutosha kuthibitisha kuwa hakuna namna nyingine yoyote inayoweza kufanyika bila kupata madhara makubwa.

Imgekuwa ni Ulaya, siku ile ile wataalam wa wizara wangeebda kuwapima vifaranga kuthibitisha kama ni salama. Na kama ni salama, wangeruhusiwa kupita aurport. Baada ya pale zingefuata taratibu nyingine, na kufuatilia kulikuwa na tatizo gani mpaka vifaranga wakafika nchini bila vibali:

1) Mwingizaji aliziona mamlaka zinazohusika?

2) Muingizaji kama aluziona mamlaka zinazohusika, mamlaka hizo zilimsaidia vipi kuhakikisha anafuata taratibu zote?

3) Kama alikamilisha taratibu alizoelekezwa, ucheleweshaji wa kibali ulifanywa na taasisi gani, na ofisa gani?

4) Nini kifanyike ili tatizo hilo lisitomee tena?

Wenzwtu wameendelea kwa sababu ya kuwajali na kuwawezesha watu wao. Lakini watumishi wa Serikali kwa nchini mwetu ni watu negative wanaofikiria kuwa kazi ya Serikali ni kuwakomoa au kuwakomesha wananchi.
Kweli kabisa.
 
Yaonekana huyu mkulima amezoea njia za mkato. Na hapa yawezekana watu wake wa airport anaowatumia siku zote walichanganyana.

Ili dili kama hizi zibumbuluke, lazima walishawahi kuzulumiana michongo ya nyuma. Haiwezekani hivi hivi
Wewe mgeni nchii hii au unahisi Kila mtu ni Mjinga Kama wewe?
 
Ni ujinga mtupu unaofanywa na watumishi wa Serikali. Mpaka siku Serikali itakapoamua kila sehemu kuajiri the best best, ndiyo matatizo kama haya yataisha.

Kuna watemdaji wa Serikali ambao ni wajinga kupindukia. Wanadhani Serikali kazi yake ni kuumiza wananchi. Wanashindwa kuelewa kuwa Serikali inatakiwa kuwa mwezeshaji.

Hao maofisa wa Serikali walitakiwa kujiuliza wafanye nini ili muingizaji vifaranga asiingie hasara lakini pia nchi iwe salama.

Wangeweza kuruhusu vifaranga kuingia wakapelrkwa shambani kwake kwa ysimamizi maalum. Na huko wawekwe karantini, na walindwe kwa gharama ya mwingizaji. Wapimwe kwa gharama ya mwingizaji. Wakionekana hawana tatizo, aendelee na ufugaji, lakini apigwe faini.

Lakini kwa upande mwingine ilitakiwa kuangalia kama aliomba kibali cha kuingiza, aliomba lini, kwa nini watoa vibali hawakutoa vibali. Na kama walishindwa kutoa vibali kwa sababu ya uzembe au kutengeneza mazingira ya rushwa, basi hao maofisa wa wizara ya kilimo, wafukuzwe kazi na kupoteza stahiki zao zote.
Kwa ubongo wako ulivyo unadhani huyo Prof. sio best!!?
 
Hii nchi ina ujinga mwingi kweli kweli. kufanya biashara hapa lazima uwe master wa kona kona vinginevyo unafilisika.
Unaweza kushangaa labda mkurugenzi alitaka kupozwa, ikashindikana ndio maana akaamua.

Nchi hii kama una mkono mfupi hutoboi
 
Inasikitisha sana kwa vifaranga kufungiwa ndani kwa siku zote hizo hadi vikafa huku "wataalam" wakijua kuwa hawa ni viumbe hai tena dhaifu ambao umri wao ni chini ya siku 5. Sasa hapo sijui kama walikuwa wamejifungia ofisini kwao huku wamewasha AC wakiitisha makaratasi yaende ofisini ili waruhusu vifaranga vipate maji na chakula! Just papers zinacost uhai wa vifaranga na sh 200M na bado watu wapo pride na kilichofanyika kwa kivuli cha "fuata utaratibu" Hadi kifaranga kitoke Ulaya hadi hapa kwetu lazima kuna taratibu zimefuatwa. Akili ya kawaida inafikirisha hivyo. Lazima export permit imetolewa na makaratasi mengine. Kukosekana karatasi moja au mbili upande wetu ambayo si ajabu haikuwa na uhusiano na masuala ya afya ya vifaranga ni changamoto ambayo ingekuwa addressed na serious officer kwa udharura hadi kusaidia kutoa maamuzi kwa haraka kwa kujua ana deal na a day old chicks. Kwamba vifaranga vimefungiwa siku 7 wakati wanaendelea kufuatilia nyaraka ni ngumu kumeza. Walijua matokeo yake bila shaka! Mimi nina imani kuna tobo upande wa wahusika. Walistahili kumsaidia importer badala ya kumtelekeza. Hata kama utaratibu ungeonekana umekosewa basi maamuzi yangetoka ndani ya 12 hours ili hatima ya vifaranga ijulikane na si kuwaacha wafie kwenye mabox kisha tujuvune kwa hili.
 
Huo utaratibu ndo shida unaweza chukua mwaka kukamilisha utaratibu. Nikupe mfano mdogo tu. Nimelipia umeme tangu mwaka 2021 November. Hadi Sasa sijafungiwa. 2023. Hapo utaratibu uko wapi Sasa?
Swala la utaratibu hapo ni kuacha kununua vitu vinavyohitajika kutunzwa kwenye jokofu nyumbani mpaka pale utakapounganishiwa umeme!

Kama unadhani kulipia ndio kufanya "utaratibu" na ndio "utamaduni wa taasisi zetu" basi endelea kununua samaki wabichi kwa kutegemea umeme uliokwisha lipia!
 
Siyo kuamini hivyo bali ni changamoto tunazokumbana nazo hasa kwenye Idara hiyo kwa kisingizio cha kulinda usalama wa mifugo na vyakula nchini mwetu.
Ndio maana nikakutaharidhisheni kuujua mkondo na speed ya maji kabla hamjaamua kuuvuka!

Kama unaona tahadhali yangu ni gere kwenu, jitiseni tu mtoni...muda utaongea. 200m nadhani si hasara ndogo!
 
Sheria ziko wazi jamani ,ukiangiza wanyama kutoka nje lazima uwe na import permit na inalipiwa ,kwahyo ukishaipata Kule unakovitoa watakupa export permit and the viceversa is true

Sasa unaagizaje vifanga bila kibali chochote? Nini kimekupa jeuri ya kufanya hivyo ? Hii vita ni kubwa na inahitaji watu wenye msimamo kama profesa nonga ( veterinary doctor huyu) maana hapo angeweza chukua rushwa hata ya millioni 30 au 50 lakin kasimama kwenye sheria ,huwa wanasema ni bora kufuata utaratibu ili uwe na ujasiri wa kusimama na kukemea . watu jamii ya kina profesa nonga ni muhimu sana kwenye hili taifa ni bora kufa maskini kwa kutenda haki

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Inasikitisha sana kwa vifaranga kufungiwa ndani kwa siku zote hizo hadi vikafa huku "wataalam" wakijua kuwa hawa ni viumbe hai tena dhaifu ambao umri wao ni chini ya siku 5. Sasa hapo sijui kama walikuwa wamejifungia ofisini kwao huku wamewasha AC wakiitisha makaratasi yaende ofisini ili waruhusu vifaranga vipate maji na chakula! Just papers zinacost uhai wa vifaranga na sh 200M na bado watu wapo pride na kilichofanyika kwa kivuli cha "fuata utaratibu" Hadi kifaranga kitoke Ulaya hadi hapa kwetu lazima kuna taratibu zimefuatwa. Akili ya kawaida inafikirisha hivyo. Lazima export permit imetolewa na makaratasi mengine. Kukosekana karatasi moja au mbili upande wetu ambayo si ajabu haikuwa na uhusiano na masuala ya afya ya vifaranga ni changamoto ambayo ingekuwa addressed na serious officer kwa udharura hadi kusaidia kutoa maamuzi kwa haraka kwa kujua ana deal na a day old chicks. Kwamba vifaranga vimefungiwa siku 7 wakati wanaendelea kufuatilia nyaraka ni ngumu kumeza. Walijua matokeo yake bila shaka! Mimi nina imani kuna tobo upande wa wahusika. Walistahili kumsaidia importer badala ya kumtelekeza. Hata kama utaratibu ungeonekana umekosewa basi maamuzi yangetoka ndani ya 12 hours ili hatima ya vifaranga ijulikane na si kuwaacha wafie kwenye mabox kisha tujuvune kwa hili.
Ufafanuzi mzuri sana huu kwamba lazima EXPORT PERMIT ziwepo na huo ndiyo ukweli pasipo na shaka yoyote.Tatizo ni watumishi wa baadhi ya idara za Serikali hasa hasa Wizara ya Kilimo kuwa TRADE BARRIERS badala ya kuwa TRADE FACILITATORS.
 
Sheria ziko wazi jamani ,ukiangiza wanyama kutoka nje lazima uwe na import permit na inalipiwa ,kwahyo ukishaipata Kule unakovitoa watakupa export permit and the viceversa is true

Sasa unaagizaje vifanga bila kibali chochote? Nini kimekupa jeuri ya kufanya hivyo ? Hii vita ni kubwa na inahitaji watu wenye msimamo kama profesa nonga ( veterinary doctor huyu) maana hapo angeweza chukua rushwa hata ya millioni 30 au 50 lakin kasimama kwenye sheria ,huwa wanasema ni bora kufuata utaratibu ili uwe na ujasiri wa kusimama na kukemea . watu jamii ya kina profesa nonga ni muhimu sana kwenye hili taifa ni bora kufa maskini kwa kutenda haki

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
Kwa akili yako vifaranga vinaweza toka Belgium tena kwa usafiri wa ndege bila Export Permit??
 
Back
Top Bottom