Profesa Nonga: Vifaranga 62,730 kutoka Ubelgiji vilivyokamatwa JNIA vyote vimefia Airport

Profesa Nonga: Vifaranga 62,730 kutoka Ubelgiji vilivyokamatwa JNIA vyote vimefia Airport

Una kiwango gani Cha elimu. Sasa hapo vifaranga vilitakiwa kuteketezwa. Shida tupu
Usiulize kiwango cha elimu, uliza kiwango cha uelewa. Wengi munavyo vyeti vya elimu lakini uelewa ni mdogo kama unavyoonesha hapa, OK!

Kama huoni lolote la kujifunza kwenye mfano huo, basi uko chini sana. Hukutakiwa kushiriki mjadala huu. Yaani unadhani ni biashara ya mkaa wa Mkuranga? Unaishia kulalamikia control mechanism!
 
Hivi wewe unaona huyo ni professor? Kama vifaranga vina maambuzi na magonjwa iweje aende bila tahadhari? Hana safety yeyote ya kumkinga asipate maambuzi ya ugonjwa kutoka kwenye vifaranga, kwahiyo anarudi nyumbani kueneza ugonjwa? , Professor kabisa kaenda vile kukagua vifaranga na atuambie Kuna maambuki? Hawa professor wa Tanzania ni vichekesho, kwani wana soma wapi?
Duh!

Huu ndio utafsiri wako wa mtu kuwa Profesa?

Mkuu, inanilazimu nikupe pole kwa mawazo ya namna hii.
 
Kwanza unajua hizo sheria ziliwekwa kwa ajili ya nini?.
Alafu Jiulize kama wewe unauwezo wakuingiza kifaranga hatakimoja bila utaratibu huko vilipotoka hivyo 60thousand.
Wewe kwa akili yako vifaranga vinaweza toka Ubelgiji kwa usafiri wa ndege bila Export Permit?
 
Kwani wakati mnamlaumu Magufuli kuwa kateketeza vifaranga kutoka Kenya, Magufuli ndiye aliyetoka ofisini kwake kwenda kuviteketeza?Samia tumlaumu kwa kutowachukulia hatua hao wasaidizi wake, Maana hili swala la vifaranga lilianza kijadiliwa mda kwanini hakuchukua hatua kuvinusuru wakati alikuwa na tarifa?au haujui mtu kapoteza mtaji wa million 200?
CCM NI ILE ILE BHANA
 
Magonjwa ya ndege yapi ambayo mpaka sasa yamethibitiswa kuwa vifaranga walikuwa nayo. Hii lazima itakwenda na wahusika wote waliochelewesha mpaka vifaranga wakapoteza maisha.
Mmeambiwa vifaranga vimeingia nchini kimakosa muhusika hakufuata utaratibu nyie mnajifanya kama hamnazo mnatetea uhalifu.

Kwahiyo kama ugonjwa haukudhibitishwa ndio Ulitaka viachwe viingie mitaani? Huko vilikotoka wewe unaweza kupeleka vifaranga katika mazingira kama hayo?.

Then wahusika siku wakiacha vikaingia kiholela watu wakafa kwa magonjwa nyienyie mtakuja na matusihapa kutukana wahusika kwamba wamekula rushwa na kuruhusu bidhaa hatarishi kuingia nchini kiholela.

Hivi unajua kwamba hata hukovilipotoka huwezi kuvirudisha bila kibali maalum?

Acha ushabiki kwenye mambo ya hatari mnatia aibu sana.
 
Wewe kwa akili yako vifaranga vinaweza toka Ubelgiji kwa usafiri wa ndege bila Export Permit?
Akili yangu imefanyaje, soma hapa chini.
[emoji116][emoji116]

Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo (DVS) katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Hezron Nonga alisema ombi la kibali cha kuagiza cha Desemba Mosi, 2022, halijafika ofisini kwake wala wizarani.

“Tuliona barua ya maombi ya vibali kutoka nje ya nchi, muda mfupi baada ya vifaranga kukamatwa JNIA. Kadhalika, cheti cha mifugo kilichoandikwa na Shirikisho la Ubelgiji la Usalama wa Mnyororo wa Chakula (FACFAS),” alisema Profesa Nonga.

Akitoa taarifa ya vifaranga hivyo, Profesa Nonga alisema vyote 62,730 vimekufa baada ya kutelekezwa kwenye uwanja wa ndege.

“Mwagizaji ana kesi nyingine ya kujibu mbele ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuwa mipango ya uteketezaji wa kuku inaendelea,” alisema.
 
Mmeambiwa vifaranga vimeingia nchini kimakosa muhusika hakufuata utaratibu nyie mnajifanya kama hamnazo mnatetea uhalifu.

Kwahiyo kama ugonjwa haukudhibitishwa ndio Ulitaka viachwe viingie mitaani? Huko vilikotoka wewe unaweza kupeleka vifaranga katika mazingira kama hayo?.

Then wahusika siku wakiacha vikaingia kiholela watu wakafa kwa magonjwa nyienyie mtakuja na matusihapa kutukana wahusika kwamba wamekula rushwa na kuruhusu bidhaa hatarishi kuingia nchini kiholela.

Hivi unajua kwamba hata hukovilipotoka huwezi kuvirudisha bila kibali maalum?

Acha ushabiki kwenye mambo ya hatari mnatia aibu sana.
Mbona mkali sana. Na wewe ni mmojawapo nini. Mmeua vifaranga lazima muwajibike
 
Ajabu sana, wamekamata vifaranga wakadhani wamekamata mawe, wakayaacha huko Airport wao wakaendelea kula sikukuu zao za mwisho wa mwaka, kuna watendaji wa serikali wazembe sana.

Mnabwabwaja sana humu ila ruhusuni akili zenu zifanye kazi walau kidogo.

Vifaranga havijakamatwa ila vilizuiwa kuingia nchini kwa sababu nyaraka za uingizaji hazikukamilika kwa mujibu wa Sheria za masuala ya uingizaji mifugo nchini.

Umuhimu wa jambo hili ni kulinda afya za wanyama waliopo nchini na kulinda afya za watu dhidi ya magongwa yanayoweza kuletwa na wanyama kutoka nje ya nchi.

Tangu kuzuiwa vifaranga hao wahusika waliarifiwa wachukue hatua ikiwemo kuwarudisha vifaranga hao, kama hawakuchukua hatua mlitaka Wizara ifanyeje? Ichukue risk ya kuingiza vifaranga nchini kinyume cha Sheria alaf kesho mje hapa kusema ile Wizara imejaa rushwa??

Kwanza jiulizeni kama tuna wazalishaji wa ndani wanakosa pa kuuza kwanini watu wanaenda kuagiza nje? Wana agenda gani?

Watanzania tumekuwa na desturi ya kulaumu na kulalamika hata kwa tusiyoyajua kama yapo Kisheria na nchi zingine ni hivyo hivyo ila kwakuwa nchi zingine hawana utani katika kusimamia Sheria ndo maana hatusikii mtu kapeleka vifaranga Uchina n.k

Tena nchi za Ulaya wapo strict sana ila sisi ndo mnatamani tuwe shamba la bibi na mali ya wapiga dili bila kujali afya za watu.
 
Mbona mkali sana. Na wewe ni mmojawapo nini. Mmeua vifaranga lazima muwajibike

Atakaye wajibika ni muagizaji sio aliyezuia.

Kwanza kuagiza bila kibali ni kosa tayari kwahiyo kama amekutuma kamwambie ameyakanyaga this time[emoji23]
 
Wewe kwa akili yako vifaranga vinaweza toka Ubelgiji kwa usafiri wa ndege bila Export Permit?

Bado huelewei kitu kwenye hizi taratibu.

Export permit ni kibali cha kule vilipotoka lakini kuingiza nchini kwetu lazima kuwe na import permit na cheti cha Afya.

Jaribu kutafakari vema haya mambo weka interest pembeni kwanza
 
Hivi huyu serikali ni nani na anaishi wapi....maana amekuwa chanzo cha matatizo mengi....na kwanini wananchi wenye nchi yao hawamuwajibishi au kumnyang'anya madaraka yake!?

Watu wengi humu ni weupe sana kichwani nawewe ni mmoja wapo hamjui taratibu wala Sheria za Nchi mnapuyanga tu
 
Tatizo ofisi za umma zimejaa rushwa. Watoaji vibali kama waliombwa, waulizwe kwa nini hawakutoa?

Kama hawakutoa kwa uzembe na kusubiria rushwa, wafukuzwe kazi, na mafao yao yatumike kumfidia mkulima.
Anae toa kibali ni DVS Mwenyewe ambae ndio alivizuia vifaranga hapo Airport. Kwa madai yake ni kwamba maombi ya vibali hayakumfikia.

By the way. Kuna kasumba ka watu kutojisumbua kuujua na kuufuata utaratibu. Na kuna kasumba ka watu kutoshirikisha ubongo katika kutatua changamoto ndo yanatufikisha hapa.

Wakati nasoma chuo kuna rafki yangu mchaga alikua ananambia nchi hii ina. mifumo miwili mfumo wa sheria na mfumo wa busara. Yaani kun wakati wafanya maamuzi wanatumia sheria na kunawakati sheria wanaweka pembeni wanatumia busara. Na ndivyo vinavyo tufikisha hapa

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
Kuna shida pande zote mbili

1.Mwagiza Vifaranga
2.Watoa vibali

Haiwezekani tu vifaranga vizuiwe kama taratibu zote zilifanyika,kuna shida tu mahali si Rahisi hili jambo.

Hasara hiyo ni kubwa nina uhakika kama vibali vingekua vimenyooka ni simu tu zingepgwa hata kama mtu hayupo go agead ingetolewa Vifaranga vingepita.

ila katika hili lazima kuna shida pande zote mbili .
Watu wanatumia hisia sana kulijadili hili swala. Ila swala la kuingiza mnyama hai nchi yeyote hua ni critical sana, ukikosea kidogo unaweza pata hasara kubwa sana.

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
Nina Masters Degree na nimewahi kuwa CEO wa Taasisi kubwa ya Serikali inayohusiana na importation, kwa sasa ni retired officer.

Njoo tatatibu usilete matusi
Alifikri anajibizana na ndezi mwenzake! Umemjibu kwa upole kweli!
 
Kwan wangeviweka quarantine kwenye shamba la muagizaji na kumchapa fine zingine zingine ingekuwaje?
Kwani huyo mwekezaji kama angepata kibali kabla ya kuwaingiza hapa nchini angepata hasara gani? Yaani uipe serikali kazi 2 kwa wakati mmoja? Hii siyo sawa! Hicho alichokutana nacho ndiyo njia sahihi ili liwe fundisho na kwa mesheni town wengine!
 
Hao viumbe... Roho zao zitawaandama
Hujui kitu, wanyama wana moyo hawana roho. Kama wliingizwa kinyemela hiyo ndio dawa pekee. Lazima nchi iendeshwe kwa taratibu siyo kama CHADEMA mtu anaamka na mbege kichwani anatangaza kubadili gia angani.
 
Mnabwabwaja sana humu ila ruhusuni akili zenu zifanye kazi walau kidogo.

Vifaranga havijakamatwa ila vilizuiwa kuingia nchini kwa sababu nyaraka za uingizaji hazikukamilika kwa mujibu wa Sheria za masuala ya uingizaji mifugo nchini.

Umuhimu wa jambo hili ni kulinda afya za wanyama waliopo nchini na kulinda afya za watu dhidi ya magongwa yanayoweza kuletwa na wanyama kutoka nje ya nchi.

Tangu kuzuiwa vifaranga hao wahusika waliarifiwa wachukue hatua ikiwemo kuwarudisha vifaranga hao, kama hawakuchukua hatua mlitaka Wizara ifanyeje? Ichukue risk ya kuingiza vifaranga nchini kinyume cha Sheria alaf kesho mje hapa kusema ile Wizara imejaa rushwa??

Kwanza jiulizeni kama tuna wazalishaji wa ndani wanakosa pa kuuza kwanini watu wanaenda kuagiza nje? Wana agenda gani?

Watanzania tumekuwa na desturi ya kulaumu na kulalamika hata kwa tusiyoyajua kama yapo Kisheria na nchi zingine ni hivyo hivyo ila kwakuwa nchi zingine hawana utani katika kusimamia Sheria ndo maana hatusikii mtu kapeleka vifaranga Uchina n.k

Tena nchi za Ulaya wapo strict sana ila sisi ndo mnatamani tuwe shamba la bibi na mali ya wapiga dili bila kujali afya za watu.
Mbona unatetea sana. Unaogopa nini. Mmefanya makosa Kwa kuwatesa viumbe wasio na hatia mpaka kupelekea vifo. Mnatakiwa muwajibike. Unajua viumbe hai vina uhuru wa kutokuwa na njaa au kiu. Sheria ya ustawi wa wanyama Tanzania inasema hivyo na nyie ndiyo wizara husika. Iweje mvunje Sheria mliyoianzisha wenyewe. Kuna mfugaji Moshi alichoma vifaranga, wizara ya mifugo ikasema itamchukulia hatua Kwa kukiuka Sheria ya ustawi wa wanyama, Haya Sasa na nyie jichukulie hatua Kwa kukiuka Sheria ya ustawi wa wanyama Tanzania.
 
Back
Top Bottom