Profesa Nyagori ashauri Taasisi za Afya kumpa tuzo Rais Magufuli kwa mapambano ya Corona

Rubbish professor! Anatafuta kuchaguliwa/ kuteuliwa. Eti professor, ndio maana Lissu anawadharau! Tuzo apewe kwa kufnya nini? Serendipity has saved the day , wa Brazil ali-apply serendipity unajua wanakufa wangapi a day?
Haya Mambo tumeachie Mungu tu....hata hatujui kilitokea Nini....pengine Ni Bahati labda mfano wa Brazil Ni mzuri Sana!
 
Una dalili zote za uchawi, ujinga uliotamalaki na upeo usiovuka urefu wa pua yako. Una macho lakini huoni, una masiko lakini husikii. Uchadema unakupukutisha akili zako.
Mbona povu mkuu ..sema wewe alifanya Nini zaidi ya kujilock down Chato kwa miezi 2
 
Jirani yangu ni praise and worship Magufuli team lakini wiki iliyopita amefiwa na mjomba wake kwa corona. Sasa hivi anakubali kuwa corona ni tatizo na Tanzania bado lipo.
 
Pref anatafta hata ubarozi uyo. Nasikia slaa anarudoshwa muda si mref
Lini watanzania wajinga wa aina yako watakwisha.? Kila kisemwacho kizuri na mtu yeyote kuhusu serikali, kila mtu anayepongeza jambo lolote jema linalofanywa na serikali mnatafsiri kuwa anatafuta uteuzi..! Ni ujinga kuwa na fikra hizo.
 
Hawa waliugua c 19 wako wapi?

1. Muslimu - police
2. Jerry muro - DC meru
3. Waitara - mbunge
4. Wengine bado wanapigania uhai.
 
Hawa waliugua c 19 wako wapi?

1. Muslimu - police
2. Jerry muro - DC meru
3. Waitara - mbunge
4. Wengine bado wanapigania uhai.
 
Hawa waliugua c 19 wako wapi?

1. Muslimu - police
2. Jerry muro - DC meru
3. Waitara - mbunge
4. Wengine bado wanapigania uhai.
 
Hawa waliugua c 19 wako wapi?

1. Muslimu - police
2. Jerry muro - DC meru
3. Waitara - mbunge
4. Wengine bado wanapigania uhai.
 
Anatafuta uteuzi huyo. Halafu badala ya kumshukuru Mungu wao wanamtukuza Binadamu mwenzao.
Kalenga mlemle kachoka kuchezea chaki.Soon atakumbukwa, ukinisujudia na kuanguka miguuni pangu nitakupa miliki zote za dunia kwa maana vyoote vilivyomo ni Mali yangu nampa nimtakae.
Profu mzima unajipendekeza ili upate teuzi tumbo lishibe hii brain gani hii.
 
Korona kilichosaidia ni mazingira ya joto Kali la afrika ndo limeupusha thus vifo si vingi sana
 
kamanda mzuri vitani hujukikana kwenye Vita chadema walk hi lock down wao bila kushirikisha wanachama wao wakatelekeza wanachama wao wajijue wenyewe kama watakufa kwa Corona shauri yao mwenyekiti mbowe na viongozi wenzie wabunge wakatelekeza Vita.

Raisi Magufuli akawa msitari wa mbele vitani akiongoza mapambano akasema ingieni kusali tufunge tuombe Mungu siku tatu na tujifukize. Mungu akasikia na kujifukiza kukatusaidia Vita ya Corona tumeshinda chini ya jemadari kiongozi anayejali watu wasife kwa corona .Apewe nishani na awamu ya pili
But yeye aliendeleza mapambano akiwa lock down Chato!
 
PROFESA NYAGORI ASHAURI TAASISI ZA AFYA KUMPA TUZO JPM MAPAMBANO YA CORONA

NA MWANDISHI WETU-MOROGORO

Daktari Mshauri Mwandamizi wa Magonjwa ya Ndani na Moyo, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), ambaye pia ni Mhadhiri wa vyuo vikuu mbali mbali vya tiba, Profesa Harun Nyagori, ameshauri taasisi za vyuo vikuu vya Afya nchini Tanzania, pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO), kumpatia tuzo maalumu ya heshima, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kwa ajili ya kutambua mchango wake katika kupambana na janga la Corona.

Akizungumza na waandishi wa Habari mjini Morogoro jana, Profesa Nyagori ambaye amewahi kutunukiwa tuzo mbalimbali za kimataifa zilizotambua mchango wake katika tafiti za maradhi ya moyo barani afrika, alisema kuwa kuna haja ya kutambua mchango mkubwa uliotukuka alioutoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, kwa mbinu za kipekee alizozitumia kupambana na janga la mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na Virus vya Corona.

“ Nikiwa kama mtaalamu niliyebobea katika masuala ya tiba ya maradhi ya binadamu, ninampongeza sana Rais Dkt John Magufuli, kwa namna alivyoweza kutoa mchango wake mkubwa kwa Watanzania na Ulimwengu kwa ujumla katika kupambana na janga la mlipuko wa ugonjwa wa Corona na ninatoa wito kwa taasisi za vyuo vikuu vya Afya hapa nchini na Shirika la Afya la Duniani (WHO) kumpatia tuzo maalumu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli kwa kutambua mchango wake.”

Profesa Nyagori aliongeza kusema kuwa ugonjwa wa Corona ulipoingia kwa mara ya kwanza hapa nchini, wananchi wengi walijawa na hofu kubwa juu ya athari za ugonjwa huo na hivyo walihitaji sana kumpata mtu wa kuwatoa hofu hiyo.

“ Msongo wa mawazo (stress) unasababisha uwezo wa kinga mwilini kushindwa kupigana na maradhi na hivyo kinga za mwili kupungua ambapo kichocheo cha corticosteroid kinachozalishwa kwenye mwili kinaweza kuwa kisababishi kikubwa cha kupunguza kinga za mwili. Hofu huchukua nafasi kubwa sana katika kumfanya mtu kupata athari kubwa za ugonjwa fulani. Kisayansi hofu husababisha kinga za mwili wa biniadamu kushuka na hivyo kumfanya kuwa rahisi kuambukizwa na kushambuliwa na maradhi sambamba na kupata athari kubwa zaidi. Rais Dkt John Magufuli amefanya kazi kubwa kuwajengea ujasiri Watanzania kutokuwa na hofu kubwa juu ya ugonjwa huu wa Corona, huku wakichukua taadhari za kiafya ambazo wataalam wa Afya wanazitoa. Hatua hii imeepusha kwa kiwango kikubwa, athari ambazo zingetokana na ugonjwa huu.” Alisema Profesa Nyagori.

Profesa Nyagori aliongeza kusema kuwa majirani zetu na nchi nyingine nyingi ulimwenguni zimejikuta katika sintofahamu kubwa kutokana na janga la Corona kwa sababu hazikuwa na viongozi mathubuti, wenye msimamo, mbinu na ubunifu wa namna sahihi ya kupambana na janga hili kwa njia ya kisaikolojia kama ambavyo Rais Magufuli amekuwa nao.

KUHUSU KARANTINI
Akizungumzia kuhusu mbinu ya kujifungia ndani (karantini) kama njia ya kuepuka na kuepusha kusambaa kwa maambuki ya virusi vya Covid-19, Profesa Nyagori alisema kuwa mbinu hiyo endapo kama ingetumika, ingelikuwa na madhara makubwa kuliko faida.

“ Hatua ya Rais Magufuli kutokubaliana na mbinu ya kujifungia ndani (Lockdown), imesaidia sana katika kuwafanya watanzania kuendelea kutafuta fedha ambazo zimewawesha kumudu kupata milo yenye lishe ambayo kimsingi imeimarisha kinga zao na kufanya isiwe rahisi kushambuliwa na maradhi Corona.

“Kujifungia ndani licha ya kisaikolojia kuongeza wasiwasi, lakini pia humfanya mtu kutopata fursa ya kutafuta pesa na hivyo kutomudu kupata mahitaji muhimu ikiwemo vyakula mchanganyiko ambavyo ni muhimu kwa lishe inayoimarisha kinga mfano vitamin na madini mbalimbali.” Alisema Profesa Harun Nyagori.
Huyu profesa haikosi kuokotwa dampo aisée.
 
Infixi: Soma hapa: Yule daktari aliyehatarisha maisha ya wananchi wa Mbeya kwa kujiita Dr. bingwa wa magonjwa ya moyo, ambaye aliondolewa kwa nguvu ya kalamu ya mwandishi, sasa ameibukia Morogoro.

Dr. huyo anayefahamika kwa jina la Nyagori, ambaye hajawahi kusomee degree yoyote ya udaktari, ameibuliwa kwa mara nyingine na kalamu ya Raia Mwema. Hivi ndivyo Raia Mwema ilivyoripoti kwa ufupi:

DAKTARI bingwa mshauri wa magonjwa ya moyo (consultant cardiologist), Harun Elmada Nyagori wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, anadaiwa kupachikwa udaktari huo bingwa bila kuwa na sifa zinazostahili, vyanzo kadhaa vya habari vimefichua taarifa hizo.

Vyanzo hivyo vya habari vinadai ya kwamba, hata taarifa zilizopo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro zinathibitisha utata katika wasifu wa kitaaluma wa mtaalamu huyo.

Inadaiwa kwamba kumebainika utata wa taarifa za wasifu wake (CV), kwa mfano, tarehe yake ya kuzaliwa, elimu yake ya sekondari hadi taaluma yake.

Wakati taarifa zake za kiofisi zikidaiwa kuonesha kuwa alisoma elimu ya sekondari kuanzia mwaka 1993 na kuhitimu mwaka 1998, cheti chake cha kidato cha nne kinaonesha kuwa alihitimu elimu ya sekondari mwaka 1996 akiwa amepewa cheti cha daraja la nne (division IV) baada ya kufaulu masomo manne alama D, moja alama C na manne yaliyosalia akipata F.

Taarifa zake hazioneshi amepitia mafunzo yoyote ya afya hapa nchini bali zinaonesha amefanya masomo yake ya awali ya utabibu (preparatory foundation course in medicine) kati ya mwaka 1998 na 1999, huko Ukraine katika Chuo Kikuu cha Lugansk State Medical.
 
Huyu Nyangori si ndiye aligundulika kuwa ni Dr feki kule Mbeya na Mororo? Maajabu ameibukia Tasisi ya JK.
Harun nyagori.Msabato aliyesahau kumtukuza MUNGU kutuepusha na balaa la corona anatukuza mtu. MUNGU UTUREHEMU SISI WAKOSAJI. TUSAMEHEE BURE MUNGU WETU.
 
PROFESA NYAGORI ASHAURI TAASISI ZA AFYA KUMPA TUZO JPM MAPAMBANO YA CORONA

NA MWANDISHI WETU-MOROGORO

Daktari Mshauri Mwandamizi wa Magonjwa ya Ndani na Moyo, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), ambaye pia ni Mhadhiri wa vyuo vikuu mbali mbali vya tiba, Profesa Harun Nyagori, ameshauri taasisi za vyuo vikuu vya Afya nchini Tanzania, pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO), kumpatia tuzo maalumu ya heshima, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kwa ajili ya kutambua mchango wake katika kupambana na janga la Corona.

Akizungumza na waandishi wa Habari mjini Morogoro jana, Profesa Nyagori ambaye amewahi kutunukiwa tuzo mbalimbali za kimataifa zilizotambua mchango wake katika tafiti za maradhi ya moyo barani afrika, alisema kuwa kuna haja ya kutambua mchango mkubwa uliotukuka alioutoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, kwa mbinu za kipekee alizozitumia kupambana na janga la mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na Virus vya Corona.

“ Nikiwa kama mtaalamu niliyebobea katika masuala ya tiba ya maradhi ya binadamu, ninampongeza sana Rais Dkt John Magufuli, kwa namna alivyoweza kutoa mchango wake mkubwa kwa Watanzania na Ulimwengu kwa ujumla katika kupambana na janga la mlipuko wa ugonjwa wa Corona na ninatoa wito kwa taasisi za vyuo vikuu vya Afya hapa nchini na Shirika la Afya la Duniani (WHO) kumpatia tuzo maalumu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli kwa kutambua mchango wake.”

Profesa Nyagori aliongeza kusema kuwa ugonjwa wa Corona ulipoingia kwa mara ya kwanza hapa nchini, wananchi wengi walijawa na hofu kubwa juu ya athari za ugonjwa huo na hivyo walihitaji sana kumpata mtu wa kuwatoa hofu hiyo.

“ Msongo wa mawazo (stress) unasababisha uwezo wa kinga mwilini kushindwa kupigana na maradhi na hivyo kinga za mwili kupungua ambapo kichocheo cha corticosteroid kinachozalishwa kwenye mwili kinaweza kuwa kisababishi kikubwa cha kupunguza kinga za mwili. Hofu huchukua nafasi kubwa sana katika kumfanya mtu kupata athari kubwa za ugonjwa fulani. Kisayansi hofu husababisha kinga za mwili wa biniadamu kushuka na hivyo kumfanya kuwa rahisi kuambukizwa na kushambuliwa na maradhi sambamba na kupata athari kubwa zaidi. Rais Dkt John Magufuli amefanya kazi kubwa kuwajengea ujasiri Watanzania kutokuwa na hofu kubwa juu ya ugonjwa huu wa Corona, huku wakichukua taadhari za kiafya ambazo wataalam wa Afya wanazitoa. Hatua hii imeepusha kwa kiwango kikubwa, athari ambazo zingetokana na ugonjwa huu.” Alisema Profesa Nyagori.

Profesa Nyagori aliongeza kusema kuwa majirani zetu na nchi nyingine nyingi ulimwenguni zimejikuta katika sintofahamu kubwa kutokana na janga la Corona kwa sababu hazikuwa na viongozi mathubuti, wenye msimamo, mbinu na ubunifu wa namna sahihi ya kupambana na janga hili kwa njia ya kisaikolojia kama ambavyo Rais Magufuli amekuwa nao.

KUHUSU KARANTINI
Akizungumzia kuhusu mbinu ya kujifungia ndani (karantini) kama njia ya kuepuka na kuepusha kusambaa kwa maambuki ya virusi vya Covid-19, Profesa Nyagori alisema kuwa mbinu hiyo endapo kama ingetumika, ingelikuwa na madhara makubwa kuliko faida.

“ Hatua ya Rais Magufuli kutokubaliana na mbinu ya kujifungia ndani (Lockdown), imesaidia sana katika kuwafanya watanzania kuendelea kutafuta fedha ambazo zimewawesha kumudu kupata milo yenye lishe ambayo kimsingi imeimarisha kinga zao na kufanya isiwe rahisi kushambuliwa na maradhi Corona.

“Kujifungia ndani licha ya kisaikolojia kuongeza wasiwasi, lakini pia humfanya mtu kutopata fursa ya kutafuta pesa na hivyo kutomudu kupata mahitaji muhimu ikiwemo vyakula mchanganyiko ambavyo ni muhimu kwa lishe inayoimarisha kinga mfano vitamin na madini mbalimbali.” Alisema Profesa Harun Nyagori.

Huyu ni MATAGA aligombea ubunge 2015 kupitia chama cha mboga mboga akashindwa kwenye kura za maoni. Hapa anamsifia Jiwe ili ampitishe mwaka huu maana hakuna kura za maoni inategemea Jiwe ameamkaje siku hiyo.
 
Back
Top Bottom