GE2025 Profesa Shivji: Mateso hasa yale yanoyotendwa na vyombo vya dola ni udhalilishaji wa hali ya juu wa utu wa binadamu

GE2025 Profesa Shivji: Mateso hasa yale yanoyotendwa na vyombo vya dola ni udhalilishaji wa hali ya juu wa utu wa binadamu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Juu ya Mateso

Mateso hasa yale yanoyotendwa na vyombo vya mabavu vya dola ni udhalilishaji wa hali ya juu wa utu wa binadamu. Hayasahauliki, hayasameheki wala hayakubaliki. Ni udhalilishwaji wa utu mara mbili. Moja ya yule aliyeteswa - utu wake unakanyagwa, unasagwasagwa na kutupiliwa mbali. Pili ni utu wa mtesaji mwenweye. Anajisusha utu wake - anajifanya sio binadamu. Anajigeuza jitu, sio mtu tena. Nafsi yake haiwezi ikawa na amani. Hawezi akawa na raha. Nafsi yake itamsota hata kama yeye mwenyewe hayajui. Mbele ya binadamu wenzake atajihisi, hata kama hakiri, yeye sio yeyote wala lolote. Anatembea akiwa amenaamisha kichwa chake kwa aibu.

Utu ni msingi na kiini cha haki zote za binadamu na awali ya yote ni utii wa mgongo wa dhana ya usawa wa binadamu. Kiongozi yeyote anayevumulia mateso ya raia wake sio muumini wa usawa wa binadamu, hata kama akihubiri na kuuimba kiasi gani.

Mnamo mwaka wa 1976 lilitokea jambo nchini mwetu liliotuachia doa nene katika historia yetu. Kulikuwa na muaji, yaliyosambaa kwa kasi kubwa, ya biwazee maeneo ya Shinyanga na Mwanza kwa imani ya ushirikina kuwa walikuwa wachawi. Viongozi wa ngazi za juu wa usalama na siasa walikaa pamoja na kuamua kwamba jambo hilo lazima likomeshwe. Wasalama wakapanga mkakati ulioitwa operesheni mauaji na la haula likageuka kuwa “mradi” wa mateso na mauaji na udhalilishwaji wa hali ya juu ambayo nchi ilikuwa haijawahi kuona.

Mwalimu hakujua kichokuwa kinaendelea mpaka mabibi walioteswa wakafunga safari kwenda kumuona kwake Butiama alikofikia kwa mapumziko ya Chrismasi. Mbele ya Mwalimu wakavua nguzo zao kumuonyesha majeraha walioyoipata sehemu zao za siri. Mwalimu alishindwa kuyaangalia - akafunga macho yake kwa mikono yake yote miwili. Aliwaita mara moja mawaziri wahusika. Waziri wa Ndani wakati ule, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Waziri wa Usalama Bwana Peter Siyowelwa walishinikizwa na Mwalimu kujiuzulu. Wakuu wa usalama walishtakiwa mahakamani.

Ni kweli kwamba tumekuwa na matukio ya mateso katika awamu zote lakini popote pale yalipogundulika hatua ya aina moja au nyingine ilichukuliwa. Hivi karibuni kumekuwa na matukio kama haya lakini bahati mbaya hayaja karipiwa au kulaaniwa hadharani. Mara nyingine tumesikia wakuu wachache hata wakitoa matamshi ambayo yanaweza yakashawishi maafisa chini yao kutenda mambo kama haya dhidhi ya watuhumiwa au wapinzani. Hii sio sawa hata kidogo. Katika jamii na Taifa kama letu ambalo waasisi wetu walijenga juu ya misingi ya usawa na utu wa binadamu, hatunabudi sisi sote, umma pamoja na viongozi wa siasa, wakuu wa vyombo vya usalama na sheria na hata viongozi wa dini kulaani na kutokuvumilia matukio ya utesaji wa raia yeyote. Matukio ya utesaji sio ya kawaida, yasizoeleke, yasipuuzwe wala yasihalalishwe.

Katiba zetu sote mbili ya Muungano na ya Zanzibar zina vifungu vinavyo piga marufuku tendo la utesaji ama kwa tafsiri au moja kwa moja. Juu ya hili Katiba ya Zanzibar imeweka wazi bila yakumuinya maneno. Ibara ya 13(3) inasema:

(3) Ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza su kudhalulishwa.

Ibara Hii iliwekwa katika marekebisho ya 2002 (Sheria Nam 2/2002) ya Katiba ya Zanzibar kutokana na mapendekezo ya jopo la wataalam kutoka nchi za madola na Watanzania akiwemo mwandishi wa makala hii.

Ni zoea ya muda mrefu wa kimahakama, kwa mfano, kukataa katakata kupokea ushahidi wowote uliyopatikana kwa kutumia mabavu na mateso. Ni matumaini yangu kwamba desturi hii nzuri yataendelea mahakamani zetu na majaji wetu watakuwa na ujasiri wa kutosha kutupilia mbali ushahidi wowote uliyopatikana kwa njia ya kutumia mabavu na mateso. Vile vile polisi na ofisi ya Mkurungezi wa Mashtaka (DPP) wanatakiwa kuwa makini. Wakinusa tu dalili za utumiaji wa mateso wafanye uchunguzi mara moja badala ya kusubiri taarifa kutoka kwa mlalamikaji.

Issa Shivji (Prof)
Iliandikwa tarehe
12/05/2019

Utekaji pia ni utesaji. ukizoeleka tutakuwa tumezama katika udongo wa siasa chafu ambayo haina ukomo.
25/10/2025
 
Nimedhani kaiandika juzi/jana au leo!
Maana jimama angemtumia kina Mafwele.
 
Na ndiyo maana kuna watu huwa wanafurahia pale wanaposikia kumetokea kifo/vifo vya baadhi ya watu wenye mamlaka.
 
Back
Top Bottom