Profesa Shivji: Wasomi wanaogopa kukosoa Serikali ili wapate teuzi. Hawana msaada tena kwa jamii ya Watanzania

Profesa Shivji: Wasomi wanaogopa kukosoa Serikali ili wapate teuzi. Hawana msaada tena kwa jamii ya Watanzania

Lkn sisi Waafrika bhana, hata mwenye uchungu na nchi na Wananchi na anayejaribu kuwatetea bado ni Muhindi pia, wasomi weusi wote wizi tu, wanaibia na kuharibu hata nchi waliozaliwa!
 
Wasomi wapo kwa ajili ya matumbo yao tu. Hawana msaada wa kitaaluma kwa taifa letu tena. Hawakosoi kwa manufaa ya umma
--
Mwanazuoni mkongwe nchini, Profesa Issa Shivji amesema sehemu kubwa ya wasomi nchini wameshindwa kulisaidia Taifa kwa kutoa ushauri unaofaa huku wakisubiri kuteuliwa kwenye nyadhifa mbalimbali.

Profesa Shivji, gwiji la sheria kitaifa na kimataifa alitoa kauli hiyo juzi, katika mahojiano ya kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na ITV ambapo pia alizungumzia miaka 100 ya kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Nyerere.

“Mimi ni msomi, nakiri sitaki kusema nipo tofauti na wengine, zamani wasomi walikuwa wanakosoa na kushauri, tuliandika, tulikuwa na midahalo, tunazungumza, lakini sasa hivi hatusikii. Kulikuwa na wakati wasomi walikuwa wanajipanga katika foleni ya kusubiri kuteuliwa, sasa kama una matumaini ya kuteuliwa hutakosoa wala kuzungumza mambo.

“Ingawa kulikuwa na hofu pia na hilo linaeleweka pia, lakini kwa kiasi gani wasomi tumetekeleza jukumu letu. Hivi sasa wamepumua kidogo na wanaweza kuanza upya kutekeleza majukumu yao,” alisema Profesa Shivji.

Profesa Shivji alisema kunahitajika kazi ya ziada kukosoa wazo tawala na kutoa mbadala wake ili kuleta mabadiliko katika jamii ambapo alisema kazi mojawapo ya wasomi au wanazuoni ni kukosoa na kutoa wazo mbadala.

“Hatua hii itasaidia wananchi kuona kwamba kuna njia nyingine za kufanya mambo, kuelewa ukweli na kuangalia hali halisi, sio tunayoambiwa siku zote. Lazima nikiri ni jukumu letu, lakini wasomi tumefeli sana katika jukumu hili hasa katika miongo miwili iliyopita.

“Wananchi wakitulaumu tunastahili kulaumiwa kwa kweli, lakini lazima tujikumbushe haikuwa hivyo Tanzania. Wasomi au wanazuoni wa nje hadi leo wanakumbuka wasomi wa Tanzania, walichoandika, walichojadili na walichopendekeza hadi leo wanatukumbuka,” alisema.

Profesa Shivji alisema bado wasomi wa nje wanashangaa na kuhoji nini kilichotokea kwa wasomi wa Tanzania.

Hata hivyo, msomi huyo alisema wananchi wana uwezo wa kukosoa wazo tawala, akisema mara nyingine ukizungumza nao unajifunza masuala mengi kutoka kwao, ingawa wanavyozungumza sio kama wasomi.

Kwa mujibu wa Profesa Shivji, wasomi walikuwa wanafanya hivyo miaka ya 70 hadi 80 wasomi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam na pale ilipohitaji walikuwa wanaikosoa Serikali.

“Baadhi ya wasomi wetu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, hatukukubaliana moja kwa moja na Mwalimu (Nyerere) kuhusu sera za kilimo. Hata wakati wa Nyerere hatukuweza kuleta mapinduzi ya kilimo, tulifuata nyayo za kikoloni,” alisema.

Kauli ya Profesa Shivji imeungwa mkono na Mwenyekiti Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udasa), Dk Aviti Mushi aliyesema miaka kadhaa wasomi walikuwa na hofu ya kukosoa masuala mbalimbali.

“Wale waliojitokeza kukosoa waliitwa majina mabaya mara sio wazalendo au vibaraka, hali hii ilisababisha wasomi kutotoa maoni, huku wengine wakifunga mdomo na kutafuta ugali wao. Walioonekana kimya ndio walikuwa bora na kupata nafasi za uteuzi katika maeneo mbalimbali,” alisema Dk Mushi alipozungumza na Mwananchi kwa simu jana.

Aliendelea kusema kuwa, kauli ya Profesa Shivji ina uhalisia kutokana na hali iliyopo na kwamba ilifika wakati wasomi walikuwa wana hofu kuzungumza na vyombo vya habari ili kutoa maoni yao wakihofia kuitwa majina mabaya. “Wasomi tulijikuta hatuwezi kuzungumza na vyombo vya habari, hasa kutoa maoni yanayokinzana na Serikali. Ingawa sasa hivi kuna mabadiliko yametokea,” alisema.

Chanzo: ITV

Kuwa mwepesi wa kukimbilia kukosoa nako ni udhaifu. Mtu mwenye ueledi na uhodari huwa anashauri na kutoa mapendekezo.
 
Lkn sisi Waafrika bhana, hata mwenye uchungu na nchi na Wananchi na anayejaribu kuwatetea bado ni Muhindi pia, wasomi weusi wote wizi tu, wanaibia na kuharibu hata nchi waliozaliwa!
Sio Muhindi Prof Issa Shivji, ni Mtanzania kama mimi na wewe.

Utanzania sio Ubantu pekee.
 
Sio Muhindi Prof Issa Shivji ni Mtanzania kama mimi na wewe.

Najua lkn ana asili ya India, yani wazazi wake wote wawili walitokea Asia, hata ukimuangalia siyo Muafrika kwa muonekano atleast!
 
Najua lkn ana asili ya India, yani wazazi wake wote wawili walitokea Asia!
Hayati Karume alikuwa na Asili ya Nyasaland leo Malawi ina maana Bi Fatma Karume akijenga Hoja utasema Mmalawi anaupiga mwingi?

Samia Suluhu ana asili ya Mboka Kindu Maniema huko Kongo ya Mashariki

Akituhutubia kwa Kiswahili chake fasaha utasema kuna Mkongo anatuhutubia?

Acha ubaguzi ndugu.
 
Hayati Karume alikuwa na Asili ya Nyasaland leo Malawi ina maana Bi Fatma Karume akijenga Hoja utasema Mmalawi anaupiga mwingi?

Usinielewe vibaya, sijampinga Shivji, ila kuna ukweli ambao huwezi kuukwepa kwamba Shivji ana asili ya Asia, hata kwa muonekano tu, Malawi ni Afrika bado hivyo sidhani kama
inafanana!
 
Usinielewe vibaya, sijampinga Shivji, ila kuna ukweli ambao huwezi kuukwepa kwamba Shivji ana asili ya Asia, hata kwa muonekano tu, Malawi ni Afrika bado hivyo sidhani kama
inafanana!
Wote wewe mimi na Shivji tumezaliwa na Mama mmoja.
 
Sema huyu Mzee Ukomunisti wake ndio huwa unaboa.
 
Professor Shivji ameongea ukweli mtupu,
Shida ni kwamba hela za kule bungeni ni tamu sana, taamu mno!
 
Wasomi wapo kwa ajili ya matumbo yao tu. Hawana msaada wa kitaaluma kwa taifa letu tena. Hawakosoi kwa manufaa ya umma
Ni msomi yupi Tanzania anayepoteza muda wake maabara au Maktaba akihangaika na utayarishaji wa machapisho ya utafiti alioufanya.

Kaangalie, kote kwenye vyuo vyetu na taasisi maalum zenye wajibu wa kutafiti maswala mbalimbali yanayoweza kufumbua matatizo ya wakulima wetu, au huduma zetu za kiafya, ama usindikaji wa viwandani, ni machapisho mangapi yanayofanyika toka huko kwa mwaka nyakati hizi!

Lakini ukitafuta wataalam hawa wanavyohangaika na mikutano ya kisiasa ya CCM, huwezi kukosa kujua ni wapi panapowekewa uzito zaidi.
Lakini isingekuwa neno, kama uwepo wao huko kwenye hicho chama kungesaidiwa na utaalam wa watu hawa, ili kupitia huko nchi inufaike. Lakini wapi, wanapoingia huko inakuwa kama wamenyofolewa bongo zao kichwani.

Lakini tusiwalaumu wanazuoni pekee. Ni mfanya biashara yupi asiyejihusisha na siasa ili anufaishe biashara yake mwenyewe. Kwa hiyo lawama zote zinabebwa na huyo anayefanya mazingira ya watu hawa kutelekeza maeneo yao na kuingia huko kwenye siasa, kwa sababu ndiko kunakolipa zaidi.
 
Kila mkubwa yeyote akisimama jambo la kwanza ni kumsifia Rais. Why?. Wewe chapa kazi na kutokana na uchapa kazi yako Rais atakuona tu. Wengi ni wachumia tumbo.
 
Badala ya kutaja serikali kuwa imetoa huduma kutoka Kwenye makusanyo ya kodi za wananchi,

Badala yake wanamsifia kiongozi Mkuu utasema hiyo hela kaitoa mifukoni mwake ,

Na kwamba kama vile ni hisani badala ya wajibu .

Inashangaza mno!
 
Back
Top Bottom