Profesa Tibaijuka ataka maboresho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano kuimarisha mifumo ya uchaguzi

Profesa Tibaijuka ataka maboresho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano kuimarisha mifumo ya uchaguzi

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252


Profesa Anna Tibaijuka amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inahitaji kufanyiwa maboresho katika maeneo mbalimbali ili kuimarisha mfumo wa kisiasa na uchaguzi nchini.

Profesa Tibaijuka ameyasema hayo leo Ijumaa, Agosti 28, 2026, wakati akizungumza katika Jukwaa la Demokrasia Tanzania lililoandaliwa na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), jijini Dar es Salaam.

Alisema inawezekana kufanya reforms (mabadiliko) ili mgombea huru aruhusiwe, kuwe na reform za uandikishaji wa vyama vya siasa, kuna sheria ambazo zinapingana na Katiba ya 1977, vyote hivyo vibadilike.

Profesa Tibaijuka pia amesisitiza umuhimu wa kulinda kura katika uchaguzi, akisema wananchi wanapaswa kuelewa taratibu na wajibu wao katika usimamizi wa kura.

Amesema kulinda kura hakupaswi kutafsiriwa kama kufanya vurugu, bali wananchi wanapaswa kupewa uelewa kuhusu namna ya kuhakikisha kura zao zinalindwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za uchaguzi.

Soma pia: Kilichotokea Oktoba 29 ilikuwa ni mshituko "rapture"
 
Back
Top Bottom