Profesa Tibaijuka: Trump kusitisha misaada ARVs zitaadimika Afrika. African Union iitishe kikao maalum kuweka mkakati

Waziri wa zamani wa Ardhi, Prof. Anna Tibaijuka amesema afya za Mamilioni ya Waafrika na Watanzania zipo hatarini kutokana na uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump kusitisha misaada kwa Mashirika ya Afya Duniani hususani PEPFAR na GLOBAL FUND ambapo amesema uamuzi huo ukitekelezwa ni kiama.

Kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), Prof. Tibaijuka amesema “Upatikanaji wa madawa ya kuongeza kinga za mwili ARVs utaathirika, ninashauri Wizara ya Afya kuufahamisha umma wa Watanzania je ni hatua gani za haraka zinachukuliwa kutathmini jambo hili na kuchukua hatua stahiki?, ikibidi African Union waitishe kikao maalum kuangalia suala hili na kuweka mkakati wa pamoja, Waathirika wa gonjwa hili la UKIMWI ni Waafrika na ugonjwa haujulikani ulitoka wapi?, tujitetee”

“Aidha juhudi za kuthibiti maambukizi ya virusi vya UKIMWI ziwekewe nguvu mpya, upatikanaji wa ARVs utakuwa mgumu na kununua ARVs kibiashara ni jambo litakalohitaji bajeti kubwa na uwezo wa taifa kwa ujumla ni mdogo na jambo limekuwa la ghafla, Waathirika wengi hawana uwezo kununua madawa hayo wenyewe maisha yao yote”

“Afya zao zikidhoofika itatumika gharama kubwa kuwauguza hivo kusababisha umaskini na vifo, pia bila ARVs maambukizi yatashika kasi mpya, tuwe macho”

Source: Millard Ayo

Toa maoni yako
Tulivo na akili za ajabu watasema mafuta ya mwamposa si yapo
 
Ni muhimu zaidi wananchi kukujiepusha na ngono zembe ili kuepuka usumbufu wa Ukimwi baada.🐒
 
Lengo lake ngozi nyeusi tusiwepo duniani abaki yeye na pua yake kama katuni
Nani kawaambia mlane kavu?

Shida yetu waafrica au ngozi nyeusi kiujumla hatupendi kuwa responsible kwa makosa au maamuzi yetu bali hutafuta mtu wa kumtupia lawama.

Kingine ngozi nyeusi tunajiona tunastahilu misaada, msaada sio haki yako ujue
 
Nyie Kama mna rasilimali madini n.k mnaahindwa vipi kupunguza gharama za uendeshaji Kwa kujibana na kuwekeza katika Afya.

Trump anaweza akawa hayupo sahihi Ila msipende mambo ya bure lazima mjifunze kujitegemea.

Mpaka sasa mngekuwa serious mgekuwa mmeshaishinda vita ya ukimwi hata kwa asilimia kadhaa.
Mkuu ukimwi unaweza kuushinda wakat kila siku watu wanawaza ngono tena wanasema kavu ndio mzuri mbaya zaidi mwenge ukianza watu wananyanduana mpaka sehemu za siri zinaomba samahan
 
Mimi nilliiona hili na nikawaonya watu,baada ya watu kusema kuwa sasa ngoma ni kama mafua tu, nikasema kwasababu sisi Waafrika ndio tunaongoza kuwa na wagonjwa wengi iko siku atatokea Racist mmoja huko....
 
Nani kawaambia mlane kavu?

Shida yetu waafrica au ngozi nyeusi kiujumla hatupendi kuwa responsible kwa makosa au maamuzi yetu bali hutafuta mtu wa kumtupia lawama.

Kingine ngozi nyeusi tunajiona tunastahilu misaada, msaada sio haki yako ujue
Taarifa mkuu

Sina ukimwi pili sio limbukeni wa chupi

Naendelea nahoja shida ni socialization iliyo fanyika tangu nchi za afrika zinapewa au kupata uhuru hakukuwa na maandalizi na pia hakukuwa na uwezeshaji wa watu kujifunza zaidi katika kutengeneza madawa leo hii wangetoa fursa viwanda vikubwa vya dawa vinjengewe afrika na kuwapa fursa nyingine now afrika wangekuwa na kiburi jiulize mafuta afrika yapo ila yanapatika kiwepesi?
 
As I said.

Bado unatupa lawama kwingine.
 
Back
Top Bottom