Profesa Tibaijuka: Trump kusitisha misaada ARVs zitaadimika Afrika. African Union iitishe kikao maalum kuweka mkakati

Mbunge wa zamani wa Muleba, Prof Tibaijuka amesema kitendo cha Rais Trump wa US kusimamisha msaada ya kimataifa kitaleta Kiama Tanzania na Afrika

Pia soma > Trump asimamisha misaada kwa nchi nyingine kwa siku 90 ili kupitiwa upya. Tanzania nayo kuathirika

Trump amezuia misaada ya sekta za afya nk Ili Kufanya ukaguzi kama misasda hiyo inatumika kwa usahihi au fedha zinaishia mifukoni mwa eahuni wachache

Ahsanteni sana

---
Kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), Prof. Tibaijuka amesema “Upatikanaji wa madawa ya kuongeza kinga za mwili ARVs utaathirika, ninashauri Wizara ya Afya kuufahamisha umma wa Watanzania je ni hatua gani za haraka zinachukuliwa kutathmini jambo hili na kuchukua hatua stahiki?, ikibidi African Union waitishe kikao maalum kuangalia suala hili na kuweka mkakati wa pamoja, Waathirika wa gonjwa hili la UKIMWI ni Waafrika na ugonjwa haujulikani ulitoka wapi?, tujitetee”

“Aidha juhudi za kuthibiti maambukizi ya virusi vya UKIMWI ziwekewe nguvu mpya, upatikanaji wa ARVs utakuwa mgumu na kununua ARVs kibiashara ni jambo litakalohitaji bajeti kubwa na uwezo wa taifa kwa ujumla ni mdogo na jambo limekuwa la ghafla, Waathirika wengi hawana uwezo kununua madawa hayo wenyewe maisha yao yote”

“Afya zao zikidhoofika itatumika gharama kubwa kuwauguza hivo kusababisha umaskini na vifo, pia bila ARVs maambukizi yatashika kasi mpya, tuwe macho”
Tatizo lingine hili
 
Kwanza hapa kama 20% ya watanzania watakata motooo!!Hawa ni wale waliokua wanachukua huduma.

Magendo ya hizi dawa yataongezeka.
Na maambukizi kwa watoto yataongezeka.

Ila watu sasa wataacha kujiachia maana ile ya kusema DAWA SI BURE ITAISHA
 
Attachments

  • BAAABA2E-5406-4CC1-B6F0-CEA2990310E7.jpeg
    BAAABA2E-5406-4CC1-B6F0-CEA2990310E7.jpeg
    690.3 KB · Views: 2
Mbunge wa zamani wa Muleba, Prof Tibaijuka amesema kitendo cha Rais Trump wa US kusimamisha msaada ya kimataifa kitaleta Kiama Tanzania na Afrika

Pia soma > Trump asimamisha misaada kwa nchi nyingine kwa siku 90 ili kupitiwa upya. Tanzania nayo kuathirika

Trump amezuia misaada ya sekta za afya nk Ili Kufanya ukaguzi kama misasda hiyo inatumika kwa usahihi au fedha zinaishia mifukoni mwa eahuni wachache

Ahsanteni sana

---
Kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), Prof. Tibaijuka amesema “Upatikanaji wa madawa ya kuongeza kinga za mwili ARVs utaathirika, ninashauri Wizara ya Afya kuufahamisha umma wa Watanzania je ni hatua gani za haraka zinachukuliwa kutathmini jambo hili na kuchukua hatua stahiki?, ikibidi African Union waitishe kikao maalum kuangalia suala hili na kuweka mkakati wa pamoja, Waathirika wa gonjwa hili la UKIMWI ni Waafrika na ugonjwa haujulikani ulitoka wapi?, tujitetee”

“Aidha juhudi za kuthibiti maambukizi ya virusi vya UKIMWI ziwekewe nguvu mpya, upatikanaji wa ARVs utakuwa mgumu na kununua ARVs kibiashara ni jambo litakalohitaji bajeti kubwa na uwezo wa taifa kwa ujumla ni mdogo na jambo limekuwa la ghafla, Waathirika wengi hawana uwezo kununua madawa hayo wenyewe maisha yao yote”

“Afya zao zikidhoofika itatumika gharama kubwa kuwauguza hivo kusababisha umaskini na vifo, pia bila ARVs maambukizi yatashika kasi mpya, tuwe macho”
Aisee
 
Back
Top Bottom