Hahaha ndio maisha yalivyo, wote tumo duniani humu humu. Ningefarijika kuona waliosoma wanahamia sayari za mbali ili kutengeneza hizo class.
Mbona kuna ma professors wa music na hata mashahiri au nyie kwa tafsiri zenu mtu wa maana ni nani hasa?!
Tujifunze ku-value binadamu wote hata wale wenye mitindio ya ubongo, hakuna binadamu wa hovyo.
Sasa idiots na vilaza wanapaswa kuishi wapi au waishi vipi?! Social media haisemi ni intellectual peke yao ndio wanapaswa kuitumia.
Miziki yao mnaisikiliza lakini waimbaji mnawaita vilaza, hahaha jamani tujifunze kuvumiliana hanuna anayependa kuitwa idiot au kilaza.
Hata ukuwa na mali nyingi, akili nyingi,na elimu kubwa bado wewe ni binadamu kama asiyekuwa na mali au akili na elimu.
Tusiwe watu wa hivyo, tuheshimiane jamani.