Profesa wa literature aitahadharisha CCM kuhusu nguvu ya CHADEMA

Profesa wa literature aitahadharisha CCM kuhusu nguvu ya CHADEMA

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Prof. Joseph Mbele, mhadhiri wa literature wa Chuo Kikuu, Olaf College, USA; ametazama na kuchambua Uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti wa CHADEMA na kutoa angalizo zito kwa CCM. Kabla ya kuchapisha maoni yake hapa nilifanya mazungumzo naye kwa simu.

Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 26 Januari 2025

UCHAGUZI WA CHADEMA, CCM IMEPIGWA NA KITU KIZITO

Mimi sina chama, ila nina mtazamo kuhusu uchaguzi wa CHADEMA na ushiriki wa Mbowe kama mgombea.

Kwanza niseme, wakati wa Rais Magufuli, watu walipokuwa wanamsifusifu Magufuli sana, na wengine kutimkia CCM kuunga mkono juhudi, mimi nilichapisha makala mtandaoni nikimtambua Mbowe kama kiongozi wa mfano. Sikumtambua Magufuli kwa namna hiyo. Makala niliyoandika kuhusu Mbowe ni hii hapa: Freeman Mbowe kiongozi wa mfano

Mbowe amethibitisha ubora wake kama kiongozi kwa jinsi alivyoiendesha CHADEMA hadi kwenye huu uchaguzi, ambao tumeushuhudia ukiwa wa wazi, huru na haki. Fananisha na CCM, ambayo ina jadi ya kutumia hujuma na mizengwe katika chaguzi. CCM iliingia madarakani kwa njia haramu kabisa mwaka 2020. Nasema hivi kutokana na ushahidi wa ripoti iliyoandikwa na tume ya uchunguzi kutoka nchi za jirani na Tanzania, marafiki zetu. Haikuandikwa na mabeberu. Ripoti hii inaianika Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuendesha uchaguzi wa ovyo na kusababisha usiwe uchaguzi bali uchafuzi. Ripoti yenyewe ni hii hapa:

Baada ya hii ripoti kutoka, mtu ungetegemea kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ingejiuzulu au ingefutwa. Hilo halikutokea. Badala yake, CCM imeng'ang'ania tume hiyo ibaki, ingawa watu wamepiga kelele sana kwamba iundwe tume huru ya uchaguzi. CCM imegoma. Mtu unaweza kutafsiri kuwa CCM ina nia ovu ya kuendelea kuhujumu uchaguzi ujao. Mmoja wao alishatuhadithia kwa mbwembwe mambo ya goli la mkono, na akahadithia pia kwa mbwembwe kuwa ushindi katika uchaguzi hautegemei kura. Haya tumeyashuhudia kutoka CCM.

Katika hali hiyo yote, Mbowe ameiongoza CHADEMA kwenye mchakato wa uchaguzi ambao kwa uwazi wake, uhuru, na uhalali, hadi kwenye kuhesabu kura, na yeye kukubali matokeo, ameweka mfano wa kiwango cha juu kabisa. Kwa uchaguzi huu, Mbowe na CHADEMA wamekuwa kioo, na wameipiga CCM na kitu kizito. Ndio, CCM imepigwa na kitu kizito. Hongera Mbowe. Hongera Lissu. Hongera CHADEMA. Nyinyi wote ni washindi, ushindi wa kishindo.

Binafsi naona Mbowe alifanya vizuri kugombea uenyekiti sambamba na Tundu Lissu. Kwa kufanya hivyo katika kampeni na uchaguzi, amemtikisa Tundu Lissu ili Tundu Lissu mwenyewe na sisi wote tuone uimara wake Lissu ukoje. Kushindanishwa namna hii kuna manufaa sana kwa kiongozi, la sivyo, anaweza kubweteka akashindwa kujua wapi paa litavuja ikija mvua. Kwa mtazamo wangu, viongozi wote, wa ngazi zote, wakiwemo wa CCM, wawe wanashindanishwa hivi ilivyofanyika CHADEMA. Mbowe amemwachia Tundu Lissu fundisho lenye manufaa katika safari yake ya uenyekiti. Ninachotaka kusema ni kuwa Mbowe hajashindwa lolote, bali kwa kugombea uenyekiti, alifanya uamuzi wa manufaa kwa CHADEMA.

Prof. Joseph Mbele,
Mhadhiri wa Literature,
Chuo Kikuu, Olaf College, Marekani
25 Januari 2025
 
Attachments

  • 1737905316135.jpg
    1737905316135.jpg
    426.3 KB · Views: 3
Katika hali hiyo yote, Mbowe ameiongoza CHADEMA kwenye mchakato wa uchaguzi ambao kwa uwazi wake, uhuru, na uhalali, hadi kwenye kuhesabu kura, na yeye kukubali matokeo, ameweka mfano wa kiwango cha juu kabisa. Kwa uchaguzi huu, Mbowe na CHADEMA wamekuwa kioo, na wameipiga CCM na kitu kizito. Ndio, CCM imepigwa na kitu kizito. Hongera Mbowe. Hongera Lissu. Hongera CHADEMA. Nyinyi wote ni washindi, ushindi wa kishindo.
Well narrated
 
Binafsi naona Mbowe alifanya vizuri kugombea uenyekiti sambamba na Tundu Lissu. Kwa kufanya hivyo katika kampeni na uchaguzi, amemtikisa Tundu Lissu ili Tundu Lissu mwenyewe na sisi wote tuone uimara wake Lissu ukoje. Kushindanishwa namna hii kuna manufaa sana kwa kiongozi, la sivyo, anaweza kubweteka akashindwa kujua wapi paa litavuja ikija mvua. Kwa mtazamo wangu, viongozi wote, wa ngazi zote, wakiwemo wa CCM, wawe wanashindanishwa hivi ilivyofanyika CHADEMA. Mbowe amemwachia Tundu Lissu fundisho lenye manufaa katika safari yake ya uenyekiti. Ninachotaka kusema ni kuwa Mbowe hajashindwa lolote, bali kwa kugombea uenyekiti, alifanya uamuzi wa manufaa kwa CHADEMA.
Wenye akili na jicho la tatu wametazama deep siyo yule Profesa wa Ubungo aliyesema ni ujinga mtu na Makamu kugombea nafasi moja

Sasa Dunia imejifunza kutoka Tz
 
Huyu anayetunga vitabu vya sungura na fisi, mara sijui paka na panya
 
Bila katiba mpya upinzani kushinda si rahisi yaani kuna wizi wa kura wa kutisha aliyefanikiwa kusimamia uchaguzi serikali za mitaa ataungana na mm
 
Kama kuna kitu cdm wamenikosha na watanzania wengi ni jinsi walivyoendesha wao, ukaisha kwa amani na mshindi kupatikana kwa njia halali. Hakuna kitu kimewauma ccm kwa jinsi mchakato ule ulivyokuwa wa viwango, uwazi na haki.
 
Ccm hawana raha kabisa. Waliandaa hadi majeshi wakisubiri kinuke😄😄😄
 
Ccm hawana raha kabisa. Waliandaa hadi majeshi wakisubiri kinuke😄😄😄
Imewauma vibaya sana, na ikawa aibu sana ndani ya maumivu hayo, hasa ukizingatia namna wagombea wao wa urais walivyopatikana kihuni.
 
Back
Top Bottom