Amun Ra
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 4,713
- 7,218
Yule yupo kwenye corridor za lumumba anawinda teuziNilijua Prof wa Kule Jalalani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yule yupo kwenye corridor za lumumba anawinda teuziNilijua Prof wa Kule Jalalani
Mtu akihamia ccm hata angekua msomi vipi huaga anakua takataka tu; huwezi kutofautisha maoni ya msomi na asie soma; tena sometimes bora niwasikilize darasa la 7 wa ccm kuliko profesa au doctor from that chama, pumba tupu tu. Jumanne Kishimba, Joseph Kasheku Msukuma they are far better than professors on that party. Sijui huaga wanafanyiwa nini baada ya ku join kule, nasubiri siku David Kafulila nae akichaguliwa nafasi nyingine ya kisiasa jinsi atakavyo kua. Halafu eti watu wale ndio kabisaa tunawategemea kututoa hapa. Wametengeneza syllabus mpya ya elimu LAKINI watoto wao wenyewe hawawapeleki kwenye shule hizo, ina huzunisha. Kwamba walicho kitengeneza wenyewe, hawakitaki lakini wanatulazimisha wananchi tukiamini, interestingNilishangaa Mkumbo anaukosoa
Maoni yake kila mmoja anao huru wa kuandika hakuna jipya!Prof. Joseph Mbele, mhadhiri wa literature wa Chuo Kikuu, Olaf College, USA; ametazama na kuchambua Uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti wa CHADEMA na kutoa angalizo zito kwa CCM. Kabla ya kuchapisha maoni yake hapa nilifanya mazungumzo naye kwa simu.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 26 Januari 2025
UCHAGUZI WA CHADEMA, CCM IMEPIGWA NA KITU KIZITO
Mimi sina chama, ila nina mtazamo kuhusu uchaguzi wa CHADEMA na ushiriki wa Mbowe kama mgombea.
Kwanza niseme, wakati wa Rais Magufuli, watu walipokuwa wanamsifusifu Magufuli sana, na wengine kutimkia CCM kuunga mkono juhudi, mimi nilichapisha makala mtandaoni nikimtambua Mbowe kama kiongozi wa mfano. Sikumtambua Magufuli kwa namna hiyo. Makala niliyoandika kuhusu Mbowe ni hii hapa: Freeman Mbowe kiongozi wa mfano
Mbowe amethibitisha ubora wake kama kiongozi kwa jinsi alivyoiendesha CHADEMA hadi kwenye huu uchaguzi, ambao tumeushuhudia ukiwa wa wazi, huru na haki. Fananisha na CCM, ambayo ina jadi ya kutumia hujuma na mizengwe katika chaguzi. CCM iliingia madarakani kwa njia haramu kabisa mwaka 2020. Nasema hivi kutokana na ushahidi wa ripoti iliyoandikwa na tume ya uchunguzi kutoka nchi za jirani na Tanzania, marafiki zetu. Haikuandikwa na mabeberu. Ripoti hii inaianika Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuendesha uchaguzi wa ovyo na kusababisha usiwe uchaguzi bali uchafuzi. Ripoti yenyewe ni hii hapa:
Loading…
s3-eu-west-1.amazonaws.com
Baada ya hii ripoti kutoka, mtu ungetegemea kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ingejiuzulu au ingefutwa. Hilo halikutokea. Badala yake, CCM imeng'ang'ania tume hiyo ibaki, ingawa watu wamepiga kelele sana kwamba iundwe tume huru ya uchaguzi. CCM imegoma. Mtu unaweza kutafsiri kuwa CCM ina nia ovu ya kuendelea kuhujumu uchaguzi ujao. Mmoja wao alishatuhadithia kwa mbwembwe mambo ya goli la mkono, na akahadithia pia kwa mbwembwe kuwa ushindi katika uchaguzi hautegemei kura. Haya tumeyashuhudia kutoka CCM.
![]()
Tanzania Elections Watch – Final Observation Report on the General Elections Held in Tanzania on October 28, 2020 - The Elephant
A report released on 28th February 2021 by the Tanzania Elections Watch on the October 2020 elections in Tanzania.www.theelephant.info
Katika hali hiyo yote, Mbowe ameiongoza CHADEMA kwenye mchakato wa uchaguzi ambao kwa uwazi wake, uhuru, na uhalali, hadi kwenye kuhesabu kura, na yeye kukubali matokeo, ameweka mfano wa kiwango cha juu kabisa. Kwa uchaguzi huu, Mbowe na CHADEMA wamekuwa kioo, na wameipiga CCM na kitu kizito. Ndio, CCM imepigwa na kitu kizito. Hongera Mbowe. Hongera Lissu. Hongera CHADEMA. Nyinyi wote ni washindi, ushindi wa kishindo.
Binafsi naona Mbowe alifanya vizuri kugombea uenyekiti sambamba na Tundu Lissu. Kwa kufanya hivyo katika kampeni na uchaguzi, amemtikisa Tundu Lissu ili Tundu Lissu mwenyewe na sisi wote tuone uimara wake Lissu ukoje. Kushindanishwa namna hii kuna manufaa sana kwa kiongozi, la sivyo, anaweza kubweteka akashindwa kujua wapi paa litavuja ikija mvua. Kwa mtazamo wangu, viongozi wote, wa ngazi zote, wakiwemo wa CCM, wawe wanashindanishwa hivi ilivyofanyika CHADEMA. Mbowe amemwachia Tundu Lissu fundisho lenye manufaa katika safari yake ya uenyekiti. Ninachotaka kusema ni kuwa Mbowe hajashindwa lolote, bali kwa kugombea uenyekiti, alifanya uamuzi wa manufaa kwa CHADEMA.
Prof. Joseph Mbele,
Mhadhiri wa Literature,
Chuo Kikuu, Olaf College, Marekani
25 Januari 2025
Naonaga tu vitabu twake ambavyo vinastahili kutungwa na mtu wa form six. Not worth of a professor..... Ukimsoma Franz Fanon na hizo sungura na fisi ndio utawajua tofauti zao, au hata Haroub OthmanNadhani ukishakuwa ccm hata akili zinatepeta
Hakuna kitu kimewauma ccm kwa jinsi mchakato ule ulivyokuwa wa viwango, uwazi na haki.💪🏿😂Kama kuna kitu cdm wamenikosha na watanzania wengi ni jinsi walivyoendesha wao, ukaisha kwa amani na mshindi kupatikana kwa njia halali. Hakuna kitu kimewauma ccm kwa jinsi mchakato ule ulivyokuwa wa viwango, uwazi na haki.
makaratasi au vitabu?Huyu anayetunga vitabu vya sungura na fisi, mara sijui paka na panya
Kitabu cha kusimulia sungura anavyokimbizana na fisi nacho ni kitabu?makaratasi au vitabu?
kwa kweli yeye na Yericko wako sawa tu, ndio maana Lissu anawaitaga profesorial rubbish, Mungu umenitoa jalalani...Kitabu cha kusimulia sungura anavyokimbizana na fisi nacho ni kitabu?
Amejaza mandevu ku-justify uprofesa
Vitabu vya watoto hata vikaragozi ni taaluma kubwa yenye kuhitaji weledi na elimu ya kutosha.. Wee unadhani watu wanajiandikia tuu.. Jaribu uoneNaonaga tu vitabu twake ambavyo vinastahili kutungwa na mtu wa form six. Not worth of a professor..... Ukimsoma Franz Fanon na hizo sungura na fisi ndio utawajua tofauti zao, au hata Haroub Othman
Mimi chadema
Huyu Prof Mbele alisomea kwenye vyuo vya marekani ambavyo ni bure kabisa, sawa na shule za Dk Kadeghekwa kweli yeye na Yericko wako sawa tu, ndio maana Lissu anawaitaga profesorial rubbish, Mungu umenitoa jalalani...
Ccm viwanja vya mpira parking za magari na ikulu bado tu ni maskini naona umekunywa dawa za tunguri zako zimekudhuru akili!Masikini ccm😂😂😂