Professa Palamagamba Aidan Kabudi mwalimu wa Tundu Lissu mwaka wa kwanza sheria, atasimama mahakamani kumwakilisha CP Awadh dhidi ya vibaraka

😁😁😁😁
 

Wewe yawezekana uliishia kwenye certificates au vidiploma.

SIsi wengine tunajua wazi kabisa kuna watu wengi ambao waliwafundisha wengine, na hao wengine wakawa wana weledi maradufu ya watu waliowafundisha.

Mimi binafsi nawaheshimu sana walionifundisha, lakini likija suala la weledi wa kwenye fani yangu, wengi walionifundisha kwenye hatua fulani, hawajui wala kunifikia nilipofika hata kwa 50%.

Hivi unajua pale chuo Kikuu Prof. Kabudi alikuwa anafundisha nini! Kawaulize waliosoma sheria. Somo lake kuu lilikuwa ni family Law, yaani masuala ya mirathi na ndoa.

Kwa pale kitivo cha sheria, somo hilo linachukuliwa kama ilivyo DS kule Science, ni somo ambalo hakuna anayeweza kushindwa.
 
Mleta mada anadhani ukifundishwa na mwalimi mjinga na mwanafunzi utakuwa mjinga vilevile au ukifundishwa na mwalimu mwelevu sana na wewe utakuwa utakuwa mwelevu sana.
 
Lakini amesahau kuwa yeye na wenzake wote na majaji pia wamepita mikononi mwa Prof Kabudi, huwezi kuwa mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kama mtihani wako haujasahihishwa na Prof.Kabudi.

Mwanafunzi anaweza kumzidi uwezo Mwalimu wake. Tofauti tu ni kuwa mwalimu akizaliwa mapema kabla ya Mwanafunzi. Kuwa Mwalimu haimanishi kuwa una akili au uwezo kuliko wanafunzi wako.
 
 
Ndio maana alikazania, "We are social fathers" sio lazima ujue kuwa mkeo amekuzalia watoto halisi au kakubambikia we lea tu🀣
 
Sasa umeandika nini?
 
Mbona una chuki sana kakukosea nini Lissu? Hivi hata ungekuwa wewe ndie Lissu upigwe risasi namna ile ungebaki Tanzania?
Simchukii lissu kama yeye. Mimi wala binafsi simjui wala sijui kama nimewahi kumuona zaidi ya kwenye tv na magazeti. Ni kwamba kiitikadi simuungi mkono japo yapo mengi anayotetea nayakubali na nimewahi kumuunga mkono huku jf.
Nasikia ni mtu mcheshi pengine tukionana tunaweza hata kua marafiki.
 
Kesi yoyote ni ushahidi uliopo, siyo kwamba huyu alikuwa mwalimu wangu.
 
23 Agosti 2024
Ngorongoro, Arusha
Tanzania

PROF. PALAMAGAMBA KABUDI - WATANZANIA TUPO WOTE SAWA, TAIFA LA UPENDO TUNA HAKI SAWA ....RAIS ANAWAPENDA SANA WANA NGORONGORO ... IBARA YA 8 INASEMA MAMLAKA YOTE YA SERIKALI INATOKA KWA WANANCHI .... KAZI KUBWA NI KUHAKIKISHA USTAWI ....


View: https://m.youtube.com/watch?v=Xj9xjdD7bcwLeo Profesa Palamagamba Kabudi akiendelea na stori zake alipofika katika kilima ambacho wakaazi wa Ngorongoro kwa siku tano mfululizo wamepiga kambi kupinga kuhamishwa
 
Yawezekana mwalimu wa Elon Musk yupo na pesa kuliko Elon
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…