PROFESSIONALISM NA CUSTOMER SERVICE NI CANCER INAYOIKABILI SEKTA YA UTALII TANZANIA.

PROFESSIONALISM NA CUSTOMER SERVICE NI CANCER INAYOIKABILI SEKTA YA UTALII TANZANIA.

Mla Bata

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2013
Posts
8,461
Reaction score
19,779
Wasalaam,


Wakuu, kuna jambo ambalo naamini tunapaswa kulijadili kwa uzito, hasa sisi wadau wa sekta ya utalii.


Tanzania tumebarikiwa kuwa na vivutio vya kiwango cha dunia kuanzia Serengeti, Ngorongoro, Kilimanjaro hadi Zanzibar. Lakini pamoja na utajiri huu, bado tunapaswa kujiuliza kama tunafanya vya kutosha kuhakikisha wageni wanapata huduma inayolingana na ubora wa vivutio vyetu.


Ukiangalia baadhi ya nchi za Afrika kama Morocco, Misri na Afrika Kusini, utaona zinafanikiwa kuvutia idadi kubwa ya wageni kwa sababu mbalimbali, zikiwemo miundombinu, matangazo, historia na mifumo ya utalii. Tanzania hatupaswi kuishia kujivunia vivutio vyetu tunapaswa pia kujiuliza tunajifunza nini kutoka kwa washindani wetu.


Changamoto moja inayostahili kuangaliwa ni lack of professionalism katika baadhi ya maeneo ya utoaji huduma.


Unaweza kukutana na receptionist anayekupokea kwa dharau, mhudumu wa mgahawa anayekujibu kwa ukali, tour operator asiyekuwa serious kwenye mawasiliano, guide asiyejua namna ya kushughulikia malalamiko, au dereva anayemtendea vibaya abiria.


Hata katika baadhi ya huduma za kijamii, mabar, hospital wananchi wanakutana na lugha zisizofaa wanapokwenda kutafuta huduma wanazostahili, same issue (Professionalism & Customer care)



Swali ni hili: Kwa nini wakati mwingine tunachukulia customer care kama upendeleo badala ya kuwa wajibu wa kitaalamu?


Mteja kuuliza swali si usumbufu. Kulalamika kuhusu huduma aliyolipia si dharau kwa mfanyakazi. Na kuwa na uzoefu wa miaka mingi kazini hakukupi ruhusa ya kumdhalilisha mteja.


Mgeni anaweza kufurahia Serengeti lakini akaharibu uzoefu wake kutokana na huduma mbovu hotelini, usafiri usio na mpangilio au mawasiliano yasiyo ya kitaalamu. Anaondoka, anaandika review mbaya na anaweza asirudi tena.


Kwa upande mwingine tunaweza tusilaumu wafanyakazi pekee. Mishahara duni, mazingira magumu ya kazi, ukosefu wa mafunzo na usimamizi dhaifu vinaweza kuchangia tatizo hili. Waajiri na taasisi husika wana wajibu wa kujenga mazingira yanayowezesha huduma bora kwenye sekta husika.


Tunahitaji nini? Mafunzo ya customer care, uwajibikaji, usimamizi bora na utamaduni wa kuheshimu kila mteja bila kujali uwezo wake wa kifedha rangi wala kabila,

Iliwahi kunitokea Mwaka mmoja nipo Likizo na Shemeji yenu jijini Dar es salaam, jioni moja tukaingia kiwanja fulani kwaajili ya kupata chakula cha jioni, namna tulivyopokelewa pale na wahudumu ilikuwa poa sana lakini haikuhitaji maelezo kuwa ilikuwa ni racial privilege sababu ya yule mama wa kizungu. A week later nikarudi pale pale na mshikaji wangu kupata mbili tatu, ule uchangamfu wa siku ya kwanza sikuuona tena hapo nikaconfirm theory yangu.

Hili nimelisikia kwa watu wengi wakilalamika kuwa sehemu nyingi za chakula, vinywaji na starehe Dar zenye wateja wengi wa mataifa mengine, ukijulikana ni mbongo (local) huwezi kupapatikiwa kama anavyohudumiwa ngozi nyeupe, how crazy!


Maswali kwa wadau:

Kwa uzoefu wako, ni changamoto gani kubwa zaidi kwenye customer service ya utalii Tanzania: mawasiliano, ukarimu, muda wa huduma, usafi, bei au uwajibikaji?


Kwa maoni yako, ni nani anayepaswa kuongoza maboresho ya huduma: waajiri, wafanyakazi, serikali, vyuo vya utalii au wateja wenyewe?


Kama ungepewa nafasi ya kubadilisha jambo moja kwenye sekta ya utalii Tanzania leo, ungeanza na nini?

Nawasilisha.✍️

Wasalaam,

Mla bata

München, Deutschland 🇩🇪.
 
Back
Top Bottom