Professor J na Frank Majani wana beef zito

haya ya kuhusu beat sijali sana, lkn kuna unafiki mkubwa ndani ya bandiko la J, kwanza anajifanya eti anaweka taarifa tu sawa kwamba wala mpango wa gawio hana kabisa. Lkn kwenye maneno ya kwamba sijalipwa hata senti tano ndo unafiki wa J unajidhihirisha kwamba naye alistahili asilimia kadhaa ktk gawio, wakati majani kamchana kwenye kudai J wala hakuwa na habari, ila zimetoka anatamani angepewa walau visenti kadhaa.
 
COSOTA mmekosea, millioni 100 sijalipwa mimi, amelipwa mmiliki halali wa ile beat, ndugu Pfunk majani.
Wekeni kumbukumbu sawa.
Mmiliki halali wa beat ni aliyeitengeza au aliyeilipia ili aitumie?
Beat sidhani kama alipewa bure, sasa hata kama ameipigania hiyo kesi bado haiondoi ukweli kuwa baada ya kuitengeneza(Majani) ile beat alimpatia Professor J kwa malipo.
Hayo mengine nadhani COSOTA ndiyo chanzo baada ya kutoa taarifa isiyo sahihi, kulikuwa na kila sababu kwa Professor J ku'clarify, kama between the lines alikuwa anadai 'cut' flani kijanja tutabakia ku'speculate tu kwani ukweli wa moyoni mwake anaujua mwenyewe.
Kwa P Funk(Majani) kuwaka ni defensive mechanism ili Professor J asifikirie mgao kama alikuwa na wazo hizo japo COSOTA kama wakiona hawakutenda haki na ikaamuliwa vinginevyo halitakuwa suala la kutumia mabavu bali itatakiwa wafuate utaratibu utakavyoamuliwa.
All in all sidhani kama mambo yatabadilika, Majani ataendelea kuwa ndiyo mnufaika 100% kwani sitegemei Professior J kuvalia njuga hilo suala eti mpaka na yeye apate mgao.
 
Mimi nilishafika mpaka studio yake Masaki na washkaji, nikakaa naye sana, nikaona swag lake stratospheric kama yupo Compton or something.

Sidhani kama Majani katika maisha yake yote alishawahi kua na ubavu wa kuweka studio zake za Bongo records Masaki!

Studio zake zipo Mwenge maisha yao yote!

Hiyo ya Masaki labda umechanganya mambo!

Check tena vizuri!
 
Hawa watu wawili mimi binafsi nna waheshimu sana kwani wana mchango mkubwa mno kwenye mziki wetu mpaka hapa ulipofikia.

Sioni sababu yoyote ya kuliweka hili suala lao la kimaslahi kwenye social media ambapo saana inawaharibia reputation zao tu na kuwashushia heshima.

Mambo ya kipuuzi kama haya ya wawaachie akina Harmonize na Nandy
 
Prof Jay amesahihisha taarifa iliyopotoshwa, Majani kapaniki sijui tatizo nini. Ukisema 'beef' labda Majani ndo analitafuta
Halafu majani anaonekana kama ana frustration hivi.

Maana naona ameelezea vitu vingine hata visivyohusiana kabisa na hicho alichokisema Prof Jay kwenye post yake
 
Ok tufanye wewe ndo Prof alafu unaambiwa umevuta 100 sasa unataka kukanusha ungesemaje ili usilete mvutano.
Mimi sijui mambo ya haki milki na haki shiriki yanafanyaje kazi ola naona kama prof alistahili kupata chochote kwani bila sauti ya Prof J nani angetilia maani beat lake kama yeye mkali kama KEN G atoe beat bila sauti za wasanii tuone mwitikio wake. ki ubinaaadamu angempa japo kidogo
 
Kabisa Sema Prof J hakutaka kumkamia mwana na Majani anadai hiyo pesa kulikuwa na Kesi mahakamani mpaka akapata hilo gawio lakin ishu ni kuwa Prof J yeye hakuwa anafatilia wala kushiriki kwenye Kesi mahakamani so Hii pekee ndo sababu naona Majani anayo lakini kusema Yeye ndo anamiliki beat asilimia 100 Nooo ni uongoo ndo maana hata msanii akitumia beat la msanii mwingine Anaemind na kumshatki ni msanii mwenye beat SIO PRODUCER.
 
Alafu anavyosema hakuna Ubunifu wala sauti ya prof J iliyotumika??? Sielewi hapa kwani Prof j hakutumia hii beat kutoa song..
 

Ni kweli hao kina JAY na wenzake wanafiki tu.. hawakumpa support hata kidogo kwenye hiyo kesi P alikua akipambana mwenyewe tu wakati kina jay licha ya nafasi zao hawakumpa support ..halafu unaibuka eti hizo pesa sikupewa mimi!! Wtf!! naomba P aendelee kupambana hivyo hivyo ili apate haki ya nyimbo zake zote alizowatengenezea hao wanafiki..wanaojiona wametoka kwa uwezo wao wakati P alikuwa akiwarekodia bure tu studioni kwake!!..
 
Kati ya makosa makubwa aliyofanya majani enzi zake ni kuwarekodia bure wasanii yaani kishkaji tu.. anakurekodia akimaliza anabeba na kuipeleka mwenyewe studio ..yaani ana produce na kufanya promo kabisa kishkaji tu daah. huo ndio uzembe ambao master jay hakufanya au huyu Salam hawezi kufanya.. lkn huwezi kumlaumu sana alikua amelipuka sana kipindi kile haikua akili yake sasa ndio zinamrejea
 
Yote kayataka COSOTA.
kusema kuwa walimpigania profesa j.kupata hela zake.
kiukweli beat ni ya majani ya NIKUSAIDIEJE.
 
kuna wakati prodyuza anaweza AKAKUPA BEAT BURE.
Sana Sana utokea pale unaporekodi ALBUM.
 
Majani ni Mpuuzi tu kama MIBANGE aliyovuta imempanda kichwani aende mirembe wakampe tiba ya akili,hata kama beat ni la majani Prof J alistahili na yeye apate mgao hata kidogo....Majani ana stress nyingi sana ndio maana mtu wa kupanic pasipo sababu yeyote,huyo bora aendelee kukaa huko huko DAR,akija A-Town na stress zake watu wanampa "BETO za kutosha.
 
Ni kweli nilichoona mimi hapo ni kujishtukia
 
Kama kikao kilikua ni cha kamati ya bunge haya majibu pia yalipaswa kuishia huko huko kwenye kamati ya bunge, kuyaleta public na ku mtaja mtu moja kwa moja sio sawa Jay kakosea.
You have a point
 
Sidhani kama Majani katika maisha yake yote alishawahi kua na ubavu wa kuweka studio zake za Bongo records Masaki!

Studio zake zipo Mwenge maisha yao yote!

Hiyo ya Masaki labda umechanganya mambo!

Check tena vizuri!
Pitia vizuri makablasha yako Pfunk kakaa MASAKI mzee baba na alikuwa na studio Masaki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…