Professor J na Frank Majani wana beef zito

Professor J na Frank Majani wana beef zito

Sure, ukisoma bandiko la Jay kuna info flani inawasilisha kijanja, hiyo ni zaidi ya kuweka kumbukumbu sawa. Ni Kama vile anawaambia Cosota namna hawajazingatia gawio lake, kwa upande wa Majani nae kazingua, katumia nguvu nyingi Sana so anafanya kile ambacho Jay alikitaka
Huo ndo ukweli halisi....maana wimbo ulioleta hyo pesa ni ule wa chamilione alitumia beat ya nikusaidieje...prof alilalamika Sana kwamba jamaa katumia beat pasipo hata kupewa taarifa...naona wakapatanishwa ndo wakatoa Ngoma ya sivyo ndivyo....baadae Ile Ngoma ya chamilione bomboclat (aliyotumia beat ya nikusaidieje)ikachukuliwa na Walt Disney studios kama soundtrack ya movie aliyofanya lupita nyon'go (Queen of Katwe) ambapo chamilione alilamba km USD 50,000 km sikosei ....majani akapambana na yeye apate mgao maana lile beat alitengeneza...mzozo ukawa mkali kumpeleka mahakamani josee... nadhani mzigo ulivyotoka shida ndipo ilipoanzia..
 
Kwani Prof J ni my amaji wa majani kiasi cha fedha alicho lipwa kilistahili kutajwa au swala lingebaki kwa majani?
Profesa J ni msemaji wa Profesa J.

Kazushiwa kwamba kalipwa yeye.

Katika kanuni za "Information Theory", ukitaka kukanusha uongo, keta ukweli.

Sasa Profesa J katumia kanuni hii.

Kasema mimi sikulipwa, huo ni uongo.

Ukweli ni upi?

Ukweli ni kwamba aliyelipwa ni Majani.

Sasa Majani kalipuka, hajajibu hoja ya msingi kwamba kalipwa yeye. Anasema habari tofauti kwamba anastahili kulipwa. Kwani nani kasema hastahili kulipwa?

Alichofanya Majani kinaitwa "ad hominem attack".

Ni tabia ya mtu ambaye hana hoja, anashindwa kujibu hoja, sasa anamvamia na kumsema mtu binafsi badala ya kujibu hoja.
 
Na hiki ndo watu wengi wamesahau au wanajisahaulisha maksudi,jeez ni pokitician now lazima kauli zozote znzomuhusu aweke clarifications.
Imagine sttatus km hio shabiki tu useme hela imemuuma[emoji23][emoji23]
Kwa maisha yetu ya leo, zikizagaa habari Mbunge umepiga shilingi milioni mia, kesho unaweza kushtukia robo ya jimbo lako imepiga foleni ofisini kuomba mgao.

Ndiyo maana Jay kaona aweke mambo wazi asije kupata tabu buree kwa wapiga kura wake huko.
 
majani yuko sahihi 100% bandiko la profesa lina kinyongo flani "sijalipwa hata senti 5,hela yote kalipwa majani chini ya usimamizi wenu" ikiwa na maana prof. alitaka % flani ila kwa figisu za basata ajapata hata senti zote zimeenda kwa majani (tafsiri yangu)

Na majani anajibu "nimehangaika na kesi peke yangu"leo nafanikiwa unalalama inaonesha prof. alikuwa na majani kwenye hiyo kesi (siijui) ila prof. akamnawa jamaa

NB: basata ndo mnafiq kusema prof. kapata 100m huku wakijua si kweli (ama walijua naye yumo kwenye kesi basi atapata mgao)

majibu ya prof. yana unafiq flani, sema majani yuko wida kaaamua kumchanikia bila kuficha
Mkuu una jicho la tatu kabsaaa. Fikra zangu pia ziko sambamba na hapa... Prof alikua na Intention iliyojificha na si ingine bali ni kutoa shutma kwa cosota (ambao kwa mda mrefu Majani amekua akiwatuhum kushindwa kusimamia hakimiliki za Sanaa na wasanii nchini) kwamba wamesimamia haki Upande mmoja (kwa majani) na kumsahau yeye

Prof ni mwanasiasa, alitafuta namna ya kufikisha hili bila kuonekana ana ubaya na pfunk au kuonekana hana shukran kwa jinsi majani alivochangia mpk yeye kufikia hapo so akajificha kwenye maneno yenye siasa ndani yake
Sasa Pfunk kwa upande wake si mwanasiasa, yeye anapauka tu lolote linalokuja kichwani bila kuw makini na athari za baadae
Mfano kulikua hakuna ulazima wa kusema amepigania sana haki zake kwa hiyo miaka 26 sijui mara hapo ndio mwisho wa kuwabeba wasanii (sasa hapa simwelewi sijui ana maanisha wasanii ndio waliomdhulum haki zake? au....)
 
p funk yupo sahihi,tatizo watu hawajui mziki wala chimbuko la hii kesi ilikuwaje mpaka ikafika hapa,majani yupo sahihi sana
 
Mkuu una jicho la tatu kabsaaa. Fikra zangu pia ziko sambamba na hapa... Prof alikua na Intention iliyojificha na si ingine bali ni kutoa shutma kwa cosota (ambao kwa mda mrefu Majani amekua akiwatuhum kushindwa kusimamia hakimiliki za Sanaa na wasanii nchini) kwamba wamesimamia haki Upande mmoja (kwa majani) na kumsahau yeye

Prof ni mwanasiasa, alitafuta namna ya kufikisha hili bila kuonekana ana ubaya na pfunk au kuonekana hana shukran kwa jinsi majani alivochangia mpk yeye kufikia hapo so akajificha kwenye maneno yenye siasa ndani yake
Sasa Pfunk kwa upande wake si mwanasiasa, yeye anapauka tu lolote linalokuja kichwani bila kuw makini na athari za baadae
Mfano kulikua hakuna ulazima wa kusema amepigania sana haki zake kwa hiyo miaka 26 sijui mara hapo ndio mwisho wa kuwabeba wasanii (sasa hapa simwelewi sijui ana maanisha wasanii ndio waliomdhulum haki zake? au....)
Kipindi hicho midundo mikali inatoka kwa pfunk aka kinywele kimoja [emoji23] ,,

Enzi hizo afande Sele anazindua album yake inayoitwa mkuki moyoni,, pale uwanja wa Jamhuri Morogoro

Zikazuka tetesi kwamba Majani, pro Jay, pamoja na yule mama mzungu sikumbuki jina lake,, walimdhulumu mshiko afande sele,,

Ilikuwa noma sanaaaa

Tuliruka mamidundo noma sanaa,,

[emoji23][emoji23][emoji23],,

Ila nimetoka nje ya mada.
 
Mmiliki halali wa beat ni aliyeitengeza au aliyeilipia ili aitumie?
Beat sidhani kama alipewa bure, sasa hata kama ameipigania hiyo kesi bado haiondoi ukweli kuwa baada ya kuitengeneza(Majani) ile beat alimpatia Professor J kwa malipo.
Hayo mengine nadhani COSOTA ndiyo chanzo baada ya kutoa taarifa isiyo sahihi, kulikuwa na kila sababu kwa Professor J ku'clarify, kama between the lines alikuwa anadai 'cut' flani kijanja tutabakia ku'speculate tu kwani ukweli wa moyoni mwake anaujua mwenyewe.
Kwa P Funk(Majani) kuwaka ni defensive mechanism ili Professor J asifikirie mgao kama alikuwa na wazo hizo japo COSOTA kama wakiona hawakutenda haki na ikaamuliwa vinginevyo halitakuwa suala la kutumia mabavu bali itatakiwa wafuate utaratibu utakavyoamuliwa.
All in all sidhani kama mambo yatabadilika, Majani ataendelea kuwa ndiyo mnufaika 100% kwani sitegemei Professior J kuvalia njuga hilo suala eti mpaka na yeye apate mgao.
Beat kuwa Mali ya msanii au producer nadhani ni kutokana na mkataba na jinsi makubaliano yalivyo. Kwa navoelewa mimi kipindi hicho producer majani alikua anamiliki beat zake ndio mana hata alikua hawauzii wasanii alikua anawarekd bure kabisa ila yeye alikua anamalizana nao kwenye mapato ya shows na mauzo ya Album
Ndio maana hata ukiangalia aina ya wasanii aliokua anawachagua ni wale wenye vipaji hasa ili akiwa enrol kwny Lebel waweze kuuzika fast.... Check Prof J, Juma Nature, Fid Q, Afande Sele, Mangwair, Feruz, J. Moo, Temba nk nk jamaa alikuwa anakuchukua hafu hulipi ata Mia wewe unarekodi tu bure kabisa hafu mtakatana huko mbele kwa mbele

Kuna kipindi nilimsikia akilalamika kuwa system yake hiyo ndo ilimuumiza mpk akashindwa kuendelea na wkt mwingine akitoa lawama kwa Cosota.

Nadhani hii system ya sasa iko tofauti na ilivyo kwa majani maana naona wasanii wananunua beats tena kwa pesa kubwa tu so wanakuwa na umiliki wa 100% kwny nyimbo yote mf halisi ni Mwana Fa & the Ay kwny ile kesi yao against tigo.
 
Nimesoma between the lines naona kama P-Funk ana point. Kuna unnecessary details kazitoa Prof Jay kwenye hilo bandiko lake na uwasilishaji wake wa point umekaa kimuhemko.

Ila mimi nauliza, ni nani mmiliki wa beats ? Je ni Producer au Msanii? Je kama msanii alilipa gharama za studio si ina maana ana ownership flani kwenye hiyo beat?
producer huwa analipwa chake
so obvious msanii ndio mmiliki maana huwa ananunua beats kwa producer
 
Kabisa Sema Prof J hakutaka kumkamia mwana na Majani anadai hiyo pesa kulikuwa na Kesi mahakamani mpaka akapata hilo gawio lakin ishu ni kuwa Prof J yeye hakuwa anafatilia wala kushiriki kwenye Kesi mahakamani so Hii pekee ndo sababu naona Majani anayo lakini kusema Yeye ndo anamiliki beat asilimia 100 Nooo ni uongoo ndo maana hata msanii akitumia beat la msanii mwingine Anaemind na kumshatki ni msanii mwenye beat SIO PRODUCER.
Inategemeana na makubaliano mkuu
 
Tuanzie hapa muziki ni wanani msaanii anayeuimba, mtunzi au producer??

Kwa sababu sijabobea kwenye maswala haya ya hati miliki na IP, nifahamisheni, kwa uelewa wangu producer analipwa kama kubarua tu wa kuutengeza muziki ukamilike. Ndio maana zile kwanya za mikoani miaka ile tulikuwa tunachanga kuwapa hela ya nauri nankurekodi kisha wanauza "kanda" aka tape

Au ni makubaliano
 
Huo ndo ukweli halisi....maana wimbo ulioleta hyo pesa ni ule wa chamilione alitumia beat ya nikusaidieje...prof alilalamika Sana kwamba jamaa katumia beat pasipo hata kupewa taarifa...naona wakapatanishwa ndo wakatoa Ngoma ya sivyo ndivyo....baadae Ile Ngoma ya chamilione bomboclat (aliyotumia beat ya nikusaidieje)ikachukuliwa na Walt Disney studios kama soundtrack ya movie aliyofanya lupita nyon'go (Queen of Katwe) ambapo chamilione alilamba km USD 50,000 km sikosei ....majani akapambana na yeye apate mgao maana lile beat alitengeneza...mzozo ukawa mkali kumpeleka mahakamani josee... nadhani mzigo ulivyotoka shida ndipo ilipoanzia..
Ukitaka kusoma kitu ambacho hakijaandikwa, unaweza kusoma lolote unalotaka.

Unaweza kisema Jay kaandika yeye ni Kim Jong Un, kiongozi wa Korea.

Kwa sababu katoa pozi la shavu kama Kim Jong Un.

Let's stick to the facts.
 
Nimeliona hilo lakini uandishi wake ndio shida.. labda kwakua ameshakua mwanasiasa
jay hajasema na p Jay kasema na cosota
usisaau ye ni mbunge kitu chochote cha uongo kitaaribu safari yake ya kisiasa
emb fikiria ccm waanze nae kwamba bila wao asingezipata izo pesa

think beyond mkuu jay ni mwanasiasa asaiv
 
Back
Top Bottom