Mmiliki halali wa beat ni aliyeitengeza au aliyeilipia ili aitumie?
Beat sidhani kama alipewa bure, sasa hata kama ameipigania hiyo kesi bado haiondoi ukweli kuwa baada ya kuitengeneza(Majani) ile beat alimpatia Professor J kwa malipo.
Hayo mengine nadhani COSOTA ndiyo chanzo baada ya kutoa taarifa isiyo sahihi, kulikuwa na kila sababu kwa Professor J ku'clarify, kama between the lines alikuwa anadai 'cut' flani kijanja tutabakia ku'speculate tu kwani ukweli wa moyoni mwake anaujua mwenyewe.
Kwa P Funk(Majani) kuwaka ni defensive mechanism ili Professor J asifikirie mgao kama alikuwa na wazo hizo japo COSOTA kama wakiona hawakutenda haki na ikaamuliwa vinginevyo halitakuwa suala la kutumia mabavu bali itatakiwa wafuate utaratibu utakavyoamuliwa.
All in all sidhani kama mambo yatabadilika, Majani ataendelea kuwa ndiyo mnufaika 100% kwani sitegemei Professior J kuvalia njuga hilo suala eti mpaka na yeye apate mgao.